Ndugai amvaa Sumaye, asema hana usafi wa kubeza posho!

Ndungai was no show bunge lilipota. Kumekuwa na mijadala mizito kama ule wa katiba mpya na hatujasikia makelele yake ila hili la posho naona limemtoa pangoni. Now we know what motivates this man! Na kama Ndungai angefuatilia vizuri kauli ya Sumaye atagunduwa kuwa yeye (Sumaye) akiwa Waziri mkuu alikuwa anazongozwa na wabunge (wa ccm?) aridhie nyongeza za posho. Hii ni tabia ya siku nyingi ila sasa elimu ya uraia imeenea na watu wanahoji tabia za wabunge. Huu ni mwanzo tu, Ndungai ajiandae, life will never be the same kwa wabunge... tutahoji everything!
 
Ananikumbusha Dr Che Mponda. Angekuwa ananifundisha ningebadilisha kozi, kila akipanua kinywa kinachotoka ni pumba mtupu. Sijui ndio kujikomba kwenyewe?!

Mkuu mbona jibu unalo tayari,huko ndio kujikomba kwenyewe,matokeo yake hata aliowazidi elimu wanamuona hakuna kitu
 
CHADEMA: Kurugenzi inayohusika na masuala ya Bunge na Kiongozi wa Upinzani Bungeni tunahitaji kauli zenu haraka kujibu UPUUZI huu wa Ndugai.

Hata kama Sumaye au waliotangulia walifanya baadhi ya madudu hai-justify wao (Ndugai na genge lake) kujihalalishia upuuzi.

Kama haya ndio mawazo ya viongozi wa Chombo cha Juu kabisa cha maamuzi katika taifa, chombo cha uwakilishi wa wananchi, chombo cha kutunga sheria, chombo cha kuisimamia na kuiwajibisha Serikali kwa niaba ya wananchi basi taifa limepoteza dira totally na tuko kwenye chaka ambalo kutoka humo inahitajika kazi ya ziada.
 
Ndugai katukumbusha "posho" nyingine inayoitwa pensheni ya viongozi wakuu wastaafu. Sumaye kama WM mstaafu ambaye "hakutuibia" kabisa wakati wote wa utumishi wake uliotukuka. Nadhani pensheni hii ya 80% ya mshahara wa WM aliyeko madarakani ingewekewa vigezo kama vile vya zawadi ya Mo Ibrahim.
 
kweli hatuna viongozi, kumbe jitihada zote za kuongezeana posho lengo ni kuweka historia ya nani alinufaika zaidi kwenye uongozi? CDM nchi iko mikononi mwenu pangeni mikakati ya kuichukua na kuondoa uozo wote kuanzia awmu ya pili hadi hii ya mafisadi
 
CCM bwana raha tupu! kumbe ndio maana mnapenda kupeana vijiti siri mwaijuia duuuuuuh kazi kweli kweli hiyo, ndio maana hata vijana wenye moyo wa kuijenga hii nchi wanashinda kabisa kutokana na mambo mnayoyafanya! Hv sisi watanzania tupoje jamani watu kama hao bado tunawapa madaraka! Ila mwisho wenu utafika kama sio leo basi kesho hayo mnayoyafanya yatawarudia tu
 
anachozungumzia huyu ndugai ni kua, wakati wao wanakula hakuna aliowaingilia sasa na wao wanakula wengine wanapiga kelele!
huyu mgogo asitufanye watz mabwege.hv hakumsikia sumaye aliposema kuwa alimuomba ben asimteue upm coz wabunge watamkataa kwa sababu alipinga posho?
Hayo marupurupu ya ustaafu sh atayapata akistaafu? Au atakataa?
Eti ukiwa mstaafu usikosoe ni sawa na mtoto kukataa kusoma kwa kuwa babaake hakusoma! Kila jambo na wakati wake
 
...hii ndo tabia ya mapanya buku,yakisha kula chakula chote kwenye ghala yanaaza kutafunana mikia...
 
Ndugai hayuko timamu lazima anafile Mirembe sijui kama alimsikiliza Sumaye kwa makini au alisimuliwa?
 
Liangalieni suala la pensheni ya viongozi wakuu wastaafu kwa umakini na upana zaidi kabla ya kumshambulia Ndugai. Tuna mawaziri wakuu wastaafu wengi. Tuna marais wastaafu wawili. Tuna makamu wa rais wastaafu. Tuna wajane wa viongozi wakuu wastaafu kama Mama Maria Nyerre, mke wa marehemu Dr OA Juma, wote hawa wanalipwa hata kama baadhi yao walikuwa wezi wazuri tu enzi zao wakiwa madarakani na wana hisa kwenye biashara kubwakubwa za nchi hii.
 
Sijawahi kuona mtu anatamka Upuuzi Mzito kama huu wa Ndugai halafu bado akaendelea kubaki madarakani. Yaani yeye anaona kwamba kula/kuwaibia Wananchi kwao ni kwa nia ya kuwakomoa Viongozi waliowatangulia! Halafu sisi Wabongo tumebaki tumekenua tu! Huyu jamaa anaweza kunisababishia BAN ya bure humu kifua kilivyonijaa. Naomba Mods siku moja moja mtuachie watu tutoe ya moyoni kwa Mitakataka kama hii ili ijue kwamba hawaongozi Mbuzi bali Watu wenyeakili timamu.
 
Kama jana nilikosea, na leo sipo tena mahali pale lakini natambua (au pengine sitambui) kuwa nilikosea, je sina haki ya kukosoa wengine, as far as na mimi nilifanyakosa hilo? Hivi kama ulizaa nej ya ndoa enzi za ujana wako (whether kwa kukusudia au kwa bahati mbaya) na baadae mwanao huyo huyo nae akaanza tabia zinazoelekea huko ulikotoka wewe, hutazikemea kwasababu eti na wewe ulifanya hivyo? Naona kwa kufanya hivyo tutakua mapunguani wa akili, Sumaye ameliona hilo kama kiongozi mwengine ( yeye pia si msafi) ana wajibu wa kulikemea sana hilo, hayo ya kugombea urais ni ku-divert hoja ya msingi kwa sasa ambayo ni posho za wabunge na ukosefu wa umakini katika serikali.
 
Kama jana nilikosea, na leo sipo tena mahali pale lakini natambua (au pengine sitambui) kuwa nilikosea, je sina haki ya kukosoa wengine, as far as na mimi nilifanyakosa hilo? Hivi kama ulizaa nej ya ndoa enzi za ujana wako (whether kwa kukusudia au kwa bahati mbaya) na baadae mwanao huyo huyo nae akaanza tabia zinazoelekea huko ulikotoka wewe, hutazikemea kwasababu eti na wewe ulifanya hivyo? Naona kwa kufanya hivyo tutakua mapunguani wa akili, Sumaye ameliona hilo kama kiongozi mwengine ( yeye pia si msafi) ana wajibu wa kulikemea sana hilo, hayo ya kugombea urais ni ku-divert hoja ya msingi kwa sasa ambayo ni posho za wabunge na ukosefu wa umakini katika serikali.
Liangalieni suala la pensheni ya viongozi wakuu wastaafu kwa umakini na upana zaidi kabla ya kumshambulia Ndugai. Tuna mawaziri wakuu wastaafu wengi. Tuna marais wastaafu wawili. Tuna makamu wa rais wastaafu. Tuna wajane wa viongozi wakuu wastaafu kama Mama Maria Nyerre, mke wa marehemu Dr OA Juma, wote hawa wanalipwa hata kama baadhi yao walikuwa wezi wazuri tu enzi zao wakiwa madarakani na wana hisa kwenye biashara kubwakubwa za nchi hii.
 
Sijaelewa kama Ndugae anasema wao wamejitengenezea mazingira ya kujinufaisha kwa kutumia nafasi yao Bungeni kwa vile kina Sumaye nao walitumia nafasi hiyo hiyo kujinufaisha? Au amesema nini hasa?
Nafikiri nia ya Ndungai ni kutujulisha kuwa hata Sumaye alitumia bunge kujinufaisha kwa mafao na marupurupu ya baada ya kustaafu nasi wananchi tulifanyie kazi ili kupunguza kiwango kikubwa cha ajabu wanachojilipa baada ya kustaafu wakati wastaafu wengine wanataabika na hata matibabu hawana
 
Liangalieni suala la pensheni ya viongozi wakuu wastaafu kwa umakini na upana zaidi kabla ya kumshambulia Ndugai. Tuna mawaziri wakuu wastaafu wengi. Tuna marais wastaafu wawili. Tuna makamu wa rais wastaafu. Tuna wajane wa viongozi wakuu wastaafu kama Mama Maria Nyerre, mke wa marehemu Dr OA Juma, wote hawa wanalipwa hata kama baadhi yao walikuwa wezi wazuri tu enzi zao wakiwa madarakani na wana hisa kwenye biashara kubwakubwa za nchi hii.
Naunga mkono hoja yako kuna haja kubwa kuangalia mafao ya wastaafu na hata matibabu wanayopata nje ya nchi wakati wao wakiwa madarakani hakujenga na kuboresha hospitali na huduma za matibabu ili wote tufaidike na matibabu hapa nchini
 
Sijaelewa kama Ndugae anasema wao wamejitengenezea mazingira ya kujinufaisha kwa kutumia nafasi yao Bungeni kwa vile kina Sumaye nao walitumia nafasi hiyo hiyo kujinufaisha? Au amesema nini hasa?

MMK jibu la swali lako Ndugai mwenyewe kakujibu cheki hapa: “Mimi nakwambia kitu ambacho nakijua na wakati huo nilikuwa bungeni kama mbunge na Sumaye alikuwa akizipokea hizi posho, Rais (Ali Hassan) Mwinyi aliwahi kusema kila zama na kitabu chake, hebu na yeye (Sumaye) atuache na sisi tuandike kitabu chetu,” alisema Ndugai.
 
Inaelekea Viongozi wetu wako kwenye mashindano jinsi ya kupata pesa na siyo kuwaongoza wananchi .Jamani tuwachambue kwa pumba zao
 
Eti huyu ndiye Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika. Kweli ipo JOB!
 
Back
Top Bottom