Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Hivi Ndugai alikuwa na uharaka gani wa kumuita Masele nyumbani akijua alikuwa katikati ya kikao cha PAP, kama kweli hakuwa akitumika na Raisi wa PAP aliyetuhumiwa kwa makosa ya ngono?
Kwa kiongozi mwenye hekima na busara, vitu ambavyo naona ni adimu kwa Ndugai, hata kama Masele alikuwa na kosa, basi angesubiri kwanza amalize shughuli ya PAP, kwa kuwa Masele angerudi tu nyumbani. Hakukuwa na ulazima wa kufanya jambo hili kwa kutumia nguvu kubwa aliyotumia na kuiingiza Tanzania katika mmweko wenye kutia aibu kwamba tunafanya mambo ovyo ovyo. Mwenye kufanya mabo ovyo ovyo hapa ni wazi ni Ndugai, sio Masele.
Ndugai anakiri kwamba kumwita Masele hakuhusiani na PAP, sasa kwa nini unataka kuvuruga vikao vya PAP kwa jambo ambalo lilihitaji subira kidogo tu? Je ni Ndugai kujiona kuwa ana mamlaka makubwa kuliko PAP, au kuona kuwa Bunge na Tanzania ni muhimu kuliko PAP?
Huyu Ndugai ana matatizo sana ya kisaikolojia. Analalamika Bunge la Tanzania kudharilishwa kwa kuitwa dhaifu lakini yeye anafanya tendo la juu kabisa kuonyesha dharau kwa Bunge la Afrika. Na huyo huyo Ndugai alipiga mtu, mwanachama mwenzie wa CCM, fimbo ya kichwa kwa jambo dogo tu la kutoelewana. Ni huyo huyo Ndugai alitoa matamko kwamba CAG atakuja hata kwa pingu. Na yote haya yanadhihirisha jambo moja ambalo inabidi uwe na akili ya mwenda wazimu kutoliona - Ndugai ana dharau, hana busara wala hekima, na hafai katika uongozi wa nafasi nyeti kama Uspika.
AU inapaswa kuilalamikia rasmi Tanzania kwa tabia ya kuonyesha dharau kwa kikao halali cha PAP.