Ndugai atishia kuifumua kamati ya Bunge ya Bajeti kwa kupitisha ushuru wa mazao

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,481
9,242
Spika wa Bunge, Job Ndugai ametishia kuifumua Kamati ya Bunge ya Bajeti baada ya kukerwa na kupitishwa kwa sheria inayoruhusu Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kuanza kutoza ushuru wa bidhaa wa asilimia mbili kwa mazao nchini.

Spika Ndugai ameyasema hayo leo Jumatatu Septemba 6, 2021 bungeni mara baada ya majibu ya Wizara ya Kilimo yaliyotokana na swali la nyongeza la Mbunge wa Namtumbo (CCM), Vita Kawawa.

Kawawa amesema wakulima wa tumbaku wamekuwa wanalipa ushuru wa wilaya wa mazao, tozo ya vyama vikuu vya ushirika, chama cha msingi.

Amehoji kama ni kweli kuwa TRA mwaka huu itaanza kuwatoza wakulima wa tumbaku ushuru wa bidhaa.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema ni kweli Bunge lilipitisha sheria ya ushuru wa bidhaa wa asilimia mbili kwenye mazao ya kilimo.

Hata hivyo, amesema bado wizara haijaanza kukata ushuru huo kwasababu mjengeko wa bei ya tumbaku huamuliwa kati ya Februari hadi Aprili. Amesema wakati sheria hiyo inapitishwa tayari mjengeko wa bei wa zao hilo ulikuwa umeshapitishwa.

Hata hivyo, amesema wizara yake imewasiliana na Wizara ya Fedha na Mipango kwa kuwaandikia ili kuona namna gani watatekeleza sheria hiyo lakini kwa kulinda maslahi ya wakulima wa zao hilo.

Ndugai amesema wajumbe wa bajeti wanapaswa kuwa makini sana katika kazi zao kwasababu mambo yakifika bungeni wanaiamini kamati.

“Mkiendelea hivi nitaifumua hiyo, kamati ya bajeti tumeweka watu tunaowaamini sana. Sasa kama mnaenda kule mnalala tu na kupitisha tu vitu vya kienyeji mnatuponza. mnapitishaje kitu kama hiyo bwana,”amesema.

Mwananchi
 
Nakumbuka enzi za jk nchi imekaribia kuanguka wananchi wakiwa wanapiga kelele huku chamani wakiitana "mizigo" Boys 2 men yy alikuwa zake mara sijuhi wapi huko akibembea mara yuko south anaomba misaada. Kama vipi ndugai anaona tozo za bibi zinamkereketa achukue maamuzi tu ama la akubali kuufyata
 
Spika wa Bunge, Job Ndugai ametishia kuifumua Kamati ya Bunge ya Bajeti baada ya kukerwa na kupitishwa kwa sheria inayoruhusu Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kuanza kutoza ushuru wa bidhaa wa asilimia mbili kwa mazao nchini.

Spika Ndugai ameyasema hayo leo Jumatatu Septemba 6, 2021 bungeni mara baada ya majibu ya Wizara ya Kilimo yaliyotokana na swali la nyongeza la Mbunge wa Namtumbo (CCM), Vita Kawawa.

Kawawa amesema wakulima wa tumbaku wamekuwa wanalipa ushuru wa wilaya wa mazao, tozo ya vyama vikuu vya ushirika, chama cha msingi.

Amehoji kama ni kweli kuwa TRA mwaka huu itaanza kuwatoza wakulima wa tumbaku ushuru wa bidhaa.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema ni kweli Bunge lilipitisha sheria ya ushuru wa bidhaa wa asilimia mbili kwenye mazao ya kilimo.

Hata hivyo, amesema bado wizara haijaanza kukata ushuru huo kwasababu mjengeko wa bei ya tumbaku huamuliwa kati ya Februari hadi Aprili. Amesema wakati sheria hiyo inapitishwa tayari mjengeko wa bei wa zao hilo ulikuwa umeshapitishwa.

Hata hivyo, amesema wizara yake imewasiliana na Wizara ya Fedha na Mipango kwa kuwaandikia ili kuona namna gani watatekeleza sheria hiyo lakini kwa kulinda maslahi ya wakulima wa zao hilo.

Ndugai amesema wajumbe wa bajeti wanapaswa kuwa makini sana katika kazi zao kwasababu mambo yakifika bungeni wanaiamini kamati.

“Mkiendelea hivi nitaifumua hiyo, kamati ya bajeti tumeweka watu tunaowaamini sana. Sasa kama mnaenda kule mnalala tu na kupitisha tu vitu vya kienyeji mnatuponza. mnapitishaje kitu kama hiyo bwana,”amesema.

Mwananchi
Hivi tuna bunge tuna bangi?

Huyu mtu anaongoza bunge linapitisha vitu halafu anaanza kushangaa. Haya mambo yakipitishwa yeye anakuwa wapi?
Tunahitaji katiba mpya ili watu kama hawa wasiingie bungeni.

Kuwa na bunge la hivi ni suicide mission kwa taifa la leo na kesho.
 
Naunga mkono HOJA...

Mh.Spika Ndugai yuko sahihi sana....

Ni lazima wabunge wa hiyo kamati wawe makini ili kuitekeleza vyema ilani bora ya uchaguzi ya CCM......
 
Anawafanya wagogo wote waonekane wapuuuzi wapuuuzi
Unawatukanaje kabila zima kwa kuwa tu una chuki na mh.Spika Ndugai?!!!

Mh.Ndugai yuko sahihi....mpinge tu kwa kuwa una "mbango" zako.....

#SiempreJMT
 
Mh. Ndugai kuna wakati yuko vizuri sana ila sijui muda mwingine huwa anayumba wapi.
Kwa hyo yeye ndiye bunge? Ujinga huu hadi lini? Kwamba asipokuwepo madudu yanapitishwa. Tunahitaji watu wenye akili siyo ndumba.
Watu wenye kujali taifa na kulisimamia kwa maslahi ya sasa na vizazi vijavyo dhidi ya uvamizi wa ndani na nje kwa misingi yoyote iwe ya kidiplomasia, kiteknolja, kijogiraphia, kiuchumi, jamii,, biologia n.k.

Ukiwa na watu waina mbovu, hawajui ulimwengu unakwenda je na nini madhara ya kusinzia bila kuona nini kipo katikati ya mistari. Wanachokifanya ni kulinda maslahi yako binafsi ili wasijekutolewa, wanapitisha kilakinachokuja mezani bila kujua kina maslahi ama madhara gani, wanatumia muda kujadili watu wenye ufahamu kliko wao badala ya kuajdili hoja.

Hii ni nini? Katiba mpya ni muhimu.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom