ndugai..;‘Msiandike mabaya tuuu, andikeni mazuri pia’ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ndugai..;‘Msiandike mabaya tuuu, andikeni mazuri pia’

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sir.JAPHET, Aug 13, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Monday, 13 August 2012 08:13

  Daniel Mjema, Dodoma
  NAIBU Spika wa Bunge, Job Ndugai, amewataka waandishi wa habari nchini kuandika habari zitakazowapa picha halisi ya maendeleo makubwa yaliyofikiwa na nchi tangu kupata Uhuru badala ya kuandika machache mabaya.

  Ndugai alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua semina ya wanahabari wanaoripoti habari za Bunge na kuwataka wanahabari kutumia kalamu yao vizuri kuielimisha jamii katika masuala mazima ya kujiletea maendeleo yao.
  Ndugai alifafanua wapo baadhi ya wanahabari wanaoandika habari kwa kuziongezea chumvi, wengine wakiandika habari zisizo za kweli na wengine kutumiwa kueneza propaganda jambo ambalo haliwatendei haki Watanzania.

  “Mfano wa propaganda ni kwamba miaka 50 ya Uhuru hakuna maendeleo…Wilaya ya Kongwa pekee hivi sasa ina matrekta 400 wakati huko nyuma hatukuwa na hata jembe la kukokotwa na ng’ombe leo unasema hakuna maendeleo,”alisema Ndugai.

  Ndugai alisema nchi kwa sasa inasonga mbele na kama kuna watu wanalala hiyo ni shauri yao na kuwataka waandishi kuandika yaliyo mazuri badala ya kujikita kwa machache mabaya na kutaka viongozi waliofanya mazuri wapewe nishani na kutambuliwa.
  “Tuchukue mema na tuandike yaliyo mazuri, tutafute mtu aliyefanya mazuri tumpe nishani au tumtambue tusitafute mabaya yake hatuwezi kusonga mbele kwa staili hii”alisisitiza Ndugai wakati akifungua semina hiyo.

  Ndugai alitolea mfano wa suala la Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye kumiliki ekari 150 katika Jimbo la Kongwa namna lilivyokuzwa na wanahabari na baadhi ya wabunge na kuonekana kama ni tatizo.
  “Kule Kongwa wapo wakulima wa kawaida kabisa wenye ekari 400 wengine 600 na hata 1,200, lakini Sumaye alikuwa na ekari 150 tu ilikuwa issue (hoja) mara fisadi jamani! hebu tutoke huko”alisema.

  Ndugai alisema hata wakati wa utawala mwalimu Julius Nyerere ulikuwapo upungufu, lakini Watanzania wanakumbuka na kumuenzi kwa mengi mema na mazuri aliyoifanyia nchi tangu Tanzania ilipopata Uhuru wake miaka 50 iliyopita.
   
 2. d

  davidie JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 329
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mheshimiwa sana ndugai! Kinyesi ni kinyesi tu hata kama kilitoka kwenye tumbo la mtu aliyekula pilau, kwa maana hiyo hata kama ccm na serikali yake emefanya mazuri machache bado uozo uko pale pale kwa kuwa ufisadi na rushwa bado vipo mikononi mwenu na mioyoni mwenu.
   
 3. a

  andrews JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  2015 msilete mgombea urais anayeanguka hadharani hovyohovyo CCM
   
 4. a

  ashakum Member

  #4
  Aug 13, 2012
  Joined: Apr 25, 2012
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata wewe mwandishi wa habari hii una matatizo. Wewe umeona hii ni habari ya kuandika? Umeacha habari za maana unaandika hii? Ndugai ndumila kuwili, pia ni mchumia tumbo tu huyo. Hukumbuki alisema zarau zenu huko huko? Ni mazuri gani anayoyaona yeye yatauza magazeti yakiandika? Wewe hujui maana ya habari na soko linataka nini? Andika hizo habari anazotaka Mungai uone kama utauza gazeti.
   
 5. a

  ashakum Member

  #5
  Aug 13, 2012
  Joined: Apr 25, 2012
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyuma ni lini ambako hakukuwa hata na jembe la kukokotwa na ng'ombe Ndugai? Hukumbuki wakati wa siasa ni kilimo kila kijiji kilipatiwa trekta hapa nchini tena ilikuwa miaka ya 70 na 80. Zamani ipi hakukuwa na matrekta? Hayo matrekta 400 ya nani kama sio ya watu walioiba hela benki kuu na kuamua kununua mashamba kila mahali hapa nchini? Anasifia wezi kumiliki utajiri? Serikali imefirisika siku hizi hata madeni ya walimu wameshindwa kulipa.
   
 6. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #6
  Aug 14, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  tatizo ni kwamba safari hii uozo ni mwingi kulinganisha na nukta tu ya uzuri.atuambie zuri alilolifanya zaidi ya kumtumia lukuvi kuzima hoja.mariemu ni mariemu tu.
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Aug 14, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,801
  Likes Received: 83,172
  Trophy Points: 280
  Kwanini yeye asiyataje hayo maendeleo? Yamepatikana katika wizara (z)ipi? ya afya, elimu, usafiri, uchumi, maliasili, madini na nishati, mambo ya ndani/nje? Kote tu kumejaa madudu hakuna hata moja la kujivunia.
   
 8. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #8
  Aug 14, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  aaaaah,hahahaha ni NDUGAI MDAU,
   
 9. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #9
  Aug 14, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  hapa ukisema utaje wizara,basi umechafua hali ya HEWA
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Aug 14, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,801
  Likes Received: 83,172
  Trophy Points: 280

  Hali ya hewa imeshachafuka miaka mingi Mkuu, ndiyo maana wanatapatapa ili yaandikwe mazuri ambayo hatuyaoni.
   
 11. zubedayo_mchuzi

  zubedayo_mchuzi JF-Expert Member

  #11
  Aug 14, 2012
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 4,922
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Nchi haina maendeleo hayo ya kuandikwa,kuna maendeleo ya kundi la watu wachache.
   
Loading...