Ndugai amvaa Sumaye, asema hana usafi wa kubeza posho! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndugai amvaa Sumaye, asema hana usafi wa kubeza posho!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Maroon4, Jan 5, 2012.

 1. M

  Maroon4 Member

  #1
  Jan 5, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  0
  digg


  Naibu Spika wa Bunge,Job Ndugai

  ASEMA HANA USAFI WA KUBEZA NYONGEZA YA POSHO
  Fredy Azzah
  NAIBU Spika wa Bunge, Job Ndugai amemjia juu Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye kuhusu kauli yake ya posho za wabunge, akisema hakupaswa kuitoa kwani aliwahi kufanikisha kupitishwa sheria ya malipo kwa viongozi wakuu wastaafu ili kujinufaisha akistaafu.Juzi, Sumaye pamoja na mambo mengine, alizungumzia mwelekeo wa taifa kwa sasa na kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015 huku akisema mpango wa ongezeko la posho za wabunge unapaswa kuachwa kwani unaweza kufanya makundi mengine ya utumishi wa umma kudai nyongeza.

  Kauli hiyo ilijibiwa vikali jana na Ndugai ambaye aliwatahadharisha viongozi wastaafu kuwa makini na kauli wanazotoa na kuwataka wale ambao wanataka urais wa 2015 ikiwa ni pamoja na Sumaye waseme sasa badala ya kuwababaisha Watanzania kwa kuzungumza mambo mbalimbali ili wawapende.

  Alisema wakati Sumaye anazungumzia posho za wabunge, sheria ya kuwalipa viongozi wastaafu mafao ilipitishwa wakati akiwa kiongozi wa shughuli za Serikali bungeni na hakuipinga kwa kuwa alikuwa anajiandalia mazingira ya kustaafu.
  “Kwa sasa analipwa asilimia 80 ya mshahara wa waziri mkuu aliyepo madarakani, ni fedha nyingi kuliko hata mshahara wa Naibu Spika (Ndugai kwa sasa), wakati sheria hii inapitishwa alikuwa kiongozi wa shughuli za Serikali bungeni (Waziri Mkuu), alikuwa anajiandalia mazingira ya kustaafu,” alisema Ndugai na kuongeza:

  *“Sitaki kuendelea kusema sana jinsi ambavyo ananufaika, lakini ninachosema viongozi wastaafu duniani kote inatakiwa wawe makini na kauli zao. Wakianza kwenda kwenye vyombo vya habari na kusema maneno haya haipendezi.”
  Alifafanua kwamba badala ya kuzungumzia posho za wabunge pekee ni vyema pia likazungumziwa suala la posho kwa viongozi wote wa umma.

  “Kwa watu wanaotaka kugombea urais mwaka 2015 ni bora waseme sasa. Waache kutubabaisha Watanzania… nasema viongozi wastaafu lazima wawe makini kwa kauli zao, mimi Sumaye ninamheshimu sana na ninatambua haki yake ya kikatiba ya kujieleza,” alisema na kumshauri kuwa makini na kauli zake anapozungumza juu ya Bunge kwa sababu yeye pia alikuwa sehemu ya mhimili huo.

  “Yeye ni kama mchezaji mstaafu wa timu hii (Bunge), inatakiwa awe makini sana hawezi kuizungumzia hii timu kama mshabiki mwingine,” alisema Ndugai.

  Ndugai alisema posho zilikuwepo tangu enzi za Sumaye akiwa mbunge, naibu waziri na hatimaye waziri mkuu na kwamba kama hoja ni kiasi cha fedha... “Aseme ni kiasi gani wabunge wanapaswa kulipwa.”
  Sumaye aliingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 1985 baada ya kushinda ubunge katika Jimbo la Hanang na mwaka 1987, aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo hadi mwaka 1994 alipoteuliwa kuwa waziri kamili katika wizara hiyo.

  “Mimi nakwambia kitu ambacho nakijua na wakati huo nilikuwa bungeni kama mbunge na Sumaye alikuwa akizipokea hizi posho, Rais (Ali Hassan) Mwinyi aliwahi kusema kila zama na kitabu chake, hebu na yeye (Sumaye) atuache na sisi tuandike kitabu chetu,” alisema Ndugai.

  Dk Bana abeza
  Akizungumzia kauli ya Sumaye, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana alisema mambo aliyozungumza si mapya na huku akimtaka kutazama kila neno linalotoka mdomoni mwake.

  Dk Bana alisema kauli ya Sumaye kuhusu matumizi ya taasisi ya urais, inaweza kutafsiriwa kwamba inatokana na yeye kuwa na uchungu wa kuikosa alipogombea na Rais Jakaya Kikwete katika uchaguzi wa ndani wa CCM.

  Sumaye katika kinyang’anyiro cha kupenya kura za maoni kwa ajili ya kupeperusha bendera ya CCM baada ya Mkapa, alishika nafasi ya tano na kushindwa kuingia hata tatu bora ambayo waliingia Rais Kikwete, Dk Salim Ahmed Salim na Profesa Mark Mwandosya.

  “Kwanza anavyozungumzia taasisi ya urais hatujui kama ni hii au ni zilizopita, lakini ikumbukwe kuwa aligombea nafasi hiyo akaikosa kwa hiyo kuna uwezekano kuwa ni roho inamuuma,” alisema Bana.

  Kuhusu suala la rushwa katika uchaguzi alisema: “Suala hili lilikuwepo kwa muda mrefu na limepigiwa sana kelele, yeye hakuweza kumshauri Rais (Benjamin) Mkapa kuwa watunge sheria ya kupambana na hali hii, lakini sasa hivi Serikali imejaribu inatakiwa aipongeze kwa hilo,” alisema Dk Bana.

  Alisema hata baada ya kuundwa kwa sheria hiyo, viongozi wengi wakubwa ikiwa ni pamoja na wale wastaafu hawaonekani kuipigia debe.

  Dk Bana alisema kuundwa kwa sheria ni jambo moja na kinachotakiwa sasa ni utekelezaji wake kufanyiwa kazi.
  Alisema pia ingekuwa jambo jema endapo viongozi wastaafu wangeunda taasisi yao ili waweze kushauri Serikali ili busara zao ziweze kutumika vyema huko... “Yeye ana nafasi kubwa sana ya kuzungumza haya mambo ndani ya chama na pia hata kumshauri Rais moja kwa moja.”

  Kuhusu suala la posho kwa wabunge, alisema Sumaye alilizungumza vizuri na inatakiwa aungwe mkono na watu wengine.

  Alichosema Sumaye
  Akizungumza kupitia kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha ITV, Sumaye alisema ongezeko la posho za wabunge linaweza kuchochea makundi mengine kama wanajeshi, polisi, Mahakama na walimu nao kutaka nyongeza, hivyo kumweka Rais katika wakati mgumu kufanya uamuzi.

  “Mwanasiasa mzuri akifanya jambo akiona limewaudhi wananchi anatakiwa aliache, lakini pia kwenye hili huu mkanganyiko wa Spika na Katibu wake na huu ukimya wa Ikulu ni tatizo, tungependa waseme ili umma ujue hali ikoje?” alisema Sumaye.

  Alisema hatua ya Bunge kujipandishia posho ya kikao kutoka Sh70,000 hadi Sh200,000 kwa siku haliingii akilini na kwamba, inakiuka utaratibu uliowekwa na Serikali katika kulipa gharama kwa maofisa wake ikiwa ni pamoja na gharama hizo za fedha za kujikimu.

  “Siyo kwamba napinga posho, wabunge wanastahili posho, lakini kwa kweli kujiongezea kutoka Sh70,000 hadi Sh200,000 siyo sahihi,” alisema Sumaye.

  Alisema wakati alipoteuliwa na Rais Benjamin Mkapa kwa Awamu ya Pili kushika wadhifa wa Waziri Mkuu, aligoma kwa sababu alikuwa amekwaruzana na wabunge kuhusu nyongeza ya posho.

  “Nilimwambia wabunge watanikataa kwa sababu nimegombana nao sana juu ya suala la posho lakini akasema lazima uwe na mimi ndipo nikakubali, lazima hili suala liangaliwe mara mbilimbili… leo wabunge mmejiongezea kesho jeshi, polisi na walimu nao watataka, tutafanyaje tusifanye mambo ambayo yatamuweka Rais pabaya,” alisema Sumaye.

  Alisema posho ni jambo ambalo kwa sasa limekuwa tatizo kwa serikali na kwamba imefika wakati ofisi za Serikali zimehamia hotelini, lengo likiwa ni watumishi wa umma kutafuta mwanya wa kulipana
   
 2. GodfreyTajiri

  GodfreyTajiri JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 846
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 60
  na bado, watachora mistari mchangani hata mtu
  atoke ngeu kabla ya 2015. dah!
   
 3. S

  SINGOGO Member

  #3
  Jan 5, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hawa ndiyo viongozi wanaotoa majibu mepesi kwa maswali mazito, hivi kama mwenzako alikula kinyesi na wewe waweza kula.
   
 4. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  ukisikia hekaya za abunuasi ndu hizi za ndugai na dr. Bana.

  Ni aibu sana kuona kiongozi anatoa kauli rojorojo namna hii.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Jan 5, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Sijaelewa kama Ndugae anasema wao wamejitengenezea mazingira ya kujinufaisha kwa kutumia nafasi yao Bungeni kwa vile kina Sumaye nao walitumia nafasi hiyo hiyo kujinufaisha? Au amesema nini hasa?
   
 6. M

  Maroon4 Member

  #6
  Jan 5, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Reminds me of George Githongo's book "it's our time to eat"
  Ndugai anasisitiza tu kua huu ni muda wao kula hivyo waachwe kama walivyo kwani hata kina SUMAYE had their time to eat. You can't help but feel sorry for this country for having such Leaders....
   
 7. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  amesema exactly that....
  Wananchi wangetakiwa wapewe uwezo wa kitunga regulation......kiongozi wa serikali akiongea upuuzi mzito namna hii, wakamate watie kiberiti.

  This is a big joke!!!
   
 8. M

  Miranda Member

  #8
  Jan 5, 2012
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ndugai:kila zama na kitabu chake? Sasa napata picha kumbe kila awamu ya bunge inajipandishia posho, ili kuunda kitabu chao...amini amini nawaambia ninyi wabunge, ipo siku yaja mtakapolia na kusaga meno mbele ya haki...mlaaniwe
   
 9. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #9
  Jan 5, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hivi huyu anayejiita dk bana ana akili kweli?au anaropoka ropoka tu....na we ndugai maliza vidonge kwanza ndo uje kuongea ongea bana
   
 10. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #10
  Jan 5, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hapo hamna msafi......msitake kuanza kutetea watu.
  Wote hao lao moja.
   
 11. nimie

  nimie JF-Expert Member

  #11
  Jan 5, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  ILI KUJINUFAISHA: Sasa nazidi kupata picha zaidi ya kile kinachoendelea, kumbe mambo mengine yanayofanyika tunafikiri ni kwa maendeleo ya nchi yetu kumbe lengo ni KUJINUFAISHA kwa siku za usoni hao walioshika mipini!

  ANALIPWA KULIKO NAIBU SPIKA (yaani yeye NDUGAI): Huu ni wivu tu, Ndugai anaona kama Sumayi analipwa bila jasho wakati yeye "anapigika" pale kwenye kile kiti cha kuzunguka, hahaha.

  "ATUACHE TUANDIKE KITABU CHETU": Haya bana (Ndugai) nyie si mnaona hili ni shamba la bibi! Kila aingiaye mawazo yote kuvuna tu, waliopanda (viongozi wa zamani walokuwa waadilifu) mnawaona hamnazo na wanaopalilia (wananchi) mnawaona si kitu. Poa tu kuna wengine (viongozi) bongo zenu zimelala kwa manono mlayo. Niliwahi kuhisi Ndugai si mzalendo, kwa kauli hizi nimejua NILIKUWA SAHIHI KABISA.

  Endeleeni tutawaona 2015, si mbali kama mdhanivyo!
   
 12. Nyamburi

  Nyamburi JF-Expert Member

  #12
  Jan 5, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 306
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hawa viongozi wetu mkuu sasa wanakua kama katuni,eti "kila kitabu na zama zake,tuwaache waandike zama zao" ni kichefuchefu tupu
   
 13. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #13
  Jan 5, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  "between the lines" Ndugai na Bana wanasema:
  Ulipitisha sheria kwa manufaa yako binafsi tuache nasisi kwasababu hii ni zamu YETU (Ndugai)
  Usimwage mpunga kwenye kuku wengi kwani hata wewe unayako ambayo tunaweza kuyasema(Bana)
  Yote aliyosema Sumaye yanahusiana na nia yake ya kutaka uraisi(2005 na 2015) (Bana na Ndugai)
   
 14. e

  ejogo JF-Expert Member

  #14
  Jan 5, 2012
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Reasoning ya Mr. Ndugai kama kiongozi ipo chini sana.
   
 15. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #15
  Jan 5, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ni heri Ndugai angebaki kimya kuliko kujiumbua. Sasa napata mwanga kwamba katika hali kama hii, hata Spika anayofanya nia sawa tu!

  Acha waandike kitabu chao!
   
 16. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #16
  Jan 5, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,512
  Likes Received: 5,628
  Trophy Points: 280
  Tunapenda kujustify mabaya yetu kwakuwa tu hata wengine walifanya!! Tunapenda kuonyesha wote tupo hivyo! Tujifunze kujadili na kutatua hoja iliyopo mbele yetu! hawa siasa tu!
   
 17. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #17
  Jan 5, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kweli hatuna viongozi, kumbe jitihada zote za kuongezeana posho lengo ni kuweka historia ya nani alinufaika zaidi kwenye uongozi? CDM nchi iko mikononi mwenu pangeni mikakati ya kuichukua na kuondoa uozo wote kuanzia awmu ya pili hadi hii ya mafisadi
   
 18. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #18
  Jan 5, 2012
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ndungai analalamika Sumaye hataki wao wale kama yeye alivyokula. Nina wasiwasi kuwa yule mwenyekiti UV CCM Pwani anashauriwa na Ndugai!
   
 19. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #19
  Jan 5, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Ananikumbusha Dr Che Mponda. Angekuwa ananifundisha ningebadilisha kozi, kila akipanua kinywa kinachotoka ni pumba mtupu. Sijui ndio kujikomba kwenyewe?!
   
 20. bona

  bona JF-Expert Member

  #20
  Jan 5, 2012
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  anachozungumzia huyu ndugai ni kua, wakati wao wanakula hakuna aliowaingilia sasa na wao wanakula wengine wanapiga kelele!
   
Loading...