Ndugai, kufanya kosa siyo kosa bali kurudia kosa

Kama taasisi za dini zenyewe zinaaminika kuwa huru ndiyo zinaongozwa na kina Mwingira, Gwajiboy, Shoo, Mwamakula na Bagonza tuendelee tu na katiba yetu.
 
Kwanini wasiruhusu na wadau, ambao ni vyama vya siasa nao kupeleka mapendekezo ya majina yao??

vyama viko vingi sana na kila chama kitasema kina haki yake kinahitaji muwakilishi wake..
 
angalau hapa naweza kukuunga mkono, wewe ni mmoja wenzio wengi ni wafukuza upepo na wasaka maslahi....ndio hukukubaliana na suala la Lowassa lakini akawa ndio mgombea Urais maana wenye maslahi ndio wenye chama...

Hao ambao unaoamini ndio wenye chama walifanikiwa kumleta Lowassa kipindi kile, kwa taarifa yako hawatakaa warudie kosa lile na waachiwe tena. Nadhani uliona walichotaka kwa Nyalandu uchaguzi uliopita,na walichoamua wanachama na hawakuthubutu kugeuza matokeo. Na ndio imetoka hiyo. Siku nyingine wakiokota hizo taka ngumu toka CCM watajua hawajui.
 
vyama viko vingi sana na kila chama kitasema kina haki yake kinahitaji muwakilishi wake..

Vyama viko 19, vilivyo serious na siasa havifiki vitano. Na vyenye wanachama zaidi ya milioni hawavivuki viwili. Vingi ni vya kwenye flash disk.
 
Hao ambao unaoamini ndio wenye chama walifanikiwa kumleta Lowassa kipindi kile, kwa taarifa yako hawatakaa warudie kosa lile na waachiwe tena. Nadhani uliona walichotaka kwa Nyalandu uchaguzi uliopita,na walichoamua wanachama na hawakuthubutu kugeuza matokeo. Na ndio imetoka hiyo. Siku nyingine wakiokota hizo taka ngumu toka CCM watajua hawajui.

hahahaha, Nyalandu alishinda na walio wengi walitaka yeye ndio awe mgombea maana alikuja na mkwanja...busara tu za watu fulani na huruma kwa Lissu..... Kwa taarifa hizo huone kama kuna mashimo hapo..
 
Vyama viko 19, vilivyo serious na siasa havifiki vitano. Na vyenye wanachama zaidi ya milioni hawavivuki viwili. Vingi ni vya kwenye flash disk.

hahahaha, navyo ni vyama vitadai haki ya uwakilishi...hata CDM ilianza kama wao....NCCR ikiwa na nguvu CDM ilikuwa kama TPP tu...
wakati CUF inanguvu CDM ilikuwa utopolo tu..

Ukiangalia trends za NCCR, TLP na CUF then CDM utagundua uelekeo ni uleule tu ni suala la muda tu....
 
Itakuwa vyema Mkiti wa tume huru ya uchaguzi asiwe Mtanzania, awe mtu mwenye hadhi ya Jaji kutoka jumuiya ya madola....
 
hahahaha, Nyalandu alishinda na walio wengi walitaka yeye ndio awe mgombea maana alikuja na mkwanja...busara tu za watu fulani na huruma kwa Lissu..... Kwa taarifa hizo huone kama kuna mashimo hapo..

Kura zilihesabiwa hadharani kwenye mkutano mkuu wa kumchagua mgombea kwa mara ya kwanza. Labda alishinda off camera kwa kumwaga hela kwa viongozi ili apate huruma ya kugombea. Hata kwenye kampeni zake za kutaka wadhamini ili agombee hazikuwa na watu. Kazunguk na basi lake nchi nzima watu wanamchora maana walishaumwa na nyoka. Hatimaye Mungu hamfichi mnafiki, leo Nyalandu yuko wapi?
 
hahahaha, navyo ni vyama vitadai haki ya uwakilishi...hata CDM ilianza kama wao....NCCR ikiwa na nguvu CDM ilikuwa kama TPP tu...
wakati CUF inanguvu CDM ilikuwa utopolo tu..

Ukiangalia trends za NCCR, TLP na CUF then CDM utagundua uelekeo ni uleule tu ni suala la muda tu....

CDM ilivyoanza imekuwa ikipanda kila msimu, na sasa dola ambayo ndio CCM halisia imebidi ijitokeze waziwazi. Kwa bahati mbaya CCM imebaki na mbinu zile zile za zamani wakati kizazi kimebadilika. Kizazi cha sasa sio kile kilichonyeshwa mauaji ya Rwanda na kuambiwa upinzani utaleta vita. Kwa jinsi CCM inavyozidiwa hata kuiba kura inakuwa shida, ndio hiyo inaishia kupora mchakato wa uchaguzi.

Hali hii inapelekea watu kutokupiga tena kura kwani hawaikubali CCM, na wapinzani hawana silaha za kulinda ushindi wao. Kwa mwendo huu wa CCM kushurutisha kubaki madarakani bila ridhaa ya umma, machafuko pekee ndio yatawatoa. Hapo ndio utajua CCM iko nje ya muda bila yenyewe kujijua.
 
Kura zilihesabiwa hadharani kwenye mkutano mkuu wa kumchagua mgombea kwa mara ya kwanza. Labda alishinda off camera kwa kumwaga hela kwa viongozi ili apate huruma ya kugombea. Hata kwenye kampeni zake za kutaka wadhamini ili agombee hazikuwa na watu. Kazunguk na basi lake nchi nzima watu wanamchora maana walishaumwa na nyoka. Hatimaye Mungu hamfichi mnafiki, leo Nyalandu yuko wapi?

kaa vizuri na inner circle ya chama chako.....hata CDM huwa kuna dip state..watafute utapata taarifa...hela hiyo hiyo Nyalandu ilitaka kuleta shida....hekima tu na busara ya mwamba ilisaidia kidogo..
 
kaa vizuri na inner circle ya chama chako.....hata CDM huwa kuna dip state..watafute utapata taarifa...hela hiyo hiyo Nyalandu ilitaka kuleta shida....hekima tu na busara ya mwamba ilisaidia kidogo..

Hakuna anayejali, hiyo hela ingeleta chochote itakacho, lakini sio rahisi kubadilisha mitazamo yetu. Tunaweza kuchambua upi ni uhuni, na ni wa kiwango gani,na namna ya kuvuka hiyo changamoto. Simply tumeshajitambua, na tunajua namna ya kudeal na hizo changamoto.
 
Hebu tuambie wewe sasa kwa maoni yako, hao wajumbe wapatikane kwa utaratibu gani?
TLS inateua wajumbe 2
AZAKI zinateua wajumbe 2
Umoja vyuo vikuu wajumbe 2
Rais aneteua mmjumbe 1
Bunge linatea mjumbe 1
Mahakama inatea mjumbe 1
 
Yaani bado Kuna watu wanamtetea ndingai,Pole Pole gwajima,yaani kwa maneno yao ya shobo wakazani hii nchi Ni yao hawafai hata kuzungumzwa
 
nahitaji kukusoma kwa utulivu kidogo....

hiko kidogo nilichosoma naomba nikupe tahadhari kidogo, hizo asasi unazosema ndio zimetupa mtu kama Pole pole na Prop Kabudi...na wengine wanaofanana..
Hawa wana kosa/tatizo gani ?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom