Ndugai awaweka JK na Pinda Ulingoni, Ngeleja Tia maji Kichwani Sasa

GHOST RYDER

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
1,025
475

“Bunge haliwezi kukubali Waziri mkuu adharauriwe na sisi tukae kimya, hizo dharau wafanyie huko huko” – Ndugai


Unaweza kuyaona maneno mafupi yasiyokuwa na Tija lakini kwa tafsiri iliyoshiba yametosha kumtikisa Rais aliyeamua kuonyesha ubabe kwa kumrudisha Kazini Jairo, na masaa machache baadaye akala matapishi yake kwa kuwahadaa watanzania wasiojua protokali kuwa anamrudisha Likizo ili kupisha uchunguzi wa Tume huru ya Bunge.

Anayafanya haya huku anamsahau Ngeleja ambaye naye jana tena alionyesha furaha isiyo kifani akipongeza Uamuzi wa Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo.

Kwa Serikali iliyo makini Ngeleja anapaswa kujipanga sasa kuachia ofisi. Kauli ya Ndugai ni Fumbo zito kwa Wizara ya Nishati na Madini na Mtihani Mkubwa kwa JK jinsi anavyoendesha Nchi kwa ushikaji.

Hapa kintendawili bado ni Kizito sitashangaa haya mabadiliko yanayokuja ya Baraza Mawaziri yakathibitisha ukurasa wa Bifu hili jipya naliliona kwa fasiri yangu juu ya kauli ya Ndugai

ADIOS
 
Ibara ya 63, (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema hiviiii!! Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndiyo chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii.. Sasa kazi kwenu wabunge kisu mnacho, watanzania wote tunakuangalieni jinsi mtakavyo tumia kisu hicho.
 
Jamani hii nchi ilishauzwa siku nyingi. JK anatuletea sinema za kihindi na sisi tumetulia tu.
Watanzania inabidi tuchukue hatu bila hata kusubiri wabunge watafanya nini
 
Ngereja he has to go wanadharilisha nchi sio wizara hatuwezi kuonekana wote waongo nchi hii haiwezekani hata kidogo Ngereja mwongo kwa kila move afanyao what a hell watanzania tumekaa tunamchekea lazima aondoke
 
me nilijua Ngeleja ameamua kujiuzulu mwenyewe kabla ya aibu kumkuta maana skendo nyingi zimemkuta lakini hataki kujiuzlu lakini kwa hili atu tendeee haki jamanii atuachie ofisi yetu
 
Tunasubiri kuona Waheshimiwa Wabunge wakila matapishi yao kutokana na sakata hili kwani usalama wa Taifa wameshaiba vielelezo muhimu. Ni sarakasi nyingine itakayotupeleka hadi kwenye uchaguzi 2015. Ila tunawaomba wabunge wasikate tamaa tunataka kuona kilichomtoa kanga manyoa. NGEREJA OUT.
 
Popcorn zangu zikowapi mie nikae mkao wa kutazama movies maana nyingi hizo!!!!!!
Sijui lini nchi hii itaisha vituko.
 
Hii ni vita ya uenyekiti wa chama mwakani: JK atavuliwa gamba la uenyekiti kumpunguzia majukumu, hivi sasa wanaoutaka uenyekiti ndo wanaotuyumbisha, maana nafasi iko wazi.
 
JK ndo ananisikitisha kabisa , huu mtindo wa kuwatumia wasaidizi wake kama "shield" yake utamuumiza vibaya muda si mrefu.
Pinda ameshabeba mizigo yao na soon atachoka ,
CAG nae tayari kachafuliwa ,
PCCB hawaaminiki
Usalama wa taifa ndo wezi wa kura
.....................

Haya yana mwisho , na upepo mbona unaonekana unavuma vipi , JK hauwezi kufanya moja iwe mbili ndugu yangu ,
Kheri lawama kuliko fedheha.
 
JK ndo ananisikitisha kabisa , huu mtindo wa kuwatumia wasaidizi wake kama "shield" yake utamuumiza vibaya muda si mrefu.
Pinda ameshabeba mizigo yao na soon atachoka ,
CAG nae tayari kachafuliwa
.

Kwa hakika hakuna matumaini tena kwa huyu maana amekwishakuwa kikaragosi.
 
.........all in all the bad animal of the issue is JK.
yote haya ni kwa sababu ya kukosekana na mvua; hivyo tunaomba mvua inyeshe, mabwawa yajae, na umeme uweze kupatikana nchi nzima; halafu tuone mavuvuzela ya magwanda sijui yataenda kupigiwa wapi?
 
Sasa wadau hii Muvi Staring ni ndugai,Jairo, Pinda au JK,? Au kuna mmoja ni Kubwa la maadui?
 
<b>yote haya ni kwa sababu ya kukosekana na mvua; hivyo tunaomba mvua inyeshe, mabwawa yajae, na umeme uweze kupatikana nchi nzima; halafu tuone mavuvuzela ya magwanda sijui yataenda kupigiwa wapi?</b>
<br />
<br />
Ila masabuli ni mkali, kwa nini siku zote alikuwa hatoboi ukweli kuwa watu kama huyu anatumia makalio kupost kitu kama hiki, hata kama ni uzalendo huu ni wa kutumia makalio
 
Kwa kweli hali ya kisiasa si nzuri nchini. Tunaiomba serikali itusaidie mvua zinyeshe na mafuta yapatikane ili kuondoa hili wingu la sintofaham
 
Mambo si shwari kufuatia kauli hii kuna mpasuko Mkubwa...Nakamilisha ukusanyaji wa Dondoo muhimu na Jumapili zitapatikana hapa katika mfumo wa arlet au tetesi kwa chochote kitakachokuwa kimekusanywa hadi muda huo

ADIOS
 
"Bunge haliwezi kukubali Waziri Mkuu adharauliwe."

Huku ni kutoelewa migawanyiko ya majukumu katika mihimili ya utawala wa nchi.

Sifurahii kuona bunge linatetea mhilimili pinzani (serikali) isidharauliwe. Pinda na Jairo na Kikwete na Luhanjo na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu ni wamoja, serikali.

Tunahitaji mfumo wa checks and balances ambapo Bunge linajitenga na serikali nzima, Bunge likiono serikali inajipinga pinga linatakiwa kudai uwajibikaji wa serikali, sio kuwachambua na kutetea mmoja mmoja, sijui Pinda is right, Luhanjo is wrong, Kikwete is right na Mkaguzi akaguliwe tena, ni mfumo wa kihohehahe.
 
"Bunge haliwezi kukubali Waziri Mkuu adharauliwe."

Huku ni kutoelewa migawanyiko ya majukumu katika mihimili ya utawala wa nchi.

Sifurahii kuona bunge linatetea mhilimili pinzani (serikali) isidharauliwe. Pinda na Jairo na Kikwete na Luhanjo na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu ni wamoja, serikali.

Tunahitaji mfumo wa checks and balances ambapo Bunge linajitenga na serikali nzima, Bunge likiono serikali inajipinga pinga linatakiwa kudai uwajibikaji wa serikali, sio kuwachambua na kutetea mmoja mmoja, sijui Pinda is right, Luhanjo is wrong, Kikwete is right na Mkaguzi akaguliwe tena, ni mfumo wa kihohehahe.

Mawazo kama haya kwao ni sumu sana maana yanahatarisha mianya yao ya utafunaji wa rasilimali za Umma. Otherwise kama wanasoma hapa watajifunza jambo muhimu sana katika mfumo huu mbovu wa utawala wa kuviziana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom