Ndugai acha kuwaona watanzania ni wajinga. Kama Hayati Magufuli alipotoshwa, wewe kama Spika kwanini haukumshauri?

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
4,086
6,568
Tunapoenda tunaelekea pabaya sana. Na hii ni dalili mbaya sana ya kuwepo kwa viongozi wanafiki na wasiofaa katika jamii yetu.

Rais wa JMT ni sehemu ya bunge, bunge la JMT lina mamlaka ya kuisimamia Serikali na kuhoji pale serikali inapofanya ndivyo sivyo, hili lipo wazi kabisa kwa mujibu wa katiba ya JMT ibara ya 63.

Leo hii spika Ndugai anaongea mambo na kuwaona watanzania ni wajinga? Kwamba alienda huko China na kuonana na bodi ya kampuni ya China Merchant, na walitoa presentation nzuri yenye kumuhakikishia kuwa wakipewa kazi ya kujenga mradi wa bandari Bagamoyo, utakuwa na faida kw Tanzania

Kwa kumalizia anasema mkuu wa nchi aliyekuwepo alipotoshwa na ndio maana akaupiga chini mradi wa Bagamoyo. Sasa kama alipotoshawa na wewe na Bunge lako mna mamlaka ya kuhoji, na kuisimamia serikali kwa nini hamkueleza ukweli? Leo unasubiri hayupo baaada ya kufariki ndio unatufanya watoto?

Wewe kama mkuu wa bunge, ulishindwa vipi kujadili na wabunge ili kumuambia mkuu wa nchi aliyekuwepo kuwa anapotoshwa? Na je, kama alikuwa hapotoshwi ila kulikuwa na mashariti yasiyo na tija?
 
Yaani najiuliza hawa watu ni wajinga kiasi gani? Sasa ndo najua kwa nini magufuli alikuwa akifanya kazi hata ambazo alitakiwa kufanya mtendaji wa kata.

Ni kwa sababu alijua anaofanya nao ni wajinga analazimika kufanya kazi mwenyewe.

Yaani wote ni wachumia tumbo hatuna wasomi wazalendo jitu linaangalia tumbo lake.

Hawa hawa ndo alifanya nao kazi kwa ukaribu leo ndo wako mstari wa mbele kumponda.

Kifo ni fumbo kama marehemu angekuwa anarudi kuwa hai duniani jpm tungempa kura za kumwaga akasafishe huu upuuzi unao endelea.

Mm ninachojua msomi anaetambua kazi yake lazima asimamie haki, bora utumbuliwe lakini kwa kusimamia haki

Sasa unajiuliza magufuli alikuwa mbovu mbona walimsifia kwa nguvu zote? Mbona walimshauri kwa nguvu zote? Hawakuwa royal kwake hawa waganga njaa.

Hata mponde vipi kisa ashakufa magufuli ni mwanaume wa shoka asiemuogopa yeyote. Kwa mtu yeyote mwenye akili ambae hatangulizi tumbo mbele anajua kuwa magufuli ni shujaa.

Watanzania wanapenda kudekezwa wafanye wanachotaka wao.bure kabisa

Rip jpm
 
Hapa ndipo tulipofikishwa na CCM. Kila aliyekuwa akijaribu kuhoji jambo lolote lililotoka kwa mtu wa CCM alionekana siyo Mzalendo kwa Nchi yake bali ni Msaliti anaetumiwa na Mabeberu kuihujumu Nchi yake.

Tulipiga kelele sana humu kuhusu utendaji wa Spika Ndugai na baadhi ya Watendaji wengine wa Serikali lkn tuliishia kukejeliwa na kuitwa majina ya kila namna.

Wale wale waliokuwa vinara wa kutupiga vijembe humu ndio hao hao waliogeuka na kuanza kuwashambulia wale waliokuwa wakiwasifia kipindi kile hata pale wanapokiuka kanuni na taratibu za kiutendaji.

Je, ni nani mnafiki kati yao na kina Ndugai?
 
Back
Top Bottom