Ndugai atishia kuifumua kamati ya Bunge ya Bajeti kwa kupitisha ushuru wa mazao

Spika wa Bunge, Job Ndugai ametishia kuifumua Kamati ya Bunge ya Bajeti baada ya kukerwa na kupitishwa kwa sheria inayoruhusu Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kuanza kutoza ushuru wa bidhaa wa asilimia mbili kwa mazao nchini.

Spika Ndugai ameyasema hayo leo Jumatatu Septemba 6, 2021 bungeni mara baada ya majibu ya Wizara ya Kilimo yaliyotokana na swali la nyongeza la Mbunge wa Namtumbo (CCM), Vita Kawawa.

Kawawa amesema wakulima wa tumbaku wamekuwa wanalipa ushuru wa wilaya wa mazao, tozo ya vyama vikuu vya ushirika, chama cha msingi.

Amehoji kama ni kweli kuwa TRA mwaka huu itaanza kuwatoza wakulima wa tumbaku ushuru wa bidhaa.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema ni kweli Bunge lilipitisha sheria ya ushuru wa bidhaa wa asilimia mbili kwenye mazao ya kilimo.

Hata hivyo, amesema bado wizara haijaanza kukata ushuru huo kwasababu mjengeko wa bei ya tumbaku huamuliwa kati ya Februari hadi Aprili. Amesema wakati sheria hiyo inapitishwa tayari mjengeko wa bei wa zao hilo ulikuwa umeshapitishwa.

Hata hivyo, amesema wizara yake imewasiliana na Wizara ya Fedha na Mipango kwa kuwaandikia ili kuona namna gani watatekeleza sheria hiyo lakini kwa kulinda maslahi ya wakulima wa zao hilo.

Ndugai amesema wajumbe wa bajeti wanapaswa kuwa makini sana katika kazi zao kwasababu mambo yakifika bungeni wanaiamini kamati.

“Mkiendelea hivi nitaifumua hiyo, kamati ya bajeti tumeweka watu tunaowaamini sana. Sasa kama mnaenda kule mnalala tu na kupitisha tu vitu vya kienyeji mnatuponza. mnapitishaje kitu kama hiyo bwana,”amesema.

Mwananchi
Hapa ndiyo inafika wakati tunaona bora hata yaliyotokea huko Guinea. Yaani NEC wanatumia B 460 kuandaa uchaguzi mkuu uliopita kisha wao wenyewe kwa msaada wa vyombo vya dola wakaunajisi kwa kura za kwenye mabegi na kutujazia vilaza ambao wanashinda mjengoni kugonga meza na kupitisha sheria mbovu kama mazuzu na zikiianza kutuumiza ndiyo wanashangaa zilipitaje. Huu ni utaahira wa kiwango cha juu kuwahi kutokea duniani, only in Tanzania.
 
Hili Spika jinga sana, yaani yeye ameona hilo tu!
Halafu yeye ndie msimamizi mkuu wa mhimili. Ana ruhusu madudu kwa interest za Ccm halafu zikipokelewa negative ana laumu wengine. Ana kwepa responsibilitu
 
Unataka kuifumua ya nini wakati Bunge lote ni la CCM ?....kwani hamuelewani na nyie humo tena?
 
Back
Top Bottom