Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 21,476
- 37,749
Katiba inasema Bunge ni uwakilishi wa wananchi. Bunge ndiyo sauti ya wananchi, Bunge ndiyo kisemeo cha Wananchi. Mbali ya upatikanaji wa kimagumashi wa bunge la sasa, lakini wao wenyewe wamejihalalisha na kusema ndio waliowekwa na Tume kuwawakilisha Wananchi. Moja kati ya kazi za uwakilishi wa Bunge ni kupokea, kujadili na kupitisha Bajeti ya serikali.
Serikali inaleta mapendekezo ya bajeti bungeni, Wabunge wanayapokea, wanayajadili, wanayachambua na kisha kuyapitisha. Hawatakiwi kupitisha bila kuchambua, na wanapochambua wanaondoa vipengele vyenye ukakasi au vinavyoelekea kuwa kero na kandamizi kwa wananchi kwa mwaka husika.
Katiba inawataka wafanye hivyo kwa Uhuru na kwa nia njema. Lakini kwetu imekuwa tofauti, tarehe 21.06.2021 Spika wa Bunge Job Agustino Ndugai alisikika akiwakoromea Wabunge KWAMBA, atakayethubutu kupinga na kutopitisha bajeti ya serikali atambue anajiandalia mwisho wake maana bunge likikataa bajeti ya serikali litavunjwa na Rais na kurudi kwenye uchaguzi ambao wengi waliopo hawatapita, nao wakaufyata.
Wakakubali kupitisha bajeti inayokwenda kuumiza Wananchi kwa kodi kandamizi zilizobatizwa jina bandia la "Uzalendo". Ongezeko la kodi ya mafuta tayari limeongeza nauli za mabasi na aina nyingine za usafirishaji. Leo 15.07.2021 ni siku rasmi ya kuanza kutumika kodi ya miamala ya simu ambayo kishindo chake kimetikisa haijawahi kutokea.
Sasa nauliza:
Ndugai na Wabunge wenzio mnamwakilisha Nani bungeni kwa kumrundikia Mtanzania mizigo ya kodi kichwani huku nyie mkikwepa kulipa kodi kutoka pato lolote mnalopokea?