Ndugai anawaonea wivu Wanasheria kujiita ‘wasomi’? Bila shaka atawaandalia Muswada

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,134
2,000
Kiukweli kwa kadri ya kumbukumbu zangu sijawahi kuona spika duni kama spika wa bunge la Tanzania , sasa sijui shida iko wapi , yaani anaona wivu hadi anakonda kwa Wanasheria kujiita "WANASHERIA WASOMI" kiasi cha kuanzisha mada bungeni ya kujadili jambo hili yaani !

Tutarajie muswada wa kufuta huo usomi hivi karibuni

View attachment 1920289
Kama wabunge wanavyotumia neno 'mheshimiwa', mahakamni wanasheria/mawakili wanakuwa addressed kama 'learned brothers' na nadhani ndiyo tafsiri ya 'mwanasheria msomi' au 'wanasheria wasomi'. Na hawajiiti, wanaitwa. Ni kama padri anavyokuwa addressed kama Fr au askofu Mhashamu na papa, Baba Mtakatifu (kwa upande wa Kanisa Katoliki).
 
Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
4,855
2,000
Kiukweli kwa kadri ya kumbukumbu zangu sijawahi kuona spika duni kama spika wa bunge la Tanzania , sasa sijui shida iko wapi , yaani anaona wivu hadi anakonda kwa Wanasheria kujiita "WANASHERIA WASOMI" kiasi cha kuanzisha mada bungeni ya kujadili jambo hili yaani !

Tutarajie muswada wa kufuta huo usomi hivi karibuni

View attachment 1920289
Naye angeacha kupenda kuitwa mheshimiwa spika kwani binadamu wote tunastahili heshima.
 
The 5

Member
Sep 3, 2016
14
45
Yaani kumiliki KAHOTELI kamumeo pale Mbeya na vibiashara unavyovitangaza msimu wa 7/7 basi unatuona sote "mahobobo malofa" si ndio eee?!!!

Mshukuruni sana hayati JPM(Rip) kwa kutobomolewa kule.....
Wa kiume alafu unakuwa na maneno ya kike. Acha upuuzi!
 
Silasy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
772
1,000
Mh.Spika Ndugai yuko sahihi sana.....

Ameamua kuivunja minyororo ya mazoea ya kijinga.....

Mathalani hivi ni nani awezaye kuwa WAKILI bila ya kusoma?!!!

Kwanini tutangulize "wakili msomi"?!!!!

Namuunga mkono Spika wetu Mtunduizi

MWENYEZI MUNGU AMBARIKI NA KUMLINDA MH.SPIKA JOB NDUGAI ,AMEEN AMEEN

#NchiKwanza
#SiempreJMT
Hapo kwenye usomi hata mm nimekuwa nikijiuliza nani wakili asiye msomi?sipati jibu .Mpk leo sijaelewa nn hasa maana ya kutanguliza neno msomi lkn ndio ilivyo tunafanyaje lbd Ilmu yao inawaruhusu kuitwa hivyo!
Kwa upande wa Madaktari amegusia km moja ya fani "zinazojikweza" kwa kujiita Daktari "Bingwa" au "Mbobezi "atleast hapa ninaweza nikamsaidia hapa hakuna janja janja ni mabingwa kweli!ila hiyo hali ya kukwezwa inatokana pia na lugha yetu ya Kiswahili kukosa tafsiri nyingine ili kukielezea kiingereza cha neno "Specialist au super specialist"NB upande huu Mh atulie tu mpk BAKITA watakapo kaa na kutoa majina mengine sahihi zaidi.
NB kila mtu anatamani atambuliwe kwa cheo na Elimu yake sawa na wao kuitwa "Waheshimiwa" sometimes unakaa unajiuliza kuna binadamu wengi hatuheshimiwi? Km hivyo basi na tuvumiliane na tubebeane mizigo.
 
Mh370

Senior Member
Mar 23, 2014
166
250
Kiukweli kwa kadri ya kumbukumbu zangu sijawahi kuona spika duni kama spika wa bunge la Tanzania , sasa sijui shida iko wapi , yaani anaona wivu hadi anakonda kwa Wanasheria kujiita "WANASHERIA WASOMI" kiasi cha kuanzisha mada bungeni ya kujadili jambo hili yaani !

Tutarajie muswada wa kufuta huo usomi hivi karibuni

View attachment 1920289
Mh.Wao wanaitana hivyo wakiwa mahakamani, ni heshima wanapeana kwa miaka mingi sana, na ni protokali za taaluma yao.hawaforce mtu yeyote wa nje ya taaluma yao kuwaita hivyo ,rather anatajwa jina la Wakili tu, ni kama Majaji au Mahakimu huku nje wanawaita tu Waheshimiwa ila mahakamani huitwa "My Lords/Your Honor) so hizo ni itifaki zao na hazilazimishi mtu wa nje kuwaita hivyo. hizi taaluma alizotaja zinaitwa Noble Professions, hiyo ndio ilivyo na haibadiliki na hakuna sheria inavunjwa wala inaelekeza hizo ni tamaduni.
 
JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
4,032
2,000
Kiukweli kwa kadri ya kumbukumbu zangu sijawahi kuona spika duni kama spika wa bunge la Tanzania , sasa sijui shida iko wapi , yaani anaona wivu hadi anakonda kwa Wanasheria kujiita "WANASHERIA WASOMI" kiasi cha kuanzisha mada bungeni ya kujadili jambo hili yaani !

Tutarajie muswada wa kufuta huo usomi hivi karibuni

View attachment 1920289
Richa ya kwamba huyu jamaa huwa namuona chenga,ila ana hoja nzito.
Kuna umuhimu gani wa kuitwa "msomi"
Wakati wewe tayari ni msomi?hayo matitle si unayo kwenye CV yako?
Kibongo bongo,kuitwa kwa title watu huona ufahari kwa sababu ya low self esteem,mtu kama Mwigulu na PHD yake ya kuunga unga hasemi kitu mpaka aseme Mimi Dokta wa uchumi,wakati kichwa kimejaa ma theory matupu.
Deputy president wa Kenya,William Ruto ni PHD holder,lakini huwezi kusikia akitumia DR Ruto
 
broken ages

JF-Expert Member
Mar 23, 2012
227
225

hapa spika hajatendea haki kiti na muda ambao ungetumika kujadili mambo yenye maana kidogo hapa anajishushia heshima na maana ya kuwa spika

kwa sababu hata tungesema na kukubaliana kwamba wanasheria wasijiite wasomi sidhani kama dhana hiyo itakuwa ndiyo majibu ya matatizo na shida za wananchi wa Tanzania

siamini kama yupo mwananchi ambaye angependa ama kufutahi kumsikia mbunge wa jimbo lake akichangia hoja na kujadili habari ya nani anjiita msomi ama dr.

yote katika yote tumsamehe maana pia umri nao umesonga kidogo.
 
broken ages

JF-Expert Member
Mar 23, 2012
227
225
S
Richa ya kwamba huyu jamaa huwa namuona chenga,ila ana hoja nzito.
Kuna umuhimu gani wa kuitwa "msomi"
Wakati wewe tayari ni msomi?hayo matitle si unayo kwenye CV yako?
Kibongo bongo,kuitwa kwa title watu huona ufahari kwa sababu ya low self esteem,mtu kama Mwigulu na PHD yake ya kuunga unga hasemi kitu mpaka aseme Mimi Dokta wa uchumi,wakati kichwa kimejaa ma theory matupu.
Deputy president wa Kenya,William Ruto ni PHD holder,lakini huwezi kusikia akitumia DR Ruto
siyo swala la kujadiliwa bungeni wabunge wanayo mambo mengi sana na ya msingi ya kujadili

wabunge siyo wasanifu wa misamiati na misemo
 
Uwazitu

JF-Expert Member
Aug 19, 2019
1,420
2,000
Mh.Spika Ndugai yuko sahihi sana.....

Ameamua kuivunja minyororo ya mazoea ya kijinga.....

Mathalani hivi ni nani awezaye kuwa WAKILI bila ya kusoma?!!!

Kwanini tutangulize "wakili msomi"?!!!!

Namuunga mkono Spika wetu Mtunduizi 👍💪💪

MWENYEZI MUNGU AMBARIKI NA KUMLINDA MH.SPIKA JOB NDUGAI ,AMEEN AMEEN 🙏

#NchiKwanza
#SiempreJMT
Hata Madiwani, Wabunge, Makatibu Wakuu, Mawaziri na Rais KUANZA na Mheshimiwa inakera sana.

Ina maana Watumishi wa kada zingine hawapaswi KUHESHIMIWA?

NAKUMBUKA KUNA WAKATI MWL. NYERERE ALIFUTA (ALIKATAA) NENO MHESHIMIWA AKAELEKEZA NENO NDUGU LITUMIKE ILI KULETA USAWA NA UPENDO.
 
Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
3,090
2,000
Mh.Spika Ndugai yuko sahihi sana.....

Ameamua kuivunja minyororo ya mazoea ya kijinga.....

Mathalani hivi ni nani awezaye kuwa WAKILI bila ya kusoma?!!!

Kwanini tutangulize "wakili msomi"?!!!!

Namuunga mkono Spika wetu Mtunduizi 👍💪💪

MWENYEZI MUNGU AMBARIKI NA KUMLINDA MH.SPIKA JOB NDUGAI ,AMEEN AMEEN 🙏

#NchiKwanza
#SiempreJMT
Nakubaliana na wewe.

Wakati mwingine saa mbovu husema ukweli.

Mimi wanasheria kujiita wasomi ama kuvaa yale mavazi yao ya ajabu ajabu na majaji kuvaa mawigi ni jambo linanisikitisha sana.

Siku hizi wahasibu hasa wa Tanzania wanataka waitwe CPA flani, hii iko Tanzania tu sijawahi kuisikia mahala popote Duniani wahasibu kujiita CPA flani.

Tuache ulimbukeni.
 
Townchild

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
7,571
2,000
Kiukweli kwa kadri ya kumbukumbu zangu sijawahi kuona spika duni kama spika wa bunge la Tanzania , sasa sijui shida iko wapi , yaani anaona wivu hadi anakonda kwa Wanasheria kujiita "WANASHERIA WASOMI" kiasi cha kuanzisha mada bungeni ya kujadili jambo hili yaani !

Tutarajie muswada wa kufuta huo usomi hivi karibuni

View attachment 1920289
Sitashangaa kwani ndio weledi wa kitanzania.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom