Ndugai aonesha ubabe wake. Yeyote anayetaka kumtunishia misuli lazima afikirie mara mbili

James Martin

JF-Expert Member
Apr 2, 2016
1,101
2,000
Leo Spika wa bunge, Mh. Job Ndugai amenifanya nikumbuke mhimili wa bunge una nguvu kiasi gani.

Baada ya kutoa adhabu kwa Mh. Jerry Slaa na Gwajima, Mh. Ndugai alikwenda mbali zaidi na kuhoji watendaji wa serikali kama waziri wa mambo ya ndani. Alishangazwa ni kwanini vyombo vilivyo chini ya wizara hiyo vimeshindwa kuwachukulia hatua wabunge hao wawili.

Mbali na kuhoji kwake, Mh. Spika pia aliwakumbusha watendaji wa serikali kwamba kama watashindwa kufanya majukumu yao ipasavyo nao pia wanaweza kuwekwa kikao na kujadiliwa.

Jambo la Mh. Slaa na Gwajima linaigusa sana wizara ya mambo ya ndani. Hii inatufanya tukumbuke kwamba mbali na hatua zinazoweza kuchukuliwa ndani ya bunge lakini pia bunge lina ushawishi mkubwa sana kwenye mambo mengine yanayotokea nje ya mhimili huo.

Maoni yangu kwa hawa wabunge watukutu wanaotaka kumtunishia misuli Mh. Spika ni kwamba wawe wapole tu. Spika anaweza kuwachapa ndani na nje ya bunge pia! Watoto wa mjini wanasema mboga moto, ugali moto!
 

Abuu Kauthar

JF-Expert Member
Jul 10, 2011
3,662
2,000
Gwajima alikuwa anajazwa ujinga na misukule yake, hawezi kushinda hoja yoyote wakati akiwa na ndimi mbili
 

sinajinasasa

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
2,585
2,000
Ndugani naye ni shetani tu, yupo kwa ajili ya ma Illuminatti ndo wanamtuma!!!
Hilo ni joka la kupigwa...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom