Ndugai: Nusu ya watumishi wa Bunge ni mzigo

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,156
2,000
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, amesema karibu nusu ya watumishi wa Taasisi ya Bunge ni mzigo.

Aliyasema hayo jana wakati akichangia katika semina ya wabunge ya Mfumo Mpya wa Usimamizi na Ufuatiliaji wa Miradi ya maendeleo ili kupata matokeo makubwa sasa.

Lengo la semina hiyo lilikuwa ni kuongeza uelewa kwa wabunge juuya Taasisi ya Rais inayojulikana kwa lugha ya Kiingereza kama Presidential Delivery Bureau (PDB).

"Tatizo kwenye halmashauri kumejaa wazembe, hata hapa (Bunge) tuna karibu nusu ya watumishi mzigo, mtupe namna ya kuwaondoa wazembe," alisema. Ndugai alisema si kwamba watumishi wanaonekana katika Bunge wote ni wazuri.

Alisema suala la uwajibikaji ni dogo nchini na kutaka Tume ya Mipango kutoa njia mbadala ili watumishi waserikali wazembe waweze kuwajibishwa. "Uwajibikaji ni mdogo, tuna watumishi wa kawaida hakuna kazi wanayoifanya, mwalimu wa sekondari unakuta kwa miaka mitano mfululizo anafelisha anaachwa tu, hakuna wa kumuandikia onyo wala kumwajibisha," alisema.

"Kwa kadri tunavyoendelea hivi hatuna namna ya kuchukuliana hatua hatutakwenda popote pale." Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamo Rais (Mazingira), Terezya Huviza, alitaka watumishi watakaochaguliwa kuunda PDB, wawe waaminifu wasiopenda kujilimbikizia mali.

Alisema bila kufanywa kwa ukaguzi mzuri kabla ya kuwaweka katika PDB, mfumo huo utakufa.

"Sisi wenyewe (wabunge), tumejichanganya, sisi ndio wafanyabiashara hatutaki kulipa kodi lazima tuchague kitu kimoja kama uongozi ama biashara," alisema.

Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Lugola, alisema tatizo la kupanda kwa bei ya sukari linaletwa na serikali.

Alisema wenye viwanda wanazalisha kidogo ili wapate vibalivya kuagiza sukari kwa msamaha wa kodi. Mbunge wa Longido (CCM), Lekule Laizer, alisema uzalendo nchini umepotea na kwamba miradi mbalimbali inayotekelezwa imejaa rushwa.

"Rushwa wakati mnaanza utekelezaji hadi mnapomalizia mradi hauna kiwango cha ubora, unakutaka mradi mzima umejaa rushwa," alisema. Alilitaja tatizo jingine ni ukiritimba katika fedha zinazotolewa katika kukuza uchumi almaarufu kama mabilioni ya JK kwamba zimekuwa zikitolewa kwa ukiritimba.

Alitoa mfano wa halmashauri ya Longido ambayo ilipangiwa Sh. milioni 250, ni Sh. milioni 40 tu ambazo zimeshatolewa hadi sasa huku nyingine zikishikiliwa katika mabenki.

Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu, alisikitishwa na mada zote katika semina kuandaliwa kwa lugha ya Kiingereza wakati walio wengi ni wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili.

"Mada zote zimeandaliwa kwa lugha ya Kiingereza ni kwa ajili ya mfadhili yupi? Huu ni ugonjwa mkubwa, tatizo ni kuwa ombaomba," alisema. Mbunge wa Ngara (CCM), Deogratius Ntukamazina, alitaka uteuzi wa nafasi mbalimbali za uongozi kuzingatia uwezo wa watu.

"Kama appointment (uteuzi) zetu zitaendelea kuwa na misingi ya udini, urafiki na ukabila, uwajibikaji na kuwajibishana hautawezekana,"alisema. Mbunge wa Muhambwe (NCCR-Mageuzi), Felix Mkosamali, alisema lazima kuwa na watu wenye upeo mkubwa na wenye kujiwekea malengo makubwa.

Alisema iwapo watu kama hao hawapo wajue kabisa ni kupoteza muda kwa kuwa mfumo huo hautafanikiwa. Alihoji taasisi hiyo si ya kwanza na kwamba ipo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imefanikiwa katika mambo gani.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dk. Philip Mpango, alisema kujikosoa na kubadilika kwa kujifunza kutokana na uzoefu wa siku za nyuma au nchi nyingine zilizofanikiwa ni hatua ya unyenyekevu na ya kimaendeleo.

"Vivyo vivyo kukosoa kunakoambatana na mapendekezo ya njia mbadala zinazotekelezeka nikitendo cha uzalendo na muhimu wamaendeleo na ustawi wa Taifa,"alisema hayo wakati akiwasilisha mada yake ya Mfumo Mpya wa Usimamizi na Ufuatiliaji wa Miradi ya Maendeleo ili Kupata Matokeo Makubwa Sasa.

CHANZO: NIPASHE
 

Dina

JF-Expert Member
Sep 18, 2008
3,059
1,500
Na huo uajiri wenu usiojua kufukuza wazembe/wafujaji kazini, mtawafukuza kweli? Mkijitahidi sana mnawapa transfer waende Tandahimba! Hiyo ndiyo adhabu kuuubwaaa.....wakati wengine ndio wanaishi huko miaka yote.
 

Mamndenyi

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
30,830
2,000
wamejazana huko na watoto wao na wajukuu zao
ambao wote walikataa shule, unategemea kuwa na watu gani zaidi ya mizigo.
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
43,635
2,000
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, amesema karibu nusu ya watumishi wa Taasisi ya Bunge ni mzigo.

Alisema suala la uwajibikaji ni dogo nchini na kutaka Tume ya Mipango kutoa njia mbadala ili watumishi waserikali wazembe waweze kuwajibishwa. “Uwajibikaji ni mdogo, tuna watumishi wa kawaida hakuna kazi wanayoifanya, mwalimu wa sekondari unakuta kwa miaka mitano mfululizo anafelisha anaachwa tu, hakuna wa kumuandikia onyo wala kumwajibisha,” alisema.

CHANZO: NIPASHE
Hili swala la uawajibikaji lingeanzia kwa Waziri wa Elimu, Matokeo ya kidaoto cha nne mwaka 2012 yangekuwa kigezo cha waziri angewajibika moja kwa moja. Wakurugenzi katika wizara pia waonyeshe utendaji kazi wao.

Mishahara ya walimu ingerekebishwa na pia viwango vya elimu kwa ujumla. Mwalimu wa secondary awa na sifa ya elimu si chini ya chuo kikuu. Hii itasaidia kupatikana kwa ajira kwa vijana na pia kuinua hadhi ya kazi ya ualimu.

 

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Sep 18, 2010
8,404
2,000
Yeye ni mzigo mkubwa kuliko hao anaowasema. Kama wazazi mnazaa watoto vilaza lazima mjitazame wenyewe, ****** na Makinda wajitazame kwanza wao
 

Bobuk

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
5,875
1,500
Huyu Ndugai aache ku-fire around the bush. Aseme nusu ya WABUNGE na hasa wa CCM na kiti cha Spika ni MZIGO.

Ndugai acha mchezo wa HIDE AND SEEK (read KOMBOLELA) kwa kusingizia watumishi wa BUNGE. Nyinyi Wabunge wa CCM ndiyo mzigo gunia la misumari kwa walipa kodi wa Tanzania.
 

Mtingaji

JF-Expert Member
Sep 28, 2012
1,209
1,225
wamejazana huko na watoto wao na wajukuu zao
ambao wote walikataa shule, unategemea kuwa na watu gani zaidi ya mizigo.
Nakubaliana na wewe kwani kwa uzembe wao wametengeneza tatizo kwa kuweka wazembe, sasa wanashindwa jinsi ya kutatua tatizo kuondoa uzembe kwa sababu ya uzembe wao.

Akili ndogo inatawala akili kubwa!
 

Mtoboasiri

JF-Expert Member
Aug 6, 2009
5,101
0
Sijawahi kukubaliana na Ndugai hapo kabla (maana almost always huongea pumba) lakini kwa hili I agree with him all the way. Lakini si watumishi wa ofisi ya bunge tu, nadiriki kusema at least 80% ya watumishi wa serikali - especially wa ngazi za juu - ni mzigo hasa. Na haya ndio matunda ya kuajiri watu kwa kujuana badala ya kuangalia merit.

cc. Pasco, Majebere, Rejao, Chama, Nape, Mwigulu, Lukosi et al!
 

Sanoyet

JF-Expert Member
Apr 3, 2013
1,324
1,225
Ndugai mwenyewe ndo mzigo na ni janga la Bunge tukutu la jamhuri ya muungano wa Tz.
 

Mercyless

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
652
250
Na yeye pia ni mmoja wa hiyo mizigo. Hana la maana analolifanya kwa manufaa ya nchi yetu.
 

Manyi

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
3,254
1,195
Mbona wakiwa ndani ya bunge wakiambiwa kweli wanang'aka pasipo sababu? Wabunge wa CCM ni janga la kitaifa
 

UmkhontoweSizwe

JF-Expert Member
Dec 19, 2008
3,841
2,000
Angekuwa siyo mzigo angalau angekuwa hata na hekima kidogo ya kujua kusimamia mijadala ya bunge.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom