Ndugai atua Zanzibar, akutana na Wajumbe wa Kamati kuu CCM Zanzibar

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,680
22,685
Spika wa Bunge na mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kusini na Kaskazini Unguja, Job Ndugai amekutana na kufanya mazungumzo na Wajumbe wa Kamati Kuu Zanzibar, Wajumbe wa Halmashauri Kuu Taifa, Wenyeviti wa Mikoa,Wilaya na Maafisa wa CCM Ofisi kuu Zanzibar alipowasili Zanzibar leo.
FB_IMG_1553593113181.jpeg
FB_IMG_1553593120394.jpeg


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Hahaha, CCM mbona ACT wanawahangaisha hivyo.....LAKINI Spika huwa anachaguliwa Na wabunge wa vyama vyote , namshangaa sana Ndugai kuwa biased katika hili Kwa kuegemea sana Upande wa Ccm huku akionesha uonevu wa waziwazi Kwa Viongozi wa Upinzani

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Spika wa Bunge na mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kusini na Kaskazini Unguja, Job Ndugai amekutana na kufanya mazungumzo na Wajumbe wa Kamati Kuu Zanzibar, Wajumbe wa Halmashauri Kuu Taifa, Wenyeviti wa Mikoa,Wilaya na Maafisa wa CCM Ofisi kuu Zanzibar alipowasili Zanzibar leo.View attachment 1054422View attachment 1054423

Sent from my iPhone using Tapatalk
Wanaweweseka tu, Maalim Seif ndii chaguo la Wazanzibar.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi mtu kama huyu anaweza kweli kuongoza Bunge kwa haki. Kama ni mlezi wa Chama Tawala CCM.


Ilimpasa awe na busara zaidi kuliko maonevu ya kufukuza na kuwaondoa wapinzania katika majimbo yao.

Lakini ni huruma sana kwake, kwa maana aseme nini kama mkubwa wake kichama ni Rais.

Huyu Mlezi wa CCM anaweza kufanyia haki Nasari wa Chadema kweli?


Mfumo wa katiba yetu ni mbovu kweli. Siku Moja tutakuja jikuta Spika ni Rais, Rais ni Raisi, IGP ni Rais, Mkuu wa Majeshi ni Rais nk.
 
mie ninachoona wanaoweweseka ni bavicha
Mmeshaambiwa ni mlezi wa ccm kusini unguja,kuna la ajabu gani hapo kukutana na wanachama wake?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom