Ndugai: Tumshughulikie Zitto kama Bunge la Marekani linavyomshughulikia Rais Trump

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema kama Bunge la Marekani linamshughulikia Rais wa nchi hiyo, Donald Trump kwa vitendo vya kukosa uzalendo, kwa nini isiwe kwa mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe ambaye amefanya kitendo cha kuisaliti kwa nchi.

Spika Ndugai amesema hayo jana Ijumaa Januari 31, 2020 bungeni mjini Dodoma wakati akihitimisha hoja iliyoletwa na Mbunge wa Siha (CCM), Dk Godwin Mollel.

Dk Mollel amewasilisha hoja binafsi bungeni akiwashauri wabunge wamuunge mkono kufikia uamuzi wa kumchukulia hatua Zitto kwa kitendo chake cha kuandika barua Benki ya Dunia (WB) akitaka Tanzania isipewe mkopo wa Dola 500 milioni za Kimarekani kwa ajili ya sekta ya elimu.

Spika Ndugai amewaambia wabunge kuwa jimboni kwake baadhi ya shule wanafunzi hawana madawati wanakalia vigoda vya miguu mitatu.

Pia, amesema kuna shule ya sekondari ina vyoo viwili, kimoja kinatumia na watoto wa kike na kingine kinatumiwa na wavulana.

Spika Ndugai amesema kitendo cha Zitto ni usaliti kwa kuwa fedha hizo zingesaidia kuondoa changamoto nyingi kwenye sekta ya elimu.

Mbunge wa Chemba (CCM), Juma Mkamia akichangia hoja ya usaliti wa Zitto ametoa mfano wa Wamarekani kwamba rais wake anayesaliti Taifa lao hawamuachi salama. Amesema kuna haja Bunge likachukua hatua kwa watu kama Zitto.
 
Lakini naona ajabu moja kubwa. Kipi bora kutumia hela za ndani au kukopa ili kuimarisha elimu. Huduma za jamii kama elimu na afya zingetumia hela za ndani halafu mikopo itumike kujenga miundo mbinu kama reli, ndege na umeme.
Sisi tumefanya kinyume chake. Anyway kukopa muhimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nani anaweza kuthibitisha kuwa fedha hizo zingesaidia kutatua matatizo yaliyotajwa na Spika kama special case?

Miaka zaidi ya 57 ya Uhuru tunaongelea watoto wetu kukalia vigoda shuleni na vyoo matundu mawili na bado tunaona ni sawa huku tukingoja fedha za wahisani!!

Kuhusu hilo alilofanya Zitto kisiasa anayo nafasi japo lina madhara yake pia.
Kila mmoja anatakiwa kubadili fikra na mitazamo yake ili kujenga taifa kwa umoja na siyo kwa mtindo wa kushambuliana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Masikini nchi yangu 🇹🇿😭😭😭 nakulilia Tanganyika. Kama taifa tumepoteza miaka 4 bure bure kabisa.
Nchi inaangamia kwa kukosa maarifa.
 
Fedha za mikopo huja na MASHARTI yake, siyo rahisi kuwa na dhamira ya kuleta mapinduzi katika Elimu kwa kutegemea mikopo.

Tukope tunapopungukiwa huku tukitumia rasilimali zetu vizuri.
Mikataba yetu pia siyo rafiki, japo tumeafanywa kuamini kuwa mambo ni shwari
Lakini naona ajabu moja kubwa. Kipi bora kutumia hela za ndani au kukopa ili kuimarisha elimu. Huduma za jamii kama elimu na afya zingetumia hela za ndani halafu mikopo itumike kujenga miundo mbinu kama reli, ndege na umeme.
Sisi tumefanya kinyume chake. Anyway kukopa muhimu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app[/i]
 
Back
Top Bottom