Ndoto zimekuwa na nafasi muhimu katika maisha ya watu. Njoo nikutafsirie ndoto yako

Ibun Sirin

Member
May 20, 2022
38
74
Usipuuzie ndoto, tafsiri ya ndoto huleta maarifa ya kina kunako ujumbe husika. Ndoto ni jambo la kushangaza ambalo hufanyika na kutokea majira ya usiku na huwa ina maana ya ndani zaidi nyuma ya uzoefu huu wa ulimwengu wa kawaida. Ndoto ni hifadhi ya ujuzi na uzoefu, lakini mara nyingi hupuuzwa kama chombo cha kuchunguza ukweli.

Ndoto ni tukio la kawaida kwetu sote. Ndoto haina mipaka huwatokea watu wote ikiwemo vijana na wazee, matajiri na maskini, rangi, dini na mataifa n.k.

Weka ndoto yako kwa Comment nikufasirie
 

RAYMANU254

JF-Expert Member
Jan 20, 2022
3,279
5,758
Ibun Sirin
Usipuuzie ndoto, tafsiri ya ndoto huleta maarifa ya kina kunako ujumbe husika. Ndoto ni jambo la kushangaza ambalo hufanyika na kutokea
Kuu mi Kuna demu niliachanaga naye muda mrefu na nikamove on vizuri bt huwa namuota Sana ndoto Mara nyingi tuko tunafanya romance, sometimes ananicheat saa zingine tunazinguana.

Yaani hizi ndoto huwa zinanijia Mara kwa Mara kwahyo sielewi Zina maana gani.Nachukia Sana Yaani.
Naomba unifungulie codes za hii ndoto tafadhali.
 

stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
14,577
19,558
Nimeota naendesha gari,ghafla naangalia kwenye dashboard taa zote zimezima na niko kwenye mteremko,nikikanyaga breki hazishiki,nikanyoosha na bahati nzuri eneo lilikuwa limenyooka kwahiyo nilienda mpaka gari likasimama mahali penye ka muinuko kidogo..
 

Ibun Sirin

Member
May 20, 2022
38
74
Ndoto mpya iyandike yenyewe kama Comment, usireplay wala ku Quote kama ni ndoto mpya andika kwa Comment
 

Gladiator4440

JF-Expert Member
Apr 12, 2018
2,285
3,758
Leo nimeota hivi:

Nikiwa nyumbani usiku (katika moja ya nyumba ambayo tulishahama zamani kidogo,zilikuwa nyumba za waalimu tatu tukiwa majirani,Kwa kifupi nimerudishwa nyuma enzi hizo wakati wazazi ni waalimu na mimi nilikuwa mdogo nikiwa darasa la tano hivi).

Nikatoka usiku nikanyata taratibu mpaka nyumba ya Mwalimu mmoja jirani yetu (Namkumbuka vizuri huyu mwalimu ni mama mmoja anaishi na familia yake na watoto 5) Basi nikafika nikaenda moja kwa moja mpaka kwenye corner moja chini ya begi nikaiba counterbook moja ambalo lilikuwa na thamani mno.

Cha ajabu nilikuta taa inawaka na mtoto mmoja alikuwa macho (Namkumbuka vizuri,Alikuwa rafiki yetu sana) Lakini hakusema lolote ndiyo kwanza akawa anajificha nisimwone! Mara mlango ukafunguliwa akaingia mama mwenye nyumba na nikamsalimia tu akaitika vizuri nikatoka nje upesi (Alijua itakuwa nilikuwa nacheza na mtoto wake ndiyo maana nimechelewa kurudi nyumbani).

Cha ajabu nilikuwa na confidence kwamba hilo counter ninastahili kuwa nalo kwamba ni la kwangu lazima nilichukue! Kufika nyumbani namkuta mama yuko macho,Akaniona na counter.Cha ajabu wala hakukasirika akacheka akasema umetoka kulichukua ee... Haya bhana.
 

Babu Ochu

JF-Expert Member
May 30, 2021
845
1,457
Ndoto hizi mbili huwa zinanijia mara kwa mara miaka mingi Sasa

1) Huwa napita njia ninayo ijua vizuri Sana lakini mwisho naishia kutokea nisipopajua na kupotea

2) Pia naota kupata tabu Sana kuoga asubuhi kwa ama kukosa maji au k
ukosa sehemu ya kuoga
Hizi huwa zinajirudia mara kwa mara ila kwa location tofauti tofauti
 

Ibun Sirin

Member
May 20, 2022
38
74
Ndoto ya kupigana na jirani
Ndoto kuhusu Mapigano na jirani hudokeza wingi, utajiri, uzazi, ukuaji na furaha. Unahitaji kufanya uwepo wako ujulikane na sauti yako isikike. Unajificha sana kwa ubinafsi wako.

Pia ni ishara ya heshima, sherehe, mwendelezo au ukamilifu. Unapata faida. Uko tayari kwa sherehe. Ndoto hii ni ujumbe wa nguvu na udhibiti. Unahisi kuwa unaulizwa katika eneo fulani la maisha yako.
 

Ibun Sirin

Member
May 20, 2022
38
74
Nimeota naendesha gari,ghafla naangalia kwenye dashboard taa zote zimezima na niko kwenye mteremko,nikikanyaga breki hazishiki,nikanyoosha na bahati nzuri eneo lilikuwa limenyooka kwahiyo nilienda mpaka gari likasimama mahali penye ka muinuko kidogo..
Breki ni kifaa cha usalama ambacho hutumia msuguano kusimamisha au kupunguza kasi ya chombo kinachotembea, ndoto ambayo breki zinashindwa kufanya kazi inamaanisha kuwa unajali nje ya udhibiti (bila mpangilio) katika eneo fulani la maisha yako.

Ina maana kwamba unajiingiza katika tabia za kujiharibu ambazo zimekufanya uchakachue ili kujaribu kurejesha udhibiti ambao umepoteza. Unaweza kuwa unajiingiza katika tabia hatarishi au unaweza kuingiwa na woga na hali ya kutokuwa na nguvu kiasi kwamba huna tena uwezo wa kutenda.

Kwa hali yoyote, uwezo wako wa kufanya kazi unaathiriwa na chaguo lako, hisia au hali zisizotarajiwa. Huenda umeingizwa katika uchumba wa mapenzi, umenaswa katika mitego ya uraibu wenye nguvu au kujikuta katikati ya kashfa mbaya.
 

Mr kenice

JF-Expert Member
Mar 15, 2022
1,469
1,974
Mkuu naomba unitafasirie hii ndoto nawewe pia usipuuzie kutafasiri,

Nmeota Leo usku ilkua mida ya sa 10,

Iko hv nachokumbuka kwenye ndoto yangua ni misiba ambapo rafki yangu nilio soma nae secondary alifariki kwa ugonjwa gafla bas kesh yake ikafka akazikwa ile sija Kaa sawa nkaskia mdo Wang kabsa kafarki kwa ajali ya pikipiki walikua wakishndana, bas nae pia kesho yake tukazka , bas mm binafsi nilikua nikilia sana hasa matukio yalivoo ongozana kifupi mpka sasa naumia japo ilikua ni mdoto TU,

bas nkawa nmestuka akili akaniambia ni ndoto TU lala, nlichofanya nkamuomba mungu ndoto isitokee kweli nkalala ndo asbh hii nmeingia JF mara paap naona Bingwa wa kuztafsr bas nikama imepengwa vile na itakua ni kwa ajil yangu

Naomba msaada wako chifu.
 

Mbulukenge

Senior Member
Jun 26, 2019
125
288
Naomba ufafanuzi wa hii ndoto.

Nmeota watu wanataka kuniua ila kila wakinikamata jaribio lao linashindikana.
Wanaendelea kunikimbiza nikapata msaada kwa wazungu wakunificha sehemu kumbe hao wazungu ni wasaliti.

Wakawaita hao watu waliokuwa wananitafuta wakawaonesha mahali nilipo.
Hapo nikawa sina ujanja nikafumba macho nijiandae na kuuliwa ila ikatokea upenyo nikakurupuka nikakimbia.

Nikaenda kujificha kwenye nyumba moja ndani ya hio nyumba nilimkuta mdogo angu na Mama.

Nikawaambia kuna watu wanataka kutuua mara wauaji wakatokea nikawaficha mdogo wangu na Mama.

Ila cha ajabu wauaji wananikimbiza tu mimi na mapanga na visu tupo humo ndani ya nyumba tunapurukushana tu.

Mama na mdogo wangu wakapanda juu ya dali mimi naendelea kupambana tu.

Chakushangaza naanza kuona sura za wauaji ote nawajua ni ndugu zangu Kaka zangu na wadogo zangu upande wa Baba.
Yaani watoto wa Shangazi zangu.

Mwisho majaribio ya kuniua yanazidi wanaendelea kunikimbiza na mapanga na visu.
Ilifika hatua nikachoka nikaamua kupambana nao nikafanikiwa kuwaua ote mwili ulijaa damu sana.
Ghafla nikashtuka kutoka usingizini huku naweweseka sana.
Naomba msaada wa kutafsiri hii ndoto.
 

Mr kenice

JF-Expert Member
Mar 15, 2022
1,469
1,974
Mkuu naomba unitafasirie hii ndoto nawewe pia usipuuzie kutafasiri,
Nmeota Leo usku ilkua mida ya sa 10,
Iko hv nachokumbuka kwenye ndoto yangua ni misiba ambapo rafki yangu nilio soma nae secondary alifariki kwa ugonjwa gafla bas kesh yake ikafka akazikwa ile sija Kaa sawa nkaskia mdo Wang kabsa kafarki kwa ajali ya pikipiki walikua wakishndana, bas nae pia kesho yake tukazka , bas mm binafsi nilikua nikilia sana hasa matukio yalivoo ongozana kifupi mpka sasa naumia japo ilikua ni mdoto TU, bas nkawa nmestuka akili akaniambia ni ndoto TU lala, nlichofanya nkamuomba mungu ndoto isitokee kweli nkalala ndo asbh hii nmeingia JF mara paap naona Bingwa wa kuztafsr bas nikama imepengwa vile na itakua ni kwa ajil yangu
Naomba msaada wako chifu.
 

Ibun Sirin

Member
May 20, 2022
38
74
1) Huwa napita njia ninayo ijua vizuri Sana lakini mwisho naishia kutokea nisipopajua na kupotea
Ndoto hii kawaida ni onyo juu ya tukio fulani la siku zijazo ambalo hutofautiana sana, kulingana na jinsi ndoto hiyo ilivyotokea. Unapoona njia ambayo hujui, ndoto hii inaonyesha kwamba huna tumaini, na hujui wapi utaanzia. Ndoto hii pia ina maana kwamba lazima uwe na jukumu la kufungua fursa mpya kwa wengine.

Ina maana kwamba unachofanya lazima kiwe na manufaa kwa wengine. Ingawa hili sio lengo lako kuu, kile unachowafanyia wengine, kitarudi kwako kila wakati kama karma nzuri.
 

HiDEmYiD

JF-Expert Member
Mar 14, 2018
1,843
3,384
Aisee bora kuna ndoto hii mara nyingi naiota ni hivi huwa naota napaaa hata leo nimeota sijui ina maana gani nakuwa napaaa kama ndege angani.
 

Nature

JF-Expert Member
Nov 5, 2014
558
1,420
Usipuuzie ndoto, tafsiri ya ndoto huleta maarifa ya kina kunako ujumbe husika. Ndoto ni jambo la kushangaza ambalo hufanyika na kutokea majira ya usiku...
Maarifa na Hekima ya kutafsiri ndoto umepata wapi mkuu?

Hebu tufundishe kidogo naamini ndyo itasaidia wengi

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 

Ibun Sirin

Member
May 20, 2022
38
74
Leo nimeota hivi:

Nikiwa nyumbani usiku (katika moja ya nyumba ambayo tulishahama zamani kidogo,zilikuwa nyumba za waalimu tatu tukiwa majirani,Kwa kifupi nimerudishwa nyuma...
Inamaanisha kuwa unakaribia kujifunza jambo jipya kuhusu somo linalokuvutia, inaweza kuwa kitu ambacho umekuwa ukifikiria. Inaweza kuwakilisha upotevu wa sasa au wa siku zijazo wa heshima, kustahi kupongezwa kwa wale wanaokujua.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom