Ndugai: Mbunge wa CCM hatakiwi kupingana na serikali yake bali aishauri tuuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndugai: Mbunge wa CCM hatakiwi kupingana na serikali yake bali aishauri tuuu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by babykailama, Jun 27, 2012.

 1. babykailama

  babykailama JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kama Naibu Spika umekiuka miongozo ya uendeshaji shughuli za Bunge, umedhalilisha shule yako na hata Chama chetu cha Mapinduzi. Unawezaje kusimamia mijadala Bungeni kinyume na Kanuni za Kudumu za 2007 Sehemu ya Tano hasa Kanuni ya Majadiliano (mambo yasiyoruhusiwa Bungeni) ibara ya 46: 1 (g).

  Haijalishi wewe au mimi ni mwana CCM au la, umeyumba sana leo katika kutoa miongozo yako juu ya haya mambo matatu:


  1. Mbunge Kiwia wa Ilemela, alipotoa kwa masikitiko maelezo yake juu ya kutishiwa maisha yake na hata kujeruiwa. Mh. Ndugai, hujatoa hata pole kwa muhusika juu ya hilo, ukaamua kukubali mwongozo wa CW atoe ushahidi hapo hapo kitu ambacho unajua si rahisi maana inahitaji muda na pia ili tuwe serious, anahitaji kuyaweka katika maandishi ili kuweka kumbukumbu na pengine kwa usalama wa wengine ambao wanaweza kuwa mashahidi katika tukio hili ambao wangependa kutojulikana.

  Aidha ulipaswa kuchunguza kwanza juu ya jinsi Polisi Mwanza walipoyafikisha malalamiko ya huyo Mbunge kabla ya kukimbilia kulazimisha Mbunge atoe maelezo ya kuthibitisha ambayo baadaye huwa yanaishia kuumbua wengine na kuleta speculations kibao zinazozagaa na kuendela kuchafua watu wengine na au kuendeleza majungu na tishio la ukosefu wa amani.


  2. Kuhusu taarifa ya Mh. Mwigulu akinena kuwa "Hata sasa gari la Mh. …… lime-pack hapo nje", hukustahili tu kumwambia Mh. Kiwia aendelee na kutoa hoja zake na kugairi hiyo ‘taarifa'ya Mwiguru. Ulistahili kumsahihisha / kumkemea Mh. Mwigulu kuwa awe makini katika kutumia nafasi yake kama Mbuge kwenye mambo serious kama hili ambalo mwenzake alivamiwa na kuumizwa na epusha mbali Mola wetu kamjalia kapona.

  Hii ni mara ya tatu nimemshangaa sana Kiongozi wa ngazi ya juu ya CCM (T) Mh. Mwigulu ambavyo anashindwa kutumia elimu yako kujistahi katika kubehave kama msomi na kiongozi wa kitaifa wa Chama Tawala. Rejea alipotupa adharani hotuba ya kambi ya upinzani juu ya bajeti bila kupewa hata onyo maana kwa mujibu wa kanuni hiyo ni dharau au kejeli ambayo inaweza kufanya Bunge lako lisitawalike (lisiendeshwe);

  pili kumbuka alivyo mjibu Mbunge wa CHADEMA akitamba kwa dharau akinena kuwa ni mara ngapi atawafundisha, kwamba jana yake alimfundisha kaka yake Mbunge na siku hiyo tena dada yake Mbunge!!. Mh. Ndugai kumbuka utambulisho wa namna hii wa kuwataja watu kaka na dada si rasmi maana watu wote humo mjengoni ama wanakuwa addressed kupitia kwa Spika, Naibu Spika au Mwenyekiti na si vinginevyo hata kama watu wanamahusiano ya kaka, dada , mume , mke.

  Sasa hili la leo ni la tatu; yaani Mbunge wa Taifa aliyevamiwana kwa siraha na kunusulika kufa anaeleza juu ya kilichomtokea, na Kiongozi mkuu kama huyo kwa dharau anakurupuka na kusema kuwa "hata gari lake mtajwa liko hapo nje sasa", alikuwa na maana gani? Je haikuwa busara kutafakari tuhuma ya namna hii na kutaka vyombo vya dola vishughulike?

  Ni nani asiyejua kuwa packing ya gari au uonekano wa mtu kwenye criminal scene ni tofauti na muonekano wa mtu au gari mahala pengine popote na kwamba hiyo inaweza kuwa ya muhimu sana katika kuisaidia polisi juu ya kupata taarifa kamili ya kilichotokea. Mh. Msomi Mwigulu, bila kujali sisi ni wa vyama gani, mimi na wote wanaopenda maendeleo, amani na kutopenda aibu isiyo ya lazima kwa Wasomi kama wewe nasema, ‘you have got to restrain yourself and recap your social inhibition to do justice to your cognitive ability by allowing your thinking process take precedence over your hasty vocalizations!

  3. Kuhusu, masahihisho toka Mh. Mbatia alikuwa sahihi sana. Hakika mtu anaposema bungeni "mwenye uchungu akazae" ni lugha ya mipasho na tena udhalilishaji kwa akina mama kama yule Mh. Lusunde alivyochafua hewa pale Arumeru Mashariki (replay hii video usiikie Mh. Livingstone Lusinde akimwaga Sera za CCM Arumeru - YouTube).

  Kwanza kisemantiki wanaonekana hata kutojua kuwa kuna utofauti kati ya uchungu na utungu, pili mtu anapojaribu kulitumia vibaya tendo la kuzaa au (kujifungua) pasipohusika ni mdhalilishaji wa hilo tendo lililomleta hapa duniani in the first place! Shame be, on them!

  Ndugai kwa sababu unazozijua, kuhusu hili ukapigia mstari tamko la mipasho na kumkingia kifua kuwa Mpashaji hawezi kuliondoa au kulibadilisha eti kwa kuwa ni ukweli. Je, wewe kama Naibu Spika unaweza sasa kututhibitishia sisi Waajiri wako Watanzania kuwa huyu Mbunge wa kiume anaweza kuwa na mimba, ilihali wewe usupport mipasho kama hiyo kuwa aende kujifungua?


  Namaliza kwa kusema kuwa CCM inaweza kuwa si mbaya kama tunavyodhani, lakini vitendo vya kipuuzi visivyovumilika vya kushindwa kuonyesha ukomavu wa ki-uongozi (wakati uwezo unao) katika dhamana uliyopewa wewe Mh. Ndugai na pia kauli za kebehi na kujinyanyua kuonekana kuwa na elimu ya juu sana na ya kipekee (eti Economics) toka kwa Mh. Mwigulu na wengine wenye tabia kama hizi, ndizo zinafanya Watanzania wengi sana Vijana kwa Wazee waanze kuichukia CCM na kuiona kuwa ni jinamizi.

  kwa mwendo huu, ambapo teknolojia iko juu, watu sasa wanarekodi maneno yenu na taswira zenu kwenye mp3 & mp4 na wanazitunza na kuzionyesha kila mahala; msije mkashangaa siku moja (hata kama ni baada ya karne), mkajikuta mnaburuzwa na makucha ya sheria mkiwa wazima au mnapumulia mashine kama yaliyomkuta Rais Mubaraka!
   
 2. mhalisi

  mhalisi JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,181
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Mwigulu ni mgoni tu. wananchi wa Iramba Magharibi wamekula hasara.
   
 3. babykailama

  babykailama JF-Expert Member

  #3
  Jun 27, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  [h=2]Moderator, kichwa cha habari kisomeke:

  Mh. Job Ndugai umenihuzunisha sana![/h]
   
 4. dfreym

  dfreym JF-Expert Member

  #4
  Jun 27, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hawa jamaa wanaishi kihisia zaidi.
   
 5. Mbaga Michael

  Mbaga Michael Verified User

  #5
  Jun 27, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 2,914
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 160
  Chukua 5
   
 6. d

  dguyana JF-Expert Member

  #6
  Jun 27, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 426
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole na Ahsante Ulimboka. Watakuja wengi na kauli za kuvua Gambaleo. Na bado.
   
 7. Nicas Mtei

  Nicas Mtei JF-Expert Member

  #7
  Jun 27, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 11,569
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Ndugai ni mweupe. Nilidhrisha hlo siku ile alpokuwa na mdahalo wa waz pamoja na Tundu Lissu ktk hotel 1 hapa Dodoma.
   
 8. NdasheneMbandu

  NdasheneMbandu JF-Expert Member

  #8
  Jun 27, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 940
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwenye akili aelewe maneno haya ambayo roho wa bwana amenena kupitia kichwa cha mtumishi wake. Asante mkuu wa makala ndefu na inayosisimua na kuamsha ari ya mapinduzi ya kuikomboa nchi hii kutoka kwenye makucha ya chama tawala.
   
 9. Parata

  Parata JF-Expert Member

  #9
  Jun 27, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 3,119
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  bado magamba mtayavua sana leo hii ni trela tu kuna picha inakuja
   
 10. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #10
  Jun 27, 2012
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Mwigulu anajiona kama Albert Einstein. Ndio kichwa cha genius kimejaa tope kama kile? Hajui hata anachoongea, degree za kuiba mitihani hizo.
   
 11. L

  Lua JF-Expert Member

  #11
  Jun 27, 2012
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kabla ya kuahirisha bunge leo job ndugai alitoa maelekezo ya wabunge kufuata kanuni na akaelezea kuwa mbunge akitoa 'taarifa' anayepewa taarifa anapaswa kuipokea au kutoipokea, lakini nashanga leo wakati Mdee akichangia hotuba ya waziri mkuu alisimama mbunge wa ccm na kumpa taarifa halima mdee. badala ndugai kumuhoji mdee kama taarifa anaipokea au haipokei yeye alimtaka mdee atoe maelezo kile alichosema kuhusu kauli ya waziri mkuu ya leo ya 'liwalo na liwe' na tukio la kutekwa kwa ulimboka.je kumwambia mdee atoe maelezo badala ya kumuhoji kama anapokea au hapokei taarifa je ni kufuata kanuni?
   
 12. K

  Kyatsvapi JF-Expert Member

  #12
  Jun 27, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 316
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 45
  Mara nyingi wasimamapo magamba bungeni huwa natoa sauti (mute) luninga yangu na mara wamalizapo nairudisha tena.

  Wengi wao huwa hawana hoja za msingi kuhusu vile wavichangiavyo.

  Sijui kwa nini hawajifunzi kwa wengine?
   
 13. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #13
  Jun 27, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Kwi! Kwi! Kwi! Kwani ulikuwa hujui ndugai na Yule mwenyekiti wao kile Chama cha majambazi ni dhaifu
   
 14. KirilOriginal

  KirilOriginal JF-Expert Member

  #14
  Jun 27, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 1,934
  Likes Received: 464
  Trophy Points: 180
  Wenye mawazo ya enzi ya chama kimoja ni vigumu sana kuondokana na hiyo dhana, watu wasiowaza kuwa dunia hubadilika, watu wenye kiburi kwamba 'utanifanya nini' endeleeni vivyo hivyo mnajikaanga wenyewe!
   
 15. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #15
  Jun 27, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Albert Einstein hakuwahi kujisifu hata siku moja, na hii ni kawaida ya gifted persons wote. Mwigulu ni mtupu kwa kila hali na kwa tafsiri ya neno utupu. Makelele ya huyu makalio ni kutokana na utupu wa akili aliouvaa!
   
 16. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #16
  Jun 27, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Ni Kauli ya Naibu Spika bwana John Ndugai wakati akihitimisha shughuri za bunge jioni hii kuwa mbunge wa Chama Tawala hatakiwi kupinga hoja za serikali yake bali wanaotakiwa kupinga ni wapinzani.

  Najiuliza bungeni kumbe ni ndiooo kwa kila jambo linaloletwa na serikali hata kama halina maslai kwa taifa
   
 17. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #17
  Jun 27, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ukombozi wa nchi u karibu. Wananchi kwa sasa nashauri tuanze kutafakari jinsi ya kufanya, kwani kuna viashiria vingi tu ambavyo vimesimamiwa na huyu kichaa mwigulu
  1. Alisimamia mauaji wa wapiga kura Igunga
  2. Akaenda kuchochea chuki Arumeru
  3. Ni muongo na mnafiki ambaye yupo tayari kuua
  Tuungane kumtosa ktk kura. Na ikumbukwe "time is not our best friend" ipo siku hawa jamaa watajikuta kwenye makucha ya sheria!
   
 18. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #18
  Jun 27, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Mwigulu anawakondesha sana vilaza wa CDM, jioni hii pia kawachana na bajeti yenu ya harusi, hakuna cha Tundu wala Lusu aliye waokoa. Mwaka huu hadi mlie mule mjengoni.
   
 19. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #19
  Jun 27, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,811
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kilaza tu
   
 20. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #20
  Jun 27, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  Mwelevu hata siku moja hajisifii
   
Loading...