Ndoto zimekuwa na nafasi muhimu katika maisha ya watu. Njoo nikutafsirie ndoto yako

Mkuu naomba unitafasirie hii ndoto nawewe pia usipuuzie kutafasiri,
Nmeota Leo usku ilkua mida ya sa 10...
Inaonyesha kuwa habari njema itapokelewa kwako. Inaonyesha kwamba mtu yeyote aliye na matatizo ya afya katika familia atarejesha afya yake.

Pia, ndoto hii inaonyesha kwamba utapokea habari za furaha. Ikiwa muotaji yupo kwenye ndoa ni ishara anaweza kuwa na shida na mwenzi wake au kupeana talaka. Muotaji anaweza kurudi nyumbani kwa familia yake kwa sababu ya kupigana na mwenzi wake.

Kuona kwamba mdogo wako amekufa katika ndoto inamaanisha kuwa habari za furaha zitakuja kwa yule anayeota ndoto.

Hasa ikiwa kuna shida ya afya, inaonyesha kwamba tatizo hili litatatuliwa katika siku za usoni. Kwa kuongeza, ikiwa kuna tamaa, inaonyesha kwamba hamu hii itaisha. Huenda hUtaki kuzungumza na wanafamilia kwa muda.
 
Asanteh sana
Inaonyesha kuwa habari njema itapokelewa kwako. Inaonyesha kwamba mtu yeyote aliye na matatizo ya afya katika familia atarejesha afya yake. Pia, ndoto hii inaonyesha kwamba utapokea habari za furaha. Ikiwa muotaji yupo kwenye ndoa ni ishara anaweza kuwa na shida na mwenzi wake au kupeana talaka. Muotaji anaweza kurudi nyumbani kwa familia yake kwa sababu ya kupigana na mwenzi wake. Kuona kwamba mdogo wako amekufa katika ndoto inamaanisha kuwa habari za furaha zitakuja kwa yule anayeota ndoto. Hasa ikiwa kuna shida ya afya, inaonyesha kwamba tatizo hili litatatuliwa katika siku za usoni. Kwa kuongeza, ikiwa kuna tamaa, inaonyesha kwamba hamu hii itaisha. Huenda hUtaki kuzungumza na wanafamilia kwa muda.
Asanteh saa kiongozi
 
2) Pia naota kupata tabu Sana kuoga asubuhi kwa ama kukosa maji au k
ukosa sehemu ya kuoga
Inawakilisha hisia juu yako kuwa hauwezi kurejesha au kurekebisha eneo fulani la maisha yako. Ukosefu wa Maji ya kuoga au kupata maji kwa shida huashiria utu wako, tabia yako na hali yako ya ndani ya ustawi. Unapanga kitu muhimu katika maisha yako. Unaogopa ukweli. Ndoto hii inasema una upendo mwingi wa kuwapa wengine.
 
Mm nimeota kama ifuatavyo
Nimeota niko safarini, usafiri ni zile basi kubwa za mikoani, ila mm nimekaa mbele kabsa karbu na dereva, sijakaa kwenye kiti niko kwenye ile sehemu ya kawaida

Safari ikiwa inaendelea tulikutana na mlima mkali mno, yaan sana, ule mlima sijawahi kuuoni, dereva alipambana sana tukawa tunavuka taratibu hatimaye tukafaulu kuupanda ule mlima na kushuka

Baada ya kushuka tulikuta kuna mvua imenyesha kwahyo full matope, tukaanza kuyavagaa yale matope na gari letu, ghafla nikaamka.

Kumbuka gari ilikuwa na abiria wengi tuh,
Na barabara ilikuwa ni ya vumbi.

Maeleze yeyote kuhusu hiyo ndoto
 
Naomba ufafanuzi wa hii ndoto.

Nmeota watu wanataka kuniua ila kila wakinikamata jaribio lao linashindikana.
Wanaendelea kunikimbiza nikapata msaada kwa wazungu wakunificha sehemu kumbe hao wazungu ni wasaliti.

Wakawaita hao watu waliokuwa wananitafuta wakawaonesha mahali nilipo.
Hapo nikawa sina ujanja nikafumba macho nijiandae na kuuliwa ila ikatokea upenyo nikakurupuka nikakimbia.

Nikaenda kujificha kwenye nyumba moja ndani ya hio nyumba nilimkuta mdogo angu na Mama.

Nikawaambia kuna watu wanataka kutuua mara wauaji wakatokea nikawaficha mdogo wangu na Mama.

Ila cha ajabu wauaji wananikimbiza tu mimi na mapanga na visu tupo humo ndani ya nyumba tunapurukushana tu.

Mama na mdogo wangu wakapanda juu ya dali mimi naendelea kupambana tu.

Chakushangaza naanza kuona sura za wauaji ote nawajua ni ndugu zangu Kaka zangu na wadogo zangu upande wa Baba.
Yaani watoto wa Shangazi zangu.

Mwisho majaribio ya kuniua yanazidi wanaendelea kunikimbiza na mapanga na visu.
Ilifika hatua nikachoka nikaamua kupambana nao nikafanikiwa kuwaua ote mwili ulijaa damu sana.
Ghafla nikashtuka kutoka usingizini huku naweweseka sana.
Naomba msaada wa kutafsiri hii ndoto.
Inaonyesha kafara (kuacha kitu kinachothaminiwa kwa ajili ya mambo mengine) ambazo umetoa na shida ambazo umevumilia. Maisha yako ni kama mchezo wa kuigiza. Unahitaji utaratibu na utulivu. Ndoto hiyo inaashiria hitaji la kuhifadhi. Unahitaji kujifunza kuomba msaada unapohitaji. Ndugu kutaka kukuua inaashiria juu ya matamanio yako ya kurudi kwenye mizizi yako. Unaweza kuwa unatilia shaka imani yako ya kiroho. Unahisi hisia zako za maadili na sifa zinahujumiwa. Ndoto hii inaonyesha hisia hivyo unahitaji kuendelea na kazi nzuri. Ndoto yako ni ishara ya nidhamu binafsi. Unatathmini upya maadili yako mwenyewe na kutilia shaka utambulisho wako.
 
Mkuu..

Mimi huwa sizingatii ndoto..lakini hii ya usiku wa kuamkia Leo imenifikirisha..

Nimeota nimepanda baskeli inayoendeshwa na mpenzi wangu ambaye Ni mlemavu.( Mpenzi huyo Ni wa hapo ndotoni ) ..tupo nje tunaizunguka ngome kongwe znz.. ,katika kuzunguka chochoro tukakutana na mtu kabeba maiti anapita nikamuangalia Sana nikampisha njia.. .kusogea kidogo akapita Tena mtu mwengine amebeba maiti kwenye rikwama anasukuma.. hiyo maiti ilikuwa kama mtu ninayemfahamu nikamsogelea nimuone vizuri...nikashangaa,maiti mbili tunapishana nazo hapo kwa hapo..na nikashuka kwenye mile kibaskeli Cha walemavu nilichokuwa nimepanda Nika simama pembeni!
Hii Ina tafsiri gani mkuu?!

Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
 
Usipuuzie ndoto, tafsiri ya ndoto huleta maarifa ya kina kunako ujumbe husika. Ndoto ni jambo la kushangaza ambalo hufanyika na kutokea majira ya usiku na huwa ina maana ya ndani zaidi nyuma ya uzoefu huu wa ulimwengu wa kawaida. Ndoto ni hifadhi ya ujuzi na uzoefu, lakini mara nyingi hupuuzwa kama chombo cha kuchunguza ukweli.

Ndoto ni tukio la kawaida kwetu sote. Ndoto haina mipaka huwatokea watu wote ikiwemo vijana na wazee, matajiri na maskini, rangi, dini na mataifa n.k.

Weka ndoto yako kwa Comment nikufasirie
ndoto zinazohusiana na shule msingi/sekondari na chuo au kuota unafanya mtihani huwa zina maana gani? Hapo ina maana kuwa shule zote umeshahitimu hausomi tena
 
Mimi naota mambo yanatotokea mbele hasa hasa hatari zinazokuja mbeleni

Nilivyokuwa mdg nilikuwa naota na pambana na wanyama hasa nyoka na fisi anaingia ndani ya nyumba kupitia kwenye pembe ya nyumba then anakuja kitandani basi tunaanza kupambana mpk anakimbia

Achana na wachawi ambao karibia wote wa mtaani niliwaota nakweli ni wachawi.

Sasa nilivyokuja kugundua nina uwezo wa kuota matukio ya mbeleni.

Ndoto 1:niliota mahali napolaza pikipiki inaweza kuibiwa kuna ki mlango kdg ambacho inapita kila siku nikilala wazo linanijia,pikipiki unapoiweka itaibiwa na puuza basi siku moja ikaibiwa kweli

2. Nikiwa mkoa mwingine nikaota machine ya amec kwa nje inaibiwa nikaamka nikafungua dirisha ipo. Kesho yake nikaota tena inaibiwa ndotoni naiona inapelekwa getini,nikastuka nikaicheki ipo nikamwambia wife nimeota inaibiwa akasema uoga wako.Keshokutwa ikaibiwa

3.Nikaota gari yangu inaibiwa yaani ndotoni imetolewa kila kitu ipo juu ya mawe.Mara ya pili nikaota imeibiwa mataili tu.Mara ya 3 nikaota nimetoka kununua kitu flani hivi natoka na wife tuelekee kwenye gari nakuta haipo .Hapo nikasema sikubali ikabidi nipigie simu kwa jamaa yangu anipelekee kuleeee

Sasa tukaenda kuleeee siku nayorudi kesho yake nikasafiri likizo cha ajabu narudi tu likizo,mpangaji mwenzangu ambaye nae ana gari akaniambia yaani ulivyosafiri tu,kesho yake alarm ya gari ililia vby mno nikaamka kuchungulia dirishani nikakuta wezi 6 wapo busy kufungua mlango wa gari yangu basi nikakumbuka na ndoto zangu zile nikasema kweli Ndoto zipo na zina maana.

4.Niliota mfanyakazi mwenzangu anani fitini na kwenye ndoto mimi nina ushahidi wote wa fitina zake sasa nimemuita boss nikampa ushahidi akaumbuka nikawa nimeshinda hapo ndotoni na kila mtu naemuota ni halisi kabisa na nawafahamu.Kweli km week nikapata msala na cha ajabu boss yule yule akaniuliza km nina chakujitetea na nikawa na ushahidi usio nashaka na boss akamaliza kwa kusema kuwa makini na flani maana anakufitini

Ulimwengu wa ndoto upo sanaa na mandoto nilianza kuyaota toka nipo darasa 3 sema mama alikuwa ananipiga.Nikisema nimeota mama flani kaja uchi nyumbani kwetu usiku napigwa ila nilivyokuwa ndo vitu vikaanza ku make sense.
 
Sijui ni ndoto au nini nashtukaga usiku Kwa kusikia Jina langu Kama kuna mtu kaniita nje.
Sijawahi kuitika wala kutoka kitandani nashtukaga tu kitandani na kusikilizia nagundua hakuna mtu.
Inakuwa ni nini kiongozi au mawenge tu
 
Naomba unisaidie kutafasiri hii ndoto

Mimi nafanya biashara kwenye duka, Sasa nimeota duka langu nilikuwa nimefunga kwa mda mrefu ila kodi nimelipia kwa huo mda, Sasa nakuja kuambiwa ile frame yangu kuna mtu amekuja kulipia akae yeye pale.


Baadae nikawambia hapa sitoki kwasababu nimelipia, ndipo akaondoka yule mtu, hii ndoto ina maana gani?
 
Ndoto kuhusu Mapigano na jirani hudokeza wingi, utajiri, uzazi, ukuaji na furaha. Unahitaji kufanya uwepo wako ujulikane na sauti yako isikike. Unajificha sana kwa ubinafsi wako.

Pia ni ishara ya heshima, sherehe, mwendelezo au ukamilifu. Unapata faida. Uko tayari kwa sherehe. Ndoto hii ni ujumbe wa nguvu na udhibiti. Unahisi kuwa unaulizwa katika eneo fulani la maisha yako.
Ndoto ni marudio ya mambo uliyowahi kutenda, kuwaza, kuona, kusikia au kuhisi.

Huo utafasiriaji wa ndoto ni janja janja tu, utapeli utapeli tu, uwongo uwongo mwingi kwa lengo la kuchanganya na kupotosha watu.
 
Naomba ufafanuzi wa hii ndoto.

Nmeota watu wanataka kuniua ila kila wakinikamata jaribio lao linashindikana.
Wanaendelea kunikimbiza nikapata msaada kwa wazungu wakunificha sehemu kumbe hao wazungu ni wasaliti.

Wakawaita hao watu waliokuwa wananitafuta wakawaonesha mahali nilipo.
Hapo nikawa sina ujanja nikafumba macho nijiandae na kuuliwa ila ikatokea upenyo nikakurupuka nikakimbia.

Nikaenda kujificha kwenye nyumba moja ndani ya hio nyumba nilimkuta mdogo angu na Mama.

Nikawaambia kuna watu wanataka kutuua mara wauaji wakatokea nikawaficha mdogo wangu na Mama.

Ila cha ajabu wauaji wananikimbiza tu mimi na mapanga na visu tupo humo ndani ya nyumba tunapurukushana tu.

Mama na mdogo wangu wakapanda juu ya dali mimi naendelea kupambana tu.

Chakushangaza naanza kuona sura za wauaji ote nawajua ni ndugu zangu Kaka zangu na wadogo zangu upande wa Baba.
Yaani watoto wa Shangazi zangu.

Mwisho majaribio ya kuniua yanazidi wanaendelea kunikimbiza na mapanga na visu.
Ilifika hatua nikachoka nikaamua kupambana nao nikafanikiwa kuwaua ote mwili ulijaa damu sana.
Ghafla nikashtuka kutoka usingizini huku naweweseka sana.
Naomba msaada wa kutafsiri hii ndoto.
hiii ni.move babuu amke usje kojoa kitandan
 
Wakuu nisaidien mm nna tatzo hili nikiota ndoto kuna baadhi ya vitu hutokea au nikiota nimeongea na mtu bas mtu huyo sku ya pili huongea nae hata kama kwa kunitext wakuu hii inaitwaje??
 
Back
Top Bottom