KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,189
- 17,157
Naona watu ambao sikutegemea kamwe kwamba tungekuwa upande mmoja nao, sasa inajitokeza hivyo, au nasoma vibaya?Ni kama waliojaribu kuuwa legacy ya Nyerere huwa wanatapa upinzani mkali hadi leo wakati Nyerere alishafariki zaidi ya miaka 20 iliyopita.
Watu huwa wanarejea hotuba tu.
Basi ngoja nikueleze kwa uchache: Magufuli alifanya kosa (yapo mengi, lakini naandika kuhusu kosa hili 'specifically')
Kosa lake hili ndio udhaifu wake mkubwa wa uongozi.
Hakuweza kuwatambua wasaidizi wake waaminifu, ambao angewalea na kuwaachia maono yake wayaendeleze. Yeye alijiona yeye tu basi, na nguvu zake kwamba atafanikisha anayotaka yafanyike.
Badala ya kuwafundisha wasaidizi wake waaminifu wapate uzoefu na kulinda hayo maono, yeye kawekeza kwenye kuwanunua watu kama akina Ndugae, kwa njia mbalimbali, mradi wasimzuie kufanya alichotaka kufanya. Hilo ndilo kosa lake kubwa, na linamtambulisha kipekee kabisa, na mbali kabisa na Mwalimu Nyerere.
Magufuli hakuwa na muda, wala uwezo wa kuwaeleza wananchi wakaelewa. Kuondoka kwake, kaondoka na kila kitu. Wananchi hawakubaki na kitu!
Mkuu 'kijogoodi' ukitaka kunisoma na kunielewa, utanielewa vizuri tu.