Ndugai amvaa Sumaye, asema hana usafi wa kubeza posho!

Huyu Ndugai ni mpuuzi kweli kwahiyo hao wabunge wanaishi kwenye kisiwa ambacho wastaafu na wananchi wengine hawaruhusiwi kuhoji au kutoa maoni kuhusu mstakabali wa nchi yao, posho ni mzigo kwa taifa hata kama Sumaye ni mchafu lakini ukweli ndo huo watanzania wengi wanasikitishwa na kulipana posho.
 
i read once that some well known majambazi are holding his constituency as their own animal farm for decades under his watch! Wat if akiwa rais si ndio atawapa nchi kabisa?

To this day, wananchi are still wondering how comes watu wanajigamba wameweka serikali mfukoni na kweli hawafanywi kitu?

One day wananchi will do the needfull to liberate themselves!

:embarassed2:

0
digg

Naibu Spika wa Bunge,Job Ndugai

ASEMA HANA USAFI WA KUBEZA NYONGEZA YA POSHO
Fredy Azzah
NAIBU Spika wa Bunge, Job Ndugai amemjia juu Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye kuhusu kauli yake ya posho za wabunge, akisema hakupaswa kuitoa kwani aliwahi kufanikisha kupitishwa sheria ya malipo kwa viongozi wakuu wastaafu ili kujinufaisha akistaafu.Juzi, Sumaye pamoja na mambo mengine, alizungumzia mwelekeo wa taifa kwa sasa na kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015 huku akisema mpango wa ongezeko la posho za wabunge unapaswa kuachwa kwani unaweza kufanya makundi mengine ya utumishi wa umma kudai nyongeza.

Kauli hiyo ilijibiwa vikali jana na Ndugai ambaye aliwatahadharisha viongozi wastaafu kuwa makini na kauli wanazotoa na kuwataka wale ambao wanataka urais wa 2015 ikiwa ni pamoja na Sumaye waseme sasa badala ya kuwababaisha Watanzania kwa kuzungumza mambo mbalimbali ili wawapende.

Alisema wakati Sumaye anazungumzia posho za wabunge, sheria ya kuwalipa viongozi wastaafu mafao ilipitishwa wakati akiwa kiongozi wa shughuli za Serikali bungeni na hakuipinga kwa kuwa alikuwa anajiandalia mazingira ya kustaafu.
“Kwa sasa analipwa asilimia 80 ya mshahara wa waziri mkuu aliyepo madarakani, ni fedha nyingi kuliko hata mshahara wa Naibu Spika (Ndugai kwa sasa), wakati sheria hii inapitishwa alikuwa kiongozi wa shughuli za Serikali bungeni (Waziri Mkuu), alikuwa anajiandalia mazingira ya kustaafu,” alisema Ndugai na kuongeza:

*“Sitaki kuendelea kusema sana jinsi ambavyo ananufaika, lakini ninachosema viongozi wastaafu duniani kote inatakiwa wawe makini na kauli zao. Wakianza kwenda kwenye vyombo vya habari na kusema maneno haya haipendezi.”
Alifafanua kwamba badala ya kuzungumzia posho za wabunge pekee ni vyema pia likazungumziwa suala la posho kwa viongozi wote wa umma.

“Kwa watu wanaotaka kugombea urais mwaka 2015 ni bora waseme sasa. Waache kutubabaisha Watanzania… nasema viongozi wastaafu lazima wawe makini kwa kauli zao, mimi Sumaye ninamheshimu sana na ninatambua haki yake ya kikatiba ya kujieleza,” alisema na kumshauri kuwa makini na kauli zake anapozungumza juu ya Bunge kwa sababu yeye pia alikuwa sehemu ya mhimili huo.

“Yeye ni kama mchezaji mstaafu wa timu hii (Bunge), inatakiwa awe makini sana hawezi kuizungumzia hii timu kama mshabiki mwingine,” alisema Ndugai.

Ndugai alisema posho zilikuwepo tangu enzi za Sumaye akiwa mbunge, naibu waziri na hatimaye waziri mkuu na kwamba kama hoja ni kiasi cha fedha... “Aseme ni kiasi gani wabunge wanapaswa kulipwa.”
Sumaye aliingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 1985 baada ya kushinda ubunge katika Jimbo la Hanang na mwaka 1987, aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo hadi mwaka 1994 alipoteuliwa kuwa waziri kamili katika wizara hiyo.

“Mimi nakwambia kitu ambacho nakijua na wakati huo nilikuwa bungeni kama mbunge na Sumaye alikuwa akizipokea hizi posho, Rais (Ali Hassan) Mwinyi aliwahi kusema kila zama na kitabu chake, hebu na yeye (Sumaye) atuache na sisi tuandike kitabu chetu,” alisema Ndugai.

Dk Bana abeza
Akizungumzia kauli ya Sumaye, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana alisema mambo aliyozungumza si mapya na huku akimtaka kutazama kila neno linalotoka mdomoni mwake.

Dk Bana alisema kauli ya Sumaye kuhusu matumizi ya taasisi ya urais, inaweza kutafsiriwa kwamba inatokana na yeye kuwa na uchungu wa kuikosa alipogombea na Rais Jakaya Kikwete katika uchaguzi wa ndani wa CCM.

Sumaye katika kinyang’anyiro cha kupenya kura za maoni kwa ajili ya kupeperusha bendera ya CCM baada ya Mkapa, alishika nafasi ya tano na kushindwa kuingia hata tatu bora ambayo waliingia Rais Kikwete, Dk Salim Ahmed Salim na Profesa Mark Mwandosya.

“Kwanza anavyozungumzia taasisi ya urais hatujui kama ni hii au ni zilizopita, lakini ikumbukwe kuwa aligombea nafasi hiyo akaikosa kwa hiyo kuna uwezekano kuwa ni roho inamuuma,” alisema Bana.

Kuhusu suala la rushwa katika uchaguzi alisema: “Suala hili lilikuwepo kwa muda mrefu na limepigiwa sana kelele, yeye hakuweza kumshauri Rais (Benjamin) Mkapa kuwa watunge sheria ya kupambana na hali hii, lakini sasa hivi Serikali imejaribu inatakiwa aipongeze kwa hilo,” alisema Dk Bana.

Alisema hata baada ya kuundwa kwa sheria hiyo, viongozi wengi wakubwa ikiwa ni pamoja na wale wastaafu hawaonekani kuipigia debe.

Dk Bana alisema kuundwa kwa sheria ni jambo moja na kinachotakiwa sasa ni utekelezaji wake kufanyiwa kazi.
Alisema pia ingekuwa jambo jema endapo viongozi wastaafu wangeunda taasisi yao ili waweze kushauri Serikali ili busara zao ziweze kutumika vyema huko... “Yeye ana nafasi kubwa sana ya kuzungumza haya mambo ndani ya chama na pia hata kumshauri Rais moja kwa moja.”

Kuhusu suala la posho kwa wabunge, alisema Sumaye alilizungumza vizuri na inatakiwa aungwe mkono na watu wengine.

Alichosema Sumaye
Akizungumza kupitia kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha ITV, Sumaye alisema ongezeko la posho za wabunge linaweza kuchochea makundi mengine kama wanajeshi, polisi, Mahakama na walimu nao kutaka nyongeza, hivyo kumweka Rais katika wakati mgumu kufanya uamuzi.

“Mwanasiasa mzuri akifanya jambo akiona limewaudhi wananchi anatakiwa aliache, lakini pia kwenye hili huu mkanganyiko wa Spika na Katibu wake na huu ukimya wa Ikulu ni tatizo, tungependa waseme ili umma ujue hali ikoje?” alisema Sumaye.

Alisema hatua ya Bunge kujipandishia posho ya kikao kutoka Sh70,000 hadi Sh200,000 kwa siku haliingii akilini na kwamba, inakiuka utaratibu uliowekwa na Serikali katika kulipa gharama kwa maofisa wake ikiwa ni pamoja na gharama hizo za fedha za kujikimu.

“Siyo kwamba napinga posho, wabunge wanastahili posho, lakini kwa kweli kujiongezea kutoka Sh70,000 hadi Sh200,000 siyo sahihi,” alisema Sumaye.

Alisema wakati alipoteuliwa na Rais Benjamin Mkapa kwa Awamu ya Pili kushika wadhifa wa Waziri Mkuu, aligoma kwa sababu alikuwa amekwaruzana na wabunge kuhusu nyongeza ya posho.

“Nilimwambia wabunge watanikataa kwa sababu nimegombana nao sana juu ya suala la posho lakini akasema lazima uwe na mimi ndipo nikakubali, lazima hili suala liangaliwe mara mbilimbili… leo wabunge mmejiongezea kesho jeshi, polisi na walimu nao watataka, tutafanyaje tusifanye mambo ambayo yatamuweka Rais pabaya,” alisema Sumaye.

Alisema posho ni jambo ambalo kwa sasa limekuwa tatizo kwa serikali na kwamba imefika wakati ofisi za Serikali zimehamia hotelini, lengo likiwa ni watumishi wa umma kutafuta mwanya wa kulipana
 
Attachments

  • himaya ya majambazi.jpg
    himaya ya majambazi.jpg
    146.2 KB · Views: 36
Ndugai endeleeni kuandika vitabu vyenu maana hizi ni zama zenu , nasisi wananchi wakawaida tumeanza kuandika kitabu chetu tupo page 2 natumai wakati nasi utafika tutaanza kukisoma.................hongereni kwakuitafuna national cake vizuri wakati sie twalala njaa
 
“Sitaki kuendelea kusema sana jinsi ambavyo ananufaika, lakini ninachosema viongozi wastaafu duniani kote inatakiwa wawe makini na kauli zao. Wakianza kwenda kwenye vyombo vya habari na kusema maneno haya haipendezi.”

Rais (Ali Hassan) Mwinyi aliwahi kusema kila zama na kitabu chake, hebu na yeye (Sumaye) atuache na sisi tuandike kitabu chetu,” alisema Ndugai.

Simtetei Sumaye na wala sina haja ya kujua anataka urais 2015. Hoja ya msingi iko wazi tu. Si busara kwa viongozi kundelea kujinufaisha wenyewe wakati wananchi wao wanakufa na njaa. Job ni Mkristu, na Maisha ya Sauli katika biblia anayajua sana. Sauli alifanya matendo yasiyompendeza Mungu (alimuudhi Mungu). Baadae alitambua wajibu na mchango wake katika jamii. Akamgeukia Mungu, naam na akawa Paulo kama anavyofanya Sumaye katika eneo la posho!

Viongozi wetu wageukieni watu wenu, acheni visingizio vya mbio za Uongozi. Geukeni hilo ndo la Muhimu. Haya mengine ni kuendeleza malumbano tusiyohitaji. Maisha yenu, hata bila kujitetea hivyo yanaonyesha jinsi mnavyoishi peponi. Pesa ina harufu. Acheni bla bla, jengeni TAIFA lililo sawa na watu huru. Aaaaaaagrrrr!!!!!!!!!!
 
Kuna mistari nilisoma kwenye Biblia yangu takatifu na nanukuu...

"HATA MPUMBAVU AKINYAMAZA UHESABIWA HAKI..."

Sasa, kwani huyu Ndungai alilazimishwa kuzungumzia swala la Posho..?
Na kama hapana mbona amenifanya na Mimi ambaye nilikuwa namweshimu na kumwona kama ananafuu kati ya wale wengine,, nimwone walewale tu..

Nikiwa nasoma hayo maneno ya ndungai,,huku feni ikiwa inanipepea gafla kajasho ka presha kalianza kunitoka na kuingiwa na hofu...
Macho yangu yaliendelea kusoma lakini midomo yangu ikitoa matusi machafu(kimyakimya) matusi ambayo sikumbuki lini niliyatukana..(MUNGU ANISAMEHE)

Ngoja niwambie nilichogundua na Ndiyo uhalisia wa mambo...

ndungai ni MPUMBAVU toka kitambo ila ukimya wake ulimuhifadhi..
Sasa kulopoka kwake kumemfanya nigundue kuwa ni MPUMBAVU KIONGOZI..!!
Baada ya kujibu Hoja za msingi za Sumaye,,anajibu kimajungu tu na umbea..
Eti uchaguzi 2015..
Umbea tu,yani hata kijiweni kwetu sikuhizi (watu ambao wengi wetu hatuna hata elimu ya 4m 4)..
Tusingejibu huu Ujinga aliojibu ndungai..
Sumae anasema hata kama kupandisha posho 70, mpaka 200, ni jambo lisilovumilika..sio kwa sumaye na watanzania wenye haki ya kupiga kura 2015..
Halivumiliki hata kwa watoto wadogo..

Siku nyingine kwa Ndungai na Viongozi wengine Ropo,ropo tafakarini kabla hamjasema hzo pumba zenu kwanu hamna makatibu jamani..!
Kauli zenu zinachefua na laiti kama unaongea na mimi niko karibu,, yangekukuta yaliyo mkuta Mwinyi...
 
Ndungai kaongea upuuzi basi itaonekana katika chama tawala kama kaongea hoja ya maana kwanza napenda kusema kuwa sheria ya kupitisha viongozi wa kuu wa serikali kama Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kulipwa asilimia 80 ya mshahara wa aliyepo madarakani ilikuwa na lengo zuri la kuwafanya viongozi hawa wasiibie taifa kwa kuhofia pindi watokapo madarakani wataishi kwa shida, pili kuwafanya wasibadili katiba kwa kuhofia maisha magumu wakatawala milele kama Museveni na Mugabe

Kuhusu Ndungai kusema Waziri Mkuu mstaafu analipwa pesa nyingi kuliko yeye naibu spika ningependa kusema huo wadhifa wake hauna umuhimu wowote kwa taifa la Tanzania kama alivyo waziri mkuu kwa Tanzania spika wa bunge anatosha na akiwa hayupo kuna wenyeviti wa muda huchaguliwa kuendesha bunge kwa hiyo Tanzania inaweza kwenda mbele bila naibu spika hana umuhimu wowote na isitoshe kawekwa pale na mafisadi yeye na Anna Makinda spika ili kuwatumikia

Mwisho ningependa kusema serikali haiitaji miaka kumi ili ilinganishwe na nyingine miaka sita inatosha kutoa tathimini au Ndungai anataka tutoe tathimi ya mwaka 2001 wakati Mkapa akiwa madarakani? pamoja na wizi wake serikali yake haikuwa na mfumuko wa bei kama hii na pesa ilikuwa na thamani, pia anaposema Sumaye anataka kuwania urais kwani ni dhambi? na mtaji wa mwanasiasa ni kuongea mabaya ya serilikali iliyopo na yeye atafanya nini kuondoa hayo mabaya hiyo ndio mitaji ya wanasiasa na vyama vya siasa vinavyotaka kushika dola
 
CCM ni noumer...yaani mwenzako akikumwagia mboga wewe unamwaga ugali. Magamba yote ni machafu.
 
Reasoning ya Mr. Ndugai kama kiongozi ipo chini sana.

Mkuu umenena. Hakuna cha maana alichoongea Ndugai ambacho kinajaribu kufanana na U-naibu spika! Shame on him! Hivi huwa hakuna vigezo vya kugombea nafasi kama ya U-naibu Spika? Kwa mtazamo wangu tokea siku ya kwanza alipoipata nafasi aliyonayo nilimuona kwamba hana uwezo wa kuongoza, kutoa msimamo, wala kujenga hoja! Like other magambas yeye anawaza POSHO tu na mipasho! Hakuna magamba wa mjengoni asiyekuwa muimba taarabu! Go to hell Ndugai!
 
Nilikuwepo Bungeni Dodoma wakati sakata la Luhanjo/Jairo/Pinda limepamba moto. Ndugai alili-"handle" vizuri hadi kuwa hivi lilivyo sasa. Mnakosea tu kumjadili yeye badala kujadili alichokisema!
 
Mimi namsamehe Ndungai kwani he is an idiot who happens to be naibu spika. Ila nimeshtushwa na kauli ya Dr. Benson Bana kwamba "kauli ya Sumaye kuhusu matumizi ya taasisi ya urais, inaweza kutafsiriwa kwamba inatokana na yeye kuwa na uchungu wa kuikosa alipogombea na Rais Jakaya Kikwete katika uchaguzi wa ndani wa CCM." Jamani inatia huruma sana kama hizi ndivyo wasomi wetu wanavyojenga hoja, halafu cha kusikitisha zaidi nilivyosearch jina la huyu bwana niligundua kuwa ni Head of Department ya political science. Hivi hizi PhD zao zinasaidia nini haswa nchi? Kweli elimu imeshuka...
 
Nilikuwepo Bungeni Dodoma wakati sakata la Luhanjo/Jairo/Pinda limepamba moto. Ndugai alili-"handle" vizuri hadi kuwa hivi lilivyo sasa. Mnakosea tu kumjadili yeye badala kujadili alichokisema!

Ndugu, kimtokacho mtu ndicho kilichomjaliza...
Aliyoyaongea Ndungai ndo ndungai mwenyewe..
Yani ameongea urofa thn amequalify kuwa Lofa...
Amejibu ujinga,thn amequalify kuwa Mjinga..
Sio mara zote chizi anavua Nguo..
Au kuvaa kwake nguo ndo kumwondelee yeye Uchizi..
Kuandle hishu ya Jairo na Upuuzi alioöngea anamaana yeye ni chizi aliyekuwa kavaa nguo na sasa kazivua sasa..
Kama naibu spika wa bungu letu..
Mim binafsi naona noma kwa kauli yake..
Wew..?!
 
Sijaelewa kama Ndugae anasema wao wamejitengenezea mazingira ya kujinufaisha kwa kutumia nafasi yao Bungeni kwa vile kina Sumaye nao walitumia nafasi hiyo hiyo kujinufaisha? Au amesema nini hasa?
Mimi ndivyo nilivyomuelewa.... la sinyo atueleze anamaanisha nini anaposema na wao waachwe waandike vitabu vyao kwa sababu kila zama ina kitabu chake. Je, kama akima Sumaye walifanya makosa, anadhani yatarekebishwa kwa wao nao kufanya makosa? Huyu jamaa hastahili kuwa katika nafasi aliyopo
 
Nilikuwepo Bungeni Dodoma wakati sakata la Luhanjo/Jairo/Pinda limepamba moto. Ndugai alili-"handle" vizuri hadi kuwa hivi lilivyo sasa. Mnakosea tu kumjadili yeye badala kujadili alichokisema!

Hivi Huyo Ngugai ..amejibu hoja au amemuongelea Sumaye?.......kwani sum aye aliongelea issue ya posho Kama issue au alimuongelea spike au naibu wake in personal level....?
Napata mashaka Kama mtu yeyote mwenye akili anaweza kumtetea Ndugai au Makinda.....
 
Ndugai kaongelea kauli ya kinafiki ya FTS juu ya posho za Wabunge. Ndugai kamkumbusha tu FTS baadhi ya maamuzi yaliyowahi kufanywa na Bunge lililopita wakati akiwa KIONGOZI wa shughuli za serikali Bungeni. Unadhani ni kwa nini Ndugai hakuwajibu watu wengine wengi tu walioliongelea suala hili?
 
Wacheni umbea kama nna nia ya kugombea si mjitokeze hadharani? malumbano ya nini hata Ndugai?CCM mmekwisha
 
0
“Mimi nakwambia kitu ambacho nakijua na wakati huo nilikuwa bungeni kama mbunge na Sumaye alikuwa akizipokea hizi posho, Rais (Ali Hassan) Mwinyi aliwahi kusema kila zama na kitabu chake, hebu na yeye (Sumaye) atuache na sisi tuandike kitabu chetu,” alisema Ndugai.

Sijaelewa kama Ndugae anasema wao wamejitengenezea mazingira ya kujinufaisha kwa kutumia nafasi yao Bungeni kwa vile kina Sumaye nao walitumia nafasi hiyo hiyo kujinufaisha? Au amesema nini hasa?

kosa + kosa = sahihi?!?!

Kweli si vibaya kila zama kuwa kitabu chake; lakini katika kutengeneza kitabu kipya, ni vyema kujifunza na kuzingatia yale mazuri yaliyomo kwenye kitabu cha zama za kale.

Katika kujifunza ndio kasheshe kwa viongozi wa Tanzania yetu; wao ujifunza yale mabaya na kuacha mazuri. Hata Mwalimu alishawahi kuliongelea hili (ingawa hilo ni debate nyingine kabisa), kwamba watu wamejifunza mabaya na kuacha mazuri yake.

Sasa huyu Ndugai anavyokuja na sweeping statement kama hiyo sijui anataka awekwe kwenye kundi lipi!!!
 
jamani hawa viongozi mimi sijui wanacho kizungumza jamani wanaishi chungu kimoja alafu wanapigana wao kwa wao si balaa hiliii
 
Mimi namsamehe Ndungai kwani he is an idiot who happens to be naibu spika. Ila nimeshtushwa na kauli ya Dr. Benson Bana kwamba "kauli ya Sumaye kuhusu matumizi ya taasisi ya urais, inaweza kutafsiriwa kwamba inatokana na yeye kuwa na uchungu wa kuikosa alipogombea na Rais Jakaya Kikwete katika uchaguzi wa ndani wa CCM." Jamani inatia huruma sana kama hizi ndivyo wasomi wetu wanavyojenga hoja, halafu cha kusikitisha zaidi nilivyosearch jina la huyu bwana niligundua kuwa ni Head of Department ya political science. Hivi hizi PhD zao zinasaidia nini haswa nchi? Kweli elimu imeshuka...

Mkuu kwa kweli ukiwa mchumia tumbo hata ungekua umepata PhD kutoka Harvard, Oxford, Cambridge, Yale, Manchester, Birmingham, Princeton et al., hakika utaonekana a dufus or yo-yo tu!

Hawa "wasomi" wetu elimu zao hazijawaelimisha; haiwezekani mtu mwenye PhD aka-act kama huyo Benson Bana. Elimu inapaswa imfanye mtu asiwe sycophant.

Vibaya zaidi wengi wa wasomi wetu hapa Tanzania ni sycophants; Bana ni mmoja wao tu ambae anatokea kwenye media mara kwa mara!
 
Kuna mistari nilisoma kwenye Biblia yangu takatifu na nanukuu...

"HATA MPUMBAVU AKINYAMAZA UHESABIWA HAKI..."

Sasa, kwani huyu Ndungai alilazimishwa kuzungumzia swala la Posho..?
Na kama hapana mbona amenifanya na Mimi ambaye nilikuwa namweshimu na kumwona kama ananafuu kati ya wale wengine,, nimwone walewale tu..
Nikiwa nasoma hayo maneno ya ndungai,,huku feni ikiwa inanipepea gafla kajasho ka presha kalianza kunitoka na kuingiwa na hofu...
Macho yangu yaliendelea kusoma lakini midomo yangu ikitoa matusi machafu(kimyakimya) matusi ambayo sikumbuki lini niliyatukana..(MUNGU ANISAMEHE)

Ngoja niwambie nilichogundua na Ndiyo uhalisia wa mambo...

ndungai ni MPUMBAVU toka kitambo ila ukimya wake ulimuhifadhi..
Sasa kulopoka kwake kumemfanya nigundue kuwa ni MPUMBAVU KIONGOZI..!!
Baada ya kujibu Hoja za msingi za Sumaye,,anajibu kimajungu tu na umbea..
Eti uchaguzi 2015..
Umbea tu,yani hata kijiweni kwetu sikuhizi (watu ambao wengi wetu hatuna hata elimu ya 4m 4)..
Tusingejibu huu Ujinga aliojibu ndungai..
Sumae anasema hata kama kupandisha posho 70, mpaka 200, ni jambo lisilovumilika..sio kwa sumaye na watanzania wenye haki ya kupiga kura 2015..
Halivumiliki hata kwa watoto wadogo..

Siku nyingine kwa Ndungai na Viongozi wengine Ropo,ropo tafakarini kabla hamjasema hzo pumba zenu kwanu hamna makatibu jamani..!
Kauli zenu zinachefua na laiti kama unaongea na mimi niko karibu,, yangekukuta yaliyo mkuta Mwinyi...

Mkuu umeongea kitu cha maana sana yani hizi kauli zao wakati mwingine zinaweza kukutoa machozi hawana huruma kabisa, mm najiuliza hivi hawaoni maisha yanavyotugonga sisi wananchi tunaolipwa 1500 kwa siku kwenye makampuni ya kichina na wahindi.
Tatizo viongozi wetu wengi hawapendi kuambiwa ukweli wao wamezoea kutudanga kwa makaratasi yaliyojaa takwimu za uongo, wanatakiwa waelewe kuwa watz sio mambumbu tena kama walivyozoea.
Kiongozi kama Ndugai amejionesha utupu wake hivyo nawashauri watu wa jimbo lake kumnyima kura maana huo ubunge ameufanya kama sehemu ya kutengenezea utajiri.
 
Back
Top Bottom