Uchaguzi 2020 Ndugai: Mimi ndio Spika wa Bunge, nawajua Wabunge wote. Hao wapinzani hawajawahi kuwatakia maendeleo watanzania maana wao kila kitu hupinga tu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,492
9,266
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kondoa kimezindua rasmi kampeni zake za Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kondoa Mji, Makoa Ally ambapo mgeni rasmi alikua Spika wa Bunge na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Job Ndugai.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Spika Ndugai amewaomba wananchi wa Kondoa wasifanye makosa katika kuchagua wawakilishi wanaojua kero zao na wenye kuweka mbele maslahi yao ili waweze kuwasemea.

" Ndugu zangu nyie wote mmejionea jinsi Dk Magufuli alivyoufanya mkoa wetu wa Dodoma kupanda chati, uchumi wetu sasa hivi umekua baada ya kuwa makao makuu ya serikali huku yeye mwenyewe akihamia hapa, nini cha kumpa zaidi ya kura za kishindo?

Mimi ndio Spika wa Bunge, nawajua wabunge wote, hao wapinzani hawajawahi kuwatakia maendeleo watanzania maana wao kila kitu hupinga tu, wanasema Rais anatumia hela hovyo kununua Ndege lakini kesho utawakuta wamezipanda, wanatumia barabara za lami kwenye kampeni zao lakini wanasema hakuna lililofanyika.

Kondoa ni wakati wa kuamka na kutoa kura nyingi za kuwafanya wapinzani wajute kwanini wameshiriki uchaguzi huu, niwahakikishieni mkimleta Makoa bungeni nitamsaidia sana katika kuwaletea maendeleo," Amesema Ndugai.

Kwa upande wake mgombea Ubunge wa Jimbo hilo la Kondoa Mji, Makoa Ally amesema anafahamu changamoto nyingi zinazowakabili wananchi wa Kondoa lakini kero ya Maji ndio kipaumbele chake cha kwanza.

" Najua kuna mambo mengi ya kufanya ila nyinyi wenyewe ni mashahidi kwamba hakuna jambo la muhimu Kondoa kwa sasa kama Maji, niwaombe nipeni ridhaa ya kuwa Mbunge wenu nikashughulike na maji ili dhana ya kumtua mwanamama ndoo kichwani iweze kutumia," Amesema Makoa.

Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na msanii wa Bongo Fleva, Keisha amewaomba watanzania na wananchi wa Kondoa kuchagua mafiga matatu ya CCM ili yaweze kufanya kazi kwa ushirikiano na kusukuma gurudumu la maendeleo mbele.

" Chagueni Rais, Wabunge na Madiwani wetu, msipowachague wote kwa pamoja mnakwamisha maendeleo maana wapinzani wale ni kupinga tu sasa watu wanaopinga maendeleo ni ngumu kuikumbusha serikali iwajengee visima vya maji maana wao wanasubiri serikali ijenge ili wapinge, naombeni msifanye kosa Oktoba 28, kura zote kwa CCM," Amesema Keisha.
 
Ndugai bwana, anafikiri waTz wote wameishageuzwa misukule!! Wapo wengi ambao wanao ufahamu wao. Wanafahamu kuwa wabunge wa upinzani wanachokifanya sio KUPINGA KILA KITU bali KUHOJI KILA KITU ili kinachofanywa na serikali kiwe na manufaa yanayostahiki au kisiwe na vimelea vya ufisadi.

Huo ndiyo wajibu wa msingi wa mbunge na wabunge wa upinzani wameonesha kuutendea haki. Sasa kwa propoganda mfu za CCM wamekazana kuwaaminisha misukule kuwa KUHOJI ni KUPINGA!!
 
Hivi kupinga kila kitu ni tatizo kama mtu ana hoja nzuri zaidi?

Kukubali hoja dhaifu zisizo faa, ni ubora?

Kama mtu ni dhaifu na ni yule yule anaendeea kutoa mau-shoes ni busara kwa mtu mwenye akili na ufahamu kuzikubali eti kwa kuwa ataonekana anapinga kila kitu? Huu siyo uhujumu wa maendeleo ya watu?

Ndugai anapashwa kujua kuangalia picha hata kama kusoma hajui.
"Ni dhahiri kwamba wenye akili walishatambua sababu za CHADEMA kupinga ma-uviatu. Ni kwamba wana hoja thabiti na za maana zaidi ya hayo mau-viatu na ndiiyo sababu "WAKAAMUA KUCHUKUA SERA NZIMA NZIMA ZA CHADEMA NA KUJARIBU KKUZITEKELEZA" . Kujaribu kuzitekeleza huko ndiko anakuita maendeeo.

Huyu mtu niaje? Ni zaidi ya fedheha.
 
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kondoa kimezindua rasmi kampeni zake za Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kondoa Mji, Makoa Ally ambapo mgeni rasmi alikua Spika wa Bunge na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Job Ndugai.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Spika Ndugai amewaomba wananchi wa Kondoa wasifanye makosa katika kuchagua wawakilishi wanaojua kero zao na wenye kuweka mbele maslahi yao ili waweze kuwasemea.

" Ndugu zangu nyie wote mmejionea jinsi Dk Magufuli alivyoufanya mkoa wetu wa Dodoma kupanda chati, uchumi wetu sasa hivi umekua baada ya kuwa makao makuu ya serikali huku yeye mwenyewe akihamia hapa, nini cha kumpa zaidi ya kura za kishindo?

Mimi ndio Spika wa Bunge, nawajua wabunge wote, hao wapinzani hawajawahi kuwatakia maendeleo watanzania maana wao kila kitu hupinga tu, wanasema Rais anatumia hela hovyo kununua Ndege lakini kesho utawakuta wamezipanda, wanatumia barabara za lami kwenye kampeni zao lakini wanasema hakuna lililofanyika.

Kondoa ni wakati wa kuamka na kutoa kura nyingi za kuwafanya wapinzani wajute kwanini wameshiriki uchaguzi huu, niwahakikishieni mkimleta Makoa bungeni nitamsaidia sana katika kuwaletea maendeleo," Amesema Ndugai.

Kwa upande wake mgombea Ubunge wa Jimbo hilo la Kondoa Mji, Makoa Ally amesema anafahamu changamoto nyingi zinazowakabili wananchi wa Kondoa lakini kero ya Maji ndio kipaumbele chake cha kwanza.

" Najua kuna mambo mengi ya kufanya ila nyinyi wenyewe ni mashahidi kwamba hakuna jambo la muhimu Kondoa kwa sasa kama Maji, niwaombe nipeni ridhaa ya kuwa Mbunge wenu nikashughulike na maji ili dhana ya kumtua mwanamama ndoo kichwani iweze kutumia," Amesema Makoa.

Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na msanii wa Bongo Fleva, Keisha amewaomba watanzania na wananchi wa Kondoa kuchagua mafiga matatu ya CCM ili yaweze kufanya kazi kwa ushirikiano na kusukuma gurudumu la maendeleo mbele.

" Chagueni Rais, Wabunge na Madiwani wetu, msipowachague wote kwa pamoja mnakwamisha maendeleo maana wapinzani wale ni kupinga tu sasa watu wanaopinga maendeleo ni ngumu kuikumbusha serikali iwajengee visima vya maji maana wao wanasubiri serikali ijenge ili wapinge, naombeni msifanye kosa Oktoba 28, kura zote kwa CCM," Amesema Keisha.
Hivi Speaker Ndugai anaamini kuwa ataendelea kuwa speaker wa bunge ?
 
Ndugai hana akili mzuri, yaani kwake mbunge mzuri ni yule anaye kubali kuburuzwa tu bungeni?
Kwani Mbowe anavyowaburuza wabunge wa Chadema mara awatoe nje, awabandike maplasta midomoni, awakate mishahara nk. Huwa Wana akili nzuri?
 
Siasa za upinzani za kitoto mno mfano unakuta wanapinga umunuzi wa ndege ili ubaki huna ndege ukibaki huna ndege uchaguzi ukiwa wanaanza kuponda nchi gani isiyokuwa na ndege ndege mijini tupeni kura tutanunua ndege.

Upinzani wa Tanzania ni wa kitoto na wa kijinga
 
Siasa za upinzani za kitoto mno mfano unakuta wanapinga umunuzi wa ndege ili ubaki huna ndege ukibaki huna ndege uchaguzi ukiwa wanaanza kuponda nchi gani isiyokuwa na ndege ndege mijini tupeni kura tutanunua ndege

Upinzani wa Tanzania ni wa kitoto na wa kijinga
Kama wewe unavyo ongoza kwa kupost ujinga kila kukicha.
 
Ndugai amekuwa rubber stamp ya serikali, Bunge butu haliwezi kuishauri na kusimamia serikali. Maslahi ya watanzania bunge limekuwa msaliti chini ya Ndugai.

Wakati Magufuli anaingia madarakani sukari ilikuwa kati ya 800 na 1200 Kwa Kilo Moja. Mwaka 2016, Magufuli akaingilia Biashara ya sukari na sukari ikapanda hadi 2400.

Mwaka 2016 Magufuli alisema Matajiri wataishi kama Mashetani...alidhamiria watanzania wakose pesa, na hakusema masikini wataishi kama malaika
. Akafanya matendo makuu ya bomoa bomoa kimara bila fidia, akapora fedha za wafanyabishara za Bureu De Change, maelfu ya wafanyakazi wakakosa ajira. Mpaka leo Magufuli hajatoa riporti kwa umma kuwa ni pesa kiasi gani alichukua?

Mwaka 2019, Magufuli akaingilia tena na Sukari ikapanda, sasa sukari ni 2600 hadi 2800 Tshs

Ukiangalia mikoa Pwani, Kibaha, Chalinze, etc. Sukari ni muhimu na kipato ni kidogo.

Angalia sukari ya Malawi, Brazil, Thailand ni rahisi kuliko ya Tanzania. Why. Mfumo wa kodi ni mbovu

Burundi na Rwanda kuagiza gari ni rahisi zaidi kuliko Tanzania, wakati magari yao yanapita bandari ya Dar es salaam.

Pia ukiangalia Ngome za CCM Chalinze, Morogoro Dodoma, Shinyanga, .., nyumba za tembe ni nyingi...Gharama za ujenzi ni kubwa mno. Cementi ni ghali sana... Hakuna sababu cementi kuwa ghali sana. Maana ni mali ghafi ya hapa hapa nchini...Mfano, Mtu akiagiza Cementi Pakistani, anakuja kuuza bei chini kuliko Simba au Twiga Cementi. Bado cement ya nje kuna usafirishaji, kodi ya taifa lao na VAT ya Tanzania. Kama alivyosema Mh. Tundu Lisu, kuna tatizo TRA.
 
Siasa za upinzani za kitoto mno mfano unakuta wanapinga umunuzi wa ndege ili ubaki huna ndege ukibaki huna ndege uchaguzi ukiwa wanaanza kuponda nchi gani isiyokuwa na ndege ndege mijini tupeni kura tutanunua ndege

Upinzani wa Tanzania ni wa kitoto na wa kijinga

Mkuu naona umepanick hata kuweka koma na nukta umeshindwa!
 
Back
Top Bottom