Ndoto zimewaingiza mkenge watu wengi sana.

streat Anthem

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
395
474
Kichwa cha habari hii kinaweza kukufanya ujiulize ulize lakini hali halisi ndiyo hiyo.

Fikiria umeonana na mtu jinsia ke au me kwa mara ya kwanza. Mtu huyo akaanza kukuangalia sana, kila ukigeuza macho unakuta anakutazama.

Kiukweli kichwani utaanza kujiuliza maswali na kujijibu mwenyewe. Huku hali hiyo inaweza kukunyima amani na we kuanza kujishtukia na kujaribu kujiweka sawa.

Hali hii ikiendelea labda mtu huyo ni mwanafunzi mwenzako, mfanyakazi, jirani au mtu yeyote.
Utajikuta taswira yake inakujia ndotoni, utakuwa unamuota kwa kadri unavyomuwazia.
Sasa watu wengi hujichanganya hapa na kujidanganya kuwa kile wakionacho kwenye ndoto kinaweza kuwa ni kitu au mtu sahihi kwao hasa kwenye mahusiano.

Bahati mbaya sana wale wapendwa( waliookoka) hudhani kama umemuota mtu labda unayemtaka, mhitaji au anayekuangalia angalia basi hapo wanadhani Mungu kajibu Maombi.

Mara nyingi mtu uliyemuota akikutongoza kuchomoa inakua vigumu kwa kuwa watu wengi washadanganyika kwenye dhana ya ndoto.

Kisayansi mtu anaweza kuota mambo aliyoyafanya kwa siku husika hasa yale yaliyojirudia rudia.
Kama mtu kakuangalia angalia sana unaweza kumuota kama ulimtia maanani.

Kiroho pia ndoto zinaweza kuwa na ujumbe. Swali ni je wangapi wanatafsiri ndoto kiusahihi.

Wito. Sio kila ndoto au yule umuonae kwenye ndoto akifanya jambo jema au baya Basi na wewe umuamini au uamini jambo hilo

Ni vyema kujali mambo yako na kuepuka kuangaliana angaliana ili kukwepa mtego wa kutekwa kifkra.
 
Kuna mwaka fulani miaka ya nyuma sana huko tukiwa wadogo niliota tuko na rafiki yangu kisha akapita mama mmoja yule rafiki yangu akaniambia huyu mama nasikia mume wake huwa anamfanya kwa kupitia mdomoni nikasema ptuuu ukatili gani huu. Look at what is happening now...
 
Na wewe je
 
Cha kusikitisha kuhusu mimi ni kwamba nikimuona binti nikampenda nikimuota tu kabla sijamtongoza basi ndio simpati tena. Hata nifanye nini hatakubali. Huwa nawaza sana uhusiano huu sijapata majibu.
 
Itabid utafute mtu mwenye karama akwambie. Kuna sirikubwa sana hapo
Cha kusikitisha kuhusu mimi ni kwamba nikimuona binti nikampenda nikimuota tu kabla sijamtongoza basi ndio simpati tena. Hata nifanye nini hatakubali. Huwa nawaza sana uhusiano huu sijapata majibu.
 
Kuna mwaka fulani miaka ya nyuma sana huko tukiwa wadogo niliota tuko na rafiki yangu kisha akapita mama mmoja yule rafiki yangu akaniambia huyu mama nasikia mume wake huwa anamfanya kwa kupitia mdomoni nikasema ptuuu ukatili gani huu. Look at what is happening now...

Ur gud when t comes to BJ....nice!
 
wewe ndio umekuwa huyo mama...una...mdomoni hehehe nimekuelewa vibaya nadhani
Ni kweli umenielewa vibaya. Kwa wakati huo niliona ni jambo la ajabu sana na sikuwahi kufikiria kuwa mtu anaweza kufanya kitu kama hicho ila sasa hivi ni jambo la kawaida
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom