Ndugai: Hakuna Ushahidi uliowahi kuwasilishwa kwenye bunge hili! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndugai: Hakuna Ushahidi uliowahi kuwasilishwa kwenye bunge hili!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mnyakatari, Jul 12, 2012.

 1. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,557
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  Akitolea ufafanuzi hoja ya Mwigulu Nchemba bungeni leo asubuhi naibu spika amesema kuwa tangu bunge hili la kumi lianze halijawahi kupokea ushahidi wowote kutoka kwa wabunge wanaotakiwa kufanya hivyo na kiti! Ilikuwa ni baada ya Mwigulu kuomba mwongozo kuhusu maneno ya Mnyika kuwa alihusika kwenye wizi wa EPA.

  Concern yangu kubwa hapa ni alichokisema Ndugai kuwa wabunge hasa wa upinzani wajiangalie na matamshi yao ndani ya bunge na wawe wapole wanapotakiwa kufuta kauli zao kuliko kujifanya wana ushahidi ukizingatia kuwa hakuna ushahidi uliowahi kuwasilishwa kwenye bunge hili.

  Sote tunakumbuka matukio kama hayo bungeni na idadi ya wabunge waliowahi kuambiwa walete ushahidi kuthibitisha wayasemayo.Zitto Kabwe,Godbless Lema ni mfano wa wabunge ambao wamewahi kutakiwa ushahidi kwenya bunge hili na wao wenyewe kusema baadaye kuwa wameshawasilisha.

  Pia kwenye sakata la Godbless Lema,Spika Makinda ameshawahi kulithibitishia bunge kuwa ameupokea.Hiyo ilikuwa ni baada ya kuombwa mwongozo na Zitto(kama sikosei) kuwa ushahidi wa Lema usomwe bungeni kama umeshawasilishwa mezani kwake naye akajibu kuwa amepokea huo ushahidi na wanaendelea kuufanyia kazi.

  Hata kwa upande wa Zitto,Makinda aliwahi kuthibitisha kupokea ushahidi wake na baadaye Zitto mwenyewe kuthibitisha.
  Ndugai pia aliendelea kudai kuwa wabunge waache kudanganya kwenye mitandao kuwa wamewasilisha ushahidi huku wakijua kuwa hawajafanya hivyo.

  Hata hili la Mnyika Ndugai amesema kilichowasilishwa ni utangulizi tu na wala sio ushahidi wa alichokizungumza kinyume na inavyosemwa kwenye mitandao na magazeti!

  Hili linaleta picha gani?kwamba wabunge wetu wanadanganya? Spika Makinda alidanganya? Wabunge wetu kwa kushirikiana na Makinda wametudanganya na Ndugai ameamua kuwatolea uvivu?Kwamba Kinachowasilishwa huwa hakikidhi kuitwa Ushahidi wa tuhuma husika?

  Tujadili.
   
 2. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Hivi hakuna mwongozo unaoruhusu kuhoji kiti (NAIBU SPIKA) kama amelidanganya bunge?!
   
 3. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwenye hoja yako kuna maswali na majibu humo humo,select majibu ujijibu.
   
 4. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inaonekana Ndugai kafuzu kozi ya kuitetea Serikali,fuatilia miongozo na ushauri wake always anasihi kutoipinga serikali as is ni naibu waziri fulani
   
 5. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,557
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  Aisee!
   
 6. k

  kimeloki JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 1,932
  Likes Received: 957
  Trophy Points: 280
  Anafikiri kwa kusema hivyo atawafunga mdomo hiyo mbinu iko weak haitasaidia.
   
 7. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #7
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,557
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  Inashangaza sana mkuu,Unafikiri ni kwa nini aliongea vile kuhusu ushahidi unaowasilishwa na wabunge?
   
 8. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #8
  Jul 12, 2012
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ndugai amevunja kanuni zifuatazo leo;

  Naomba kunukuu kanunizifuatazo ;
  1. Kanuniya 5 (1) ambayo inasema kuwa "katikakutekeleza majukumu yake yaliyotajwa katika ibara ya ya 84 ya Katiba , Spikaataongozwa na kanuni hizi ………."

  2. Kanuniya 63 (2) " Mbunge yeyote anapokuwa akisema Bungeni hatachukuliwa kuwa anasema uongo iwapo anafanya rejea ya habari kuhusu jambo Fulani lililotangazwa aulililoandikwa na vyombo vya habari"

  3. Kanuniya Adhabu : hii ni kanuni ya 73 (3) "Endapo mbunge yeyote atatakiwa kuthibitisha ukweli wa jambo au suala alilolisema Bungeni na hadi kufikia mwisho wa muda aliopewa amekataa au ameshindwa kutoa uthibitisho huo, Spika anaweza kumsimamisha Mbunge huyo kuhudhuria vikao vya Bunge visivyozidi vitano"

  4. Kanuniya kupelekwa kamati ya haki, maadili na madaraka ya bunge ni 74(1) "Spika anaweza kutaja jina la Mbunge kwamba amedharau mamlaka ya Spika na kisha kupeleka jina hilo kwenye kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge….."
   
 9. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #9
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,557
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  Hapa tunaona kuwa suala la Mnyika limepelekwa kamati ya haki,maadili na madaraka ya bunge kimakosa!Hakuna mahali ambapo mamlaka ya spika imedharauliwa na Mnyika kama inavyotaka kanini ya 74(1)
   
 10. M

  Maga JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 325
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Tatizo Ndugai ana jazba sana alikuwa na haja gani kuanza kuongea yale yote na je mbona wanapopewa ushahidi wenye mashiko wanaishiakukaa kimya? Spika na wasaidizi wake wamegeuka kuwa sehemu ya serikali. Kuna haja kupitisha kifungu kwenye katibu mpya spika na wasaidizi wake kutokuwa wabunge wawe watu huru
   
 11. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #11
  Jul 12, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 7,996
  Likes Received: 6,778
  Trophy Points: 280
  Huyu naibu spika lengo lake ni kuwatisha wabunge wa upinzani,hasa wa CDM, lakini anachosahau ni kuwa hawa jammaa hawatishiwi nyau, na wataendelea kuleta tuhuma zenye ushahidi mzito, ambapo kama kawaida ya kiti cha spika, kwa kuwa lengo lao ni kukingia kifua chama chao cha mabwepande, ushahidi wowote wenye nguvu, kama ule wa Lema vs Liwalo na liwe na Zitto vs Mkulo, ushahidi wa aina hiyo utaozea kwenye cabinet za Bunge, tusitarajie kuwa itatokea siku watathubutu kuutoa hadharani!!
   
 12. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #12
  Jul 12, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Huyu jamaa huwa anakunywa pombe kweli?
   
 13. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Naomba kujua Resume/CV ya MH Ndugai.
  Kabla ya kuwa mbunge alikuwa nani?
   
 14. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #14
  Jul 12, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Inasemekana alikuwa bwana nyama; kizungu game ranger!!!
   
 15. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #15
  Jul 12, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kwa siku za karibuni tokea Mnyika abainishe JK dhaifu naona Ndugai kachange na kuonyesha chuki zake wazi kabisa,,pamoja na mengine yote,,maneno aliyomtolea Mdee leo yanadhihirisha hili
   
 16. a

  andrews JF-Expert Member

  #16
  Jul 13, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ​sita aliyemtoa zito yukoo wapi?
   
 17. B

  BUBERWA D. JF-Expert Member

  #17
  Jul 13, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 446
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 45
  kuna uwezekano mkubwa ndugai akwa anadanganya kutokana na tabia yake ya kuilinda serikali badala ya kusimamia kanuni za bunge. Yeye na mabumba oooooooovyo kweli!
   
 18. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #18
  Jul 13, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ndugai naona ni naibu spika mfu kiakili mara anapoongoza Bunge lina mshinda na kinachotokea anapata hasira kutokana na uelewa wake kuwa mdogo kwenye nyaja ya siasa
   
 19. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #19
  Jul 13, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Tatizo si ndugai..tatizo chama kilichompendekeza..chama makini hakiwezi kuruhusu mtu mtupu kama ndugai kuongoza organ kama bunge
   
 20. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #20
  Jul 13, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  BUNGE LETU NI CHURCH OF LIERS!!! kuhusu EPA na Ufisadi wote bado makinda eti haamini mpaka kuwepo na ushahidi! she come from church of liers! wizi wa wanasiasa hauna nyayo! huwezi hata siku moja ukagundua kadokoa vipi au kapewa rushwa kiasi gani! Makinda amka mama ! wewe ngoja tuu wajifanye kumsaidia mu Iran na hao west europe na USA watazidi kuwalipua na ma aakounti yao yaliyo uswiss! hao sita ilikuwa na kuwatia jamba jamba kuwa kama mkiendelea tuuu kumbeba muiran basi sisi tuna list za wote waliiibia nchi yenu na tutatoa hadharani!!. usicheze ma myahudi hapa duniani!
   
Loading...