Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,779
18,746
Spika wa Bunge ameshauri mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo uendelee kwa sababu Magufuli alishauriwa vibaya, hii ni baada ya kamati ya Bunge ya bajeti kushauri kuwa serikali iangalie kuhusu kuendelea na mradi huo.

Ndugai amesema kuwa mradi huo utakuwa na faida kubwa kwa Watanzania na tukichelewa hatutauta tena.

Magufuli alisema mradi huo ulikuwa ni hasara kwani ulikuwa na masharti magumu ikiwemo ya kuzuia bandari yoyote kuendelezwa, wala TRA kukusanya kodi na kupewa lease kwa miaka 99.




Pia soma:

1)
Spika Job Ndugai: Kutokana na masharti ya Mradi wa Bandari Bagamoyo, ni sahihi Serikali kuusitisha

2) Rais Magufuli ataja sababu kusitisha ujenzi bandari ya Bagamoyo kwa Mkopo wa Dola Bilioni 10
 
Ukiangalia wabunge karibia wote waliopitishwa na tume kimagumashi wengine bila kupingwa (hata kupigiwa kura za ndio/hapana) ndio walikuwa wanamsifia sana JPM hata alipokosea na ndio ghafla wamebadilika na kujionyesha kumuunga mkono Mama pamoja na kukigeuka kila alichokifanya mwendazake!

So sad. Ndio makosa makubwa tunayoishi nayo kuwaweka watu wasio na sifa hata ya kumshauri na kumsimamia mwenyekiti wa kijiji kuwa washauri na watunga sheria wa taifa.

Ni mambo ya ajabu kweli lakini hii inadhihirisha kuwa tatizo la nchi hii ni CCM na kwa kiwango hiki cha unafiki hatutatawaliwa tena na UK/US/China au hata Kenya na SA bali tunakuja kutawaliwa na Comoro, Burundi na South Sudan!
 



Hapa Ndingai anaishangaa serikali kusitisha ujenzi wa bandari ya Bagamoyo. Anasema alikwenda China katika mji wa Chenzen ambako ndiko yaliko makao makuu ya wajengaji wa bandari. Walimuonyesha presention nzima a hakuona tatizo.

Pia wale wajamaa wanaoujua urafiki wa China na Tanzania wengi wamestaafu na wawili waliobaki waliwaambia wafanye haraka kufanya maamuzi ya ujenzi kwani wao of akiondoka, kizazi kipya kiko ki faida zaidi.
 
Kumaliza utata mkataba huo uwekwe wazi uanikwe hadharani. Wazee akina Ndugai musije achia vizazi vijavyo mizigo isiyowahusu si vizuri kurithisha kizazi kingine zigo Wanamchi tunaomba uwekwe wazi sababu ni wa miaka mingi pengine wote tuliopo hatutakuwepo duniani tutalaaniwa na vizazi vijavyo

Uwekeni wazi wanamchi tuseme kama una manufaa au la. Lakini kuongelea vitu tu gizani si sahihi sasa tutasemaje Magufuli alishauriwa vibaya na nani? Na Ndugai kashauriwa vizuri na nani? Mkataba wabunge wameuona?

Hiyo mikataba ya miaka mingi kupindukia hiyo iwekwe wazi
 
Hata ile somo la historia John Pombe Joseph Magufuli ataongelewa ukura mmoja, kwenye orodha ya marais.

Magufuli alikuwa dikteta sana.

Mwaka 2000 alimteka mgombea wa cuf ili asimpinge jimboni.

Mwaka 2005 alimteka Dr Sende, akazizuia boti zake kufanya usafirisha na akamteka na kumzuia asigombee ubunge.

2010 alipingwa na Dr Lukanima, mkufunzi wa uchumi Mzumbe, alifukuzwa kazi na akakimbilia uhamishoni Chile Magu alipokuwa Rais, kuna kijana mwingine alimpinga mwaka huo, baadae huyo kijana anaitwa Deusdedit, akapigwa uhujumu uchumi hadi leo yupo lupango. Alikuwa mtumishi NEMC.

Idara ya usalama, msijaribu kuruhusu mtu type yake kuwa Rais au makamu.

Tumshukuru sana Mungu.
 
Kwani hao washauri walishikiwa Bunduki hadi kumshauri mwendazake vibaya?

Unaweza kuta washauri wale wale waliomshauri JPM kutotekeleza mradi kwamba hauna manufaa makubwa kwa Nchi ndiyo hao hao wanashauri mradi Mhe. Samia Suluhu kuutekeleza kwa kuwa wamegundua Una manufaa kwa Nchi mara hii.

Tanzania kinachotugharimu ni Unafiki, Woga na kuendekeza Majungu.

Imagine kama mradi ungetekelezwa 2016 leo hii si ingekuwa Meli zimeanza kushusha na mzigo hapo. Tumekubali kuyumbishwa na siasa uchwara hatimaye tumepoteza zaidi ya maTrilioni kwenye Ushuru na Kodi.
 
Chungeni sana kauli hizi za Spika. Ali mu-outsmart prof mmoja aliye kuwa hajui kuwa hajui.
 

Hapa Ndingai anaishangaa serikali kusitisha ujenzi wa bandari ya Bagamoyo. Anasema alikwenda China katika mji wa Chenzen ambako ndiko yaliko makao makuu ya wajengaji wa bandari. Walimuonyesha presention nzima a hakuona tatizo.

Pia wale wajamaa wanaoujua urafiki wa China na Tanzania wengi wamestaafu na wawili waliobaki waliwaambia wafanye haraka kufanya maamuzi ya ujenzi kwani wao of akiondoka, kizazi kipya kiko ki faida zaidi.

Clip ya Muda
 
Back
Top Bottom