Ungetumia njia nyingine kumpelekea taarifa hii, either kupitia mbunge wako au kumuandikia barua bila kutaja jina ingesaidia, hiki kijiwe hautapata jawabu.
 
Tutakukumbuka mtetezi
baba_keagan-___CM4rhQcFSQ____-.jpg
 
Mkuu Ngaliwe heshima kwako. Nadhani hujawa fare katika kuhitimisha hoja za wanaopinga mradi wa Bagamoyo (JPM na fans) na wanaoukubali mradi wa Bagamoyo (Ndugai & JK na Fans) . Nadhani taarifa ya mchakato ya huo mradi pamoja na Proposal ya wachina kuhusu huo mradi vingewekwa hadharani ili tujue nani ni mkweli na nani mwongo. Kumbuka yote tuliyoambiwa kuhusu uzalishaji wa Umeme kupitia mradi wa Gesi kutoka kule Mtwara.Tuliambiwa umeme wa Gas ni Ghali sana ILI kutengeneza Mradi mpya wa Umeme kwa sababu ambazo wahusika na Mungu ndio wanaozijua.

Ahsante
 
Hivi kwani Ndugai alivyokwenda huko China; moja ya Terms of Reference (ToR) ya hiyo trip yake ilikuwa ni kupewa hiyo "Presentation" kuhusu huo mradi wa Bandari ya Bagamoyo? Mimi sijamuelewa; anasema alikwenda kwa ajili ya mambo ya Bunge kuwa kidigitali; sasa hayo mambo ya Bandari yaliingiaje tena kwenye hiyo safari yake? Anadhani Wachina walikuwa wajinga kumfanyia hiyo "presentation" yeye? Kama Mwendazake alidanganywa; mbona hakuwahi kusema huo ukweli wakati huo?? Hapa Mama yetu inabidi awe Makini; inaonekana kuna watu wanataka kuutumia huu mwanya kujiwekea mambo yao binafsi sawa;kwa kisingizio cha maslahi ya Taifa, kumbe ukweli ni maslahi yao binafsi.
 
Imeandikwa na mdau mmoja Mitandaoni

BANDARI YA BAGAMOYO SPIKA NDUGAI YUKO SAHIHI

Najua topic imepita, lakini ninajua kidogo kuhusu mradi wa Bandari ya Bagamoyo na napenda kumuunga mkono Mhe Spika kwa hoja zifuatazo. Na naamini Serikali yetu itazichukulia kama ushauri wa Mbunge kwa Serikali, ambao ndio wajibu wetu wa msingi kama Wabunge.

Muhimu kujua background ya mradi wa Bandari ya Bagamoyo. Kwanza, mradi huu ulibuniwa na Serikali yetu kama Bagamoyo Special Economic Zone mwaka 2004 chini ya Mpango Kabambe wa Ujenzi wa Sekta Mpya ya Viwanda. Serikali ya Japan ndio ilitusaidia kwenye hili. Mradi huu uliitwa “Tanzania-Mini Tiger 2020” na ulikuwa chini ya Wizara ya Viwanda.

Mamlaka ya Bandari nayo ilibuni Mpango Kabambe wa Miaka 20 wa Uendelezwaji wa Bandari za Tanzania (The Tanzania Port Development Master Plan 2009-2028) ambao ulipendekeza Bandari ya Bagamoyo ijengwe katika miaka ya 2021/2022 ili iwe tayari kujaza nafasi baada ya Bandari ya Dar es Salaam kufikia ukomo wa kuweza kuongezewa uwezo. Kwahiyo mambo mawili ya msingi hapa ni kwamba: (a) Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo tuliubuni sisi wenyewe, ulikuwa sehemu ya mipango yetu ya muda mrefu na haukujengwa kwa msukumo wa Wachina; (b) mradi wa Bandari ya Bagamoyo sio ni mradi wa Bandari, bali ni mradi wa Ukanda wa Kiuchumi ambao unaendana na mji wa viwanda.

Mwaka 2009 Mamlaka ya Bandari, kupitia kampuni ya Hamburg Port Counsulting ya Ujerumani, ilifanya upembuzi yakinifu wa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo na
kuona una manufaa kutekelezwa. Mwaka 2011, Wizara ya Viwanda na Biashara, kupitia CowiConsult, nayo ilifanya upembuzi yakinifu wa Mradi wa Bagamoyo Special Economic Zone (BSEZ), kwa kufungamanishwa na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.

Mipango yote hii ilikuwa ni yetu wenyewe, na tulijiridhisha kama nchi kwamba Bandari ya Bagamoyo tunaihitaji na tukaiweka kwenye Mpango wa Pili wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya Taifa kama Mradi wa Taifa wa Kielelezo.

Mwaka 2013 na 2014, Kampuni ya China Merchants Ports Limited, ikiungana na Mamlaka/Mfuko wa Uwekezaji wa Oman (OIA), waliomba kuwekeza katika Mradi wa BSEZ na Bandari ya Bagamoyo. Baadaye kidogo, Korea Kusini nao, kupitia Taasisi yao ya Science and Technology Policy Institute” (“STEPI”) ilikamilisha Upembuzi Yakinifu wa kuwekeza katika kujenga na kuendeleza “Bagamoyo High Technology Park” kwa kushirikiana na EPZA pamoja na COSTECH. Kwahiyo hoja nyingine ya kuzingatia hapa ni kwamba Bagamoyo sio uwekezaji wa Wachina pekee, kama inavyodhaniwa. Yapo mataifa mengine. Oman wanaweka pesa yao nyingi. Na Korea Kusini nao wanaweka pesa na maarifa yao.

Kama nilivyoeleza hapo awali, kwa mujibu wa Mpango wa Pili wa Miaka Mitano wa Maendeleo (“FYDP II), Mradi wa Bagamoyo Special Economic Zone (BSEZ) ni Mradi wa Taifa wa Kielelezo. Mradi huo unatarajiwa kuwa utavutia uwekezaji wa Dola za Kimarekani bilioni 10; utakuwa na Viwanda 760 na hatimaye kutoa ajira 270,000 kwa awamu ya kwanza. Majadiliano ya Utatu wa Serikali ya Tanzania, China Merchants na Mfuko wa Uwekezaji wa Oman yalikuwa yanaendelea kuelekea makubaliano na hatimaye kuingia Mikataba ya Uwekezaji kabla ya kusimamishwa.

Zipo hoja kubwa tatu zinazosemwa kuhusu mradi huu: (1) utatutwika madeni kama vile Kenya na Sri Lanka ambapo Wachina walilazimika kutaifisha Bandari; (2) tutaua bandari ya Dar es Salaam; (3) haturuhusiwi kuendeleza Bandari yoyote na haturuhusiwi kutia mguu pale Bagamoyo kwa miaka 99.

Hoja hizi zote sio za kweli, na kwa kweli wawekezaji wa huu mradi wamekuwa wana-struggle namna ya kuzijibu kwasababu zinatolewa na watu wakubwa, na hao wawekezaji, hasa wa Oman, ni mamlaka za Serikali na wasingependa malumbano na Serikali yetu.

Hoja ya kwanza, kwamba tutakopa na kujitwika deni kubwa sio ya kweli: kwenye mradi huu hakuna hata senti tano ya mkopo tunachukua. Huu ni uwekezaji. Hakuna deni hapa, ni pesa ya kigeni inaingia kuwekezwa.

Hoja ya pili kwamba tutaua bandari ya Dar haina mantiki, kwasababu hata kabla Wachina hawajafika ilikuwa ni ndoto na mipango ya Mamlaka ya Bandari kujenga Bandari ya Bagamoyo. Ukisoma Mpango Kabambe wa Miaka 20 wa Uendelezwaji wa Bandari za Tanzania (The Tanzania Port Development Master Plan 2009-2028), wenyewe Mamlaka ya Bandari walitaka Bandari ya Bagamoyo iwe imejengwa ifikapo mwaka 2023. Bandari za Bagamoyo na Dar sio bandari shindani. Ni bandari zitakazosaidiana kuongeza shehena ya mzigo unaopita nchi mwetu. Full stop! Pia Bandari ya Bagamoyo itajengwa kwa kuzingatia teknolojia ya uundwaji wa meli za kisasa (4th Generation Shipbuilding Technology Port). Meli hizi, ambazo zitakuwa zinaongezeka kadri miaka inavyokwenda, haziwezi kutia nanga kwenye bandari ya Dar. Na kama unaitazama nchi kwa miaka 30, 50 ijayo, Bandari ya Dar ina ukomo wa upanuzi. Lazima kama nchi kujenga Bandari mpya kubwa katika ukanda huu ili kuendelea kunufaika na faida ya kijiografia.

Hoja ya tatu kwamba Wachina wanataka tusijenge wala kuendeleza Bandari yoyote kwa miaka 99 na tuwape wao bandari hiyo bila sisi kutia mguu pale sio ya kweli. Hakuna pahala popote wawekezaji wametoa hayo madai. Ukweli ni kwamba kote duniani mwekezaji anapoweka hela yake mwenyewe kwenye mradi atataka muda wa kutengeneza faida kabla hajakukabidhi mradi. Hapa Wachina na Wa-Oman walitaka miaka 33 ya concession. Je, ni mingi au ni michache? Inategemea pesa iliyowekwa (US$10bn) na standard practice kwingine duniani. Reli ya kuunganisha UK na France, ambayo imejengwa na sekta binafsi ina concession ya miaka 50. Kwa bandari standard practice ni miaka 25-40, kutegemeana na ukubwa wa uwekezaji. Cha msingi kwa timu ya negotiators wetu ni kupata financial models za wawekezaji na kuzichambua na kuona wanaanza kupata faida baada ya muda gani. Na cha kutambua pia ni kwamba concession inahusu tu faida ya Bandari na kwamba katika kipindi hiki cha concession bado TRA itakuwa inakusanya kodi nyingine zote husika za mizito bandarini.

Suala lingine la kutazama katika kufanya maamuzi ni kuangalia dunia inaelekea wapi kwenye biashara ya kimataifa. Tutake tusitake, nchi yetu inategemea biashara ya nje kimapato na China kwasasa ndio kinara wa biashara ya import and exports duniani. Inaongoza kwa kuagiza na kuuza bidhaa nje na itaendelea kuwa kinara kwa miaka 50 inayokuja. Ukifungamana nao, utashinda. Kwa mujibu mpango wa China wa Belt-and-Road-Initiative (BRI), meli kubwa za bidhaa zitakazopita katika 21st Century Maritime Silk Road kusafirisha bidhaa kati ya China na Afrika ya Kati na Kusini, zitafikia katika moja ya Bandari za Mwambao wa Mashariki ya Afrika, kama Mlango na Kituo Kikubwa cha kupokea, kuhifadhi kwa muda na kusafirisha shehena kwa meli au usafiri wa nchi kavu. Kulingana na kudra ya kijiografia ya Tanzania ambayo inaimarishwa na uwepo wa Reli ya Kati (SGR) tunayojenga pamoja na reli ya TAZARA, Bandari ya Bagamoyo ambayo itaunganishwa na Reli ya Kati na TAZARA, itakuwa haina mshindani Nje ya Tanzania katika dhana nzima ya ushirikiano wa maendeleo ya uchumi baina ya China na Afrika, kupitia BRI kwa muktadha wa 21st Century Maritime Silk Road.

Mwisho, ni muhimu kutambua kwamba kuna siasa za ushindani na majirani zetu kwenye hili suala. Jirani zetu Kaskazini yetu wanapigana kufa na kupona mradi huu usitokee. Kwahiyo mtaona disinformation nyingi kuhusu huu mradi huku baadhi ya watu wetu wakitumika bila kujijua.

Wenzetu tayari wameanza tena kuifuata kampuni ya China Merchant kuwashawishi wahamishie ule mradi Kenya kule LAMU. Mwaka 2018 wakati wa mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), kiongozi wao alikwenda Shenzen kuzungumza na China Merchant kuwashawishi waende kwao. China Merchat walikataa na ndio walikutana na Waziri Mkuu Mhe Majaliwa. Na majuzi, tarehe 25 Machi 2021 wameandika barua tena China Merchant kuomba mradi upelekwe kwao (barua nimeiona).

Mwisho, nitamalizia kwa hadithi ndogo: mwaka 1970, wakati Dubai bado ni kamji kadogo jangwani, wazungu waliona potential ya location ya Dubai kibiashara na wakamwendea mfalme wa wakati huo Rashid bin Saeed Al Maktoum kupendekeza wakajenge bandari na waiendeshe kwa miaka 30. Washauri wake wakamwambia tusiwape Wazungu bandari kwenye nchi yetu. Sheikh akawauliza “sisi tuna pesa ya kujenga?”, wakajibu hapana, akawauliza “tutaipata lini”, wakasema hatujui, akawauliza “Dubai itaendelea kuwepo miaka 30 ijayo?”, wakajibu ndio, akawauliza “baada ya miaka 30 wataing’oa bandari na kuondoka nayo?”, wakajibu hapana, akasema “tuwape”. Wazungu wakajenga Port Rashid mwaka 1972. Miaka 30 ikapita haraka. Watu wa Dubai wakajenga uwezo wa kuendesha bandari na wakaanzisha Dubai Port World (DP World), moja ya makampuni makubwa duniani. Dubai sasa ni kinara wa bandari duniani. Majuzi wamechukua bandari za Senegal na Angola. Na wamejenga bandari hadi Rwanda ambapo hakuna hata bahari, wanawasaidia Rwanda kwenye biashara ya logistics.

Mpendwa wetu hayati Rais Magufuli alipenda maendeleo. Alitaka nchi yetu ipate manufaa kwenye miradi na mikataba. Namna ya kumuenzi na kufanya makubaliano yenye tija kwa taifa kwenye mradi wa Bagamoyo. Na hilo linawezekana kama timu yetu ya negotiators itakuwa makini kuzingatia maslahi ya nchi.
 
Naomba nipingane na Mh. Spika 100%... Mungu njoo tusaidie, Mungu tusaidie, presentation sio sbb, ukubwa wa mradi sio sbb, mradi wa Bagamoyo utakausha nchi yetu na Rasilimali zote ndani ya miaka 99 au 50 ijayo, kila kitu kitakuwa kimeisha, sbb ukiwapa Chinese ku operate kwa 99 or 50 yrs alafu mmpewe kuendesha hiyo Bandari, itakuwa hakuna kitu hapa Tanzania.. Naumia sana kwa Ndugai kusema haya bila kuwa na datas, anasema ukubwa tu akidhania ndio faida, kumbe isiyo na faida..

Mungu tusaidie jamani.. Mungu tusaidie, Spika amekuwa very theorical badala ya kuangalia deep inside Chinese economic Intelligence yao, ni hatari sana.

Wachina wakishika Bandari wakijenga kwa miaka 99 hakuna kodi ya Bandari, hakuna kipato serikalini, we depend sana kwenye mapato ya bandari, hivi hata huo mshahara spika atapata kweli?

Miaka 99 au 50 tusiwe na Bandari, yaani Chinese millitary waendeshe, sisi tutamalizwa na madini na rasilimali zoteee zitaisha nchii yetu.. Yaani Spika bado hajawajua Chinese hadi leo hii anawaita marafiki? Mchina wa leo unamwita Rafiki?

Mungu tusaidie jamani
Nyie wajinga mlikuwa mnakula kodi zetu ,huku mkiwambia wahitimu wakajiajiri na huyo jiwe wenu ....


Sasa ni kila mtu kula keki ya taifa nyambafu
 
Kuna gap hapa hakuna original documents za mradi wa bagamoyo na masharti yake hapa. Sasa tunajadiana nini iwapo hatuna hiyo document hapa? huku ni kutwanga maji kwenye kinu.
 
Ndio maana miradi yote inabidi ijadiliwe Bungeni kwa uwazi na kupitishwa na huku ndio baadae huwa uwajibikaji wa pamoja. Wabunge wakiwakilisha wananchi. Lakini sio Bunge hili liliwekwa mfukoni mwa serikali.
 
Tangu lini mtanzania umfundishe na umlee atafuata nyayo zako na maono yako? Nyerere aliwalea wangapi na angalia matokeo. It's genenis
Eeenh Heee,

Akina Ndugai?

Lakini si angalau Mwalimu Nyerere wananchi walimwelewa, hata kama wananchi wenyewe hawana jinsi ya kuwaamrisha viongozi wao!

Lakini, Aaah, kwa masikitiko makubwa, naiona mantiki kwenye jibu lako.

Kuna kitu/jambo haliko sawa sana katika jumuia yetu.

Hili nimelitambua baada ya kuyaona yaliyojitokeza kwenye uongozi wa Magufuli.

Nchi hii yeyote akipata nafasi ya kukaa pale juu, anao uwezo wa kufanya chochote anachopenda bila kuhojiwa na yeyote.
Kama kuna mmoja, wawili, au wachache wakitoa mhanga kupinga, yakiwapata hayamstuwi yeyote, maisha yanaendelea kama kawaida; ikiwa ni pamoja na kuwasimanga hao "wapumbavu" waliohoji na kukipata cha mtema kuni.
Sifa zinamwendea mkandamizaji.
 
Sina uhakika Ila Maghufuli alitaka hao wachina wamsupport kwenye SGR badala ya bandari , istoshe isingempa sifa yyte sababu ni idea za Mzee wa msoga. Nao wakaingia mitini baada ya kuona SGR haina manufaa na ni complete loss hasa kwenye operations zake ukilinganisha na Bandari, Sina uhakika Sana Ila JPM alipiga U-Turn.

Ukweli ni kuwa jiwe hakutaka kuingiliwa ndo mana wasaidizi wake walimsupport ili wapate pa kula, Ndugai yupo sahihi ,mradi uangaliwe upya. Pengine Yule mchina aliyeenda chato alikuja na mission yake ya kummaliza jiwe. Nawaza Tu lakini
Mbona karibu miradi yote aliyoifanya iliasisiwa na Kikwete mf, upanuzi wa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.
 
`Nawasalimia kwa jina la JMT. Salamu ya mama inaakisi kichwa cha habari yangu. Magufuli alikuwa mwanadamu pambio za baadhi yetu kumtukuza ilikuwa ni mahaba makubwa waliyokuwa nayo juu yake, ukiachana na wale waliompamba kwa kilermba cha ukoka.
Nashauri tuachane na kumlaumu, kumkosoa na kumdhihaki kwani haitusaidi kama Taifa, turekebishe makosaa aliyofanya kama binadamu tusonge mbele.
  • Miruzi ya Wapinzani - Nashauri serikali iruhusu mikutano ya kisiasa hata kama hawako bungeni bado wanao uwezo wa kuibua madudu yanayofanywa na watendaji wa halmashauri zetu, taasisi za serikali na wizara zetu. Madudu mengi aliyoyabaini CAG katika maeneo mengi ni matokeo ya kutowapa wapinzani kukosoa na kusikika kwa madudu yao. Huenda Mhe. Rais na mamlaka nyingine husika zingechukua hatua haraka na isingejitokeza katika maeneo mengine.
  • Kanuni za kiutumishi zinazowalinda watumishi wakosoaji wa wakuu wao kufuatwa - Zipo kanuni za kudumu za kiutumishi zinazowalinda watumishi wa umma lakini wamekuwa wakinyanyaswa hasa wanapokuwa wazalendo wa kutaka taratibu za kiutumishi kufuatwa. wamekuwa wananyanyaswa na wakati mwingine kuhamishwa au kuondolewa katika nafasi zao. Ushahidi ni kitendo cha mama kuanza kuwarudisha katika nafasi zao baadhi ya watumishi walioondolewa kwa majungu na wakubwa zao wa kazi.
  • Rais kujizuia kuingilia utendaji wa mihimili mingine - Tunaona nchi za wenzetu kuna uhuru wa kutosha. Spika anaweza kukosoa maamuzi ya Rais aliyepo madarakani. Lakini kwa nchi yetu haiwezekani labda mpaka atokee madarakani kwa kusitafu au kufariki. Hii inaenda mpaka level ya chini. Kitendo cha Spika kukosoa kwa sasa baadhi ya maamuzi yaliyofanyika wakat wa utawala wa awamu ya Rais wa awamu ya tano ni ushahidi wa wazi kuwa hakuwa huru. Anaposema leo Rais alishauriwa vibaya kuhusu bandari ya Bagamoyo, anapohoji kuongeza ndege nyingine wakati ATCL inapata hasara ni ushahidi wa wazi wa mhimili wa Rais kujikita zaidi chini wakati mihimili mingine ikielea juu.
  • Kuruhusu demokrasia kushamiri - Kuruhusu uchaguzi ukio huru na haki, wapo watu ndani ya vyama vya siasa wanashinda kura za maoni lakini viongozi wanaweka watu wanaokubaliana nao, wapo wagombea ambao wamedai wamechaguliwa na wananchi kupitia vyama vyao lakini wameporwa ushindi wao na Tume zetu za uchaguzi au wamedai kufanyiwa figisu figusi na NEC. Wale wanaopitishwa kwa upendeleo wanakosa uhuru wa kuwasemea wananchi kwa kile wanachoamini kura ya mwananchi haijampatia ushindi wake.
Tujisahihishe kama taifa tusonge mbele. Kuibuliwa kwa madudu mengi na CAG ni matokeo ya watendaji na wanasiasa kumuogopa mtu mmoja na siyo wananchi. Taarifa ya CAG ijayo tutasikia bunge kuwalipa wabunge tisa viti maalumu ambao hawakutokana na chama chochote cha siasa., hii ni kutokana na kukosekana wa kupaza sauti kwa kulazimisha kuwapeleka bungeni wapinzani ambao wako bungeni kwa hisani ya spika. Wabunge ambao hawawezi kuikosoa serikali kwa kuhofia kufukuzwa pale spika akiamua kuhoji uhalali wao wa kuwepo bungeni. Tujisahihishe tusonge mbele.
 
Siyo kuwa ni confirmed hao walifukuzwa CHADEMA na hivyo wapo bungeni kwa uharamu wa ubabe wa Ndugai. Ndugai ni mhalifu wa bunge anafaa amfuate Jiwe
 
`Nawasalimia kwa jina la JMT. Salamu ya mama inaakisi kichwa cha habari yangu. Magufuli alikuwa mwanadamu pambio za baadhi yetu kumtukuza ilikuwa ni mahaba makubwa waliyokuwa nayo juu yake, ukiachana na wale waliompamba kwa kilermba cha ukoka.
Nashauri tuachane na kumlaumu, kumkosoa na kumdhihaki kwani haitusaidi kama Taifa, turekebishe makosaa aliyofanya kama binadamu tusonge mbele.
Ndugai na wanasiasa viongozi wengine wanaomkosoa sasa JPM wakati kila siku walisifu sera zake ni wanafiki tu. Tumerudi enzi za Siasa = Uongo + Manufaa binafsi
 
Ndugai itakuwa na yeye hana ufahamu.

Itakuwa kapewa commission na watu wa China bandari Bagamoyo
 
Lile soko likiendelea kuitwa ndugai itakua ni kumdhalilisha marehemu na haya yanayoendelea kwa huyu mchumia tumbo asiye na haya ,aliwahi mchapa mtu bakora kwa uchu wa madaraka .Nafikiri aliyelipa lile soko jina la ndugai alishauriwa vibaya, na mimi nikiendelea kuliona naghadhibika kuhusu maneno ya hiki kiumbe kisicho na chembe ya shukrani.
Kama sitofanikiwa kulivunja basi nikang'oe yale maandishi tu

Mwenyezi Mungu nisaidie nitimize adhima yangu!
 
Aise, hivi kama mtu aliyekuwa na kicha cha pembe nne kikawa cha duara kuna haja ya kuhangaika naye? Anyways soko letu tuachie tu halina kosa deal na wahusika.
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom