X_INTELLIGENCE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 9,647
- 12,215
Ndugu zangu, kijana wenu mpambanaji nimepambana sana nikiwa hapa nyumbani, nimehangaika sana, nimetafuta kazi ya ndoto zangu bila mafanikio. hapo mwanzo kipindi nakua ndoto zangu haswa zilikuwa kujiunga na jeshi la Polisi lakini bahati sio yanu kabisa ndoto hiyo nimeisubiri sana kwa takribani miaka 15 sasa ila sioni dalili ya kufanikiwa kupata hiyo nafasi. nakumbuka nimewahi hadi kuweka thread humu yenye jina OFA YA KIWANJA KWA ATAKAENISAIDIA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI
nimekaa niwaza sana kwa sasa nina kazi nimejishikiza kwenye sekta ya Ulinzi wa makampuni binafsi GARDAWORLD ajira hii inanipa mawazo makubwa sana kila kukicha, tunaibiwa mishahala, muda wa kazi ni mwingi, matumaini ya kupanda daraja/cheo hakuna kwa sababu kampuni zetu hizi mambo ya kujuana yametamalaki kwakweli, haswa usipokuwa kabila moja na viongozi. kwa kifupi nchi yetu haina mfumo mzuri wa ajira hivyo kitu kama cheo imekuwa kama zawadi hivi. unaweza ukafanya kazi hata miaka 10 lakini kijana atakae jiunga kazi hiyo hiyo leo ukalingana nae mshahala na pengine akapandishwa na cheo wewe ukabaki palepale. {kampuni zote za Ulinzi Tanzania ni wanyonyaji wa maslahi ya wafanyakazi} na sekta binafsi alimia 95 zilizopo Tanzania ni wanyonyaji wakubwa wa haki za wafanyakazi yani ukishakuwa mfanyakazi wa sekta binafsi ni kama unakuwa huna haki kabisa unaonekana kama MTUMWA tu.
nimeishi kwa mawazo sana, hivyo nimeona pengine hii nchi mimi sio yangu, wapo wenye nayo niwaache waendelee kuifaidi. nimeomba nafasi za kazi zaidi 1000 ambazo ninakidhi vigezo lakini sikuwahi kuitwa hata kwenye interview. ajira ambazo huwa ninajiona ninabahati ya kuitwa interview haswa za serikalini huwa mara zote naangukia pua vibaya, pesa yangu nyingi sana nimeitumia kusafiria mikoa mbali mbali kuhudhuria interview ambazo mwisho wa siku siambulii chochote. nimehudhunika sana kwakweli.
lengo langu hivi sasa ni kuihama kabisa Tanzania, nimepanga niende nchi zenye fursa ya ajira haswa nchi za Uarabuni, kisha Marekani.
katika safari yangu hii ya kutafuta maisha nitaanzia kwanza nchi za kiarabu ambako nitafanya kazi usiku na mchana nimahifadhi pesa, nikisha imalika kiuchumi nitatengeneza safiri za nchi za Ulaya, nikifanikiwa kuikanyaga ardhi ya Ulaya haki nawaambia nitaitupa passport yenu ya kitanzania, nitaishi Ulaya hadi mwisho wa maisha yangu. mkipenda mtakuja kuichukua maiti yangu muizike huku...ila mimi kurudi Bongo haki vile itakuwa bahati mbaya sana kwangu.

post zangu za nyuma
MSAADA MWENYE CONNECTION NCHI ZA KIARABU
NATAFUTA KAZI ZA KUENDESHA MALORI AU MAGARI YA MAFUTA
naombeni Ushauri na mawazo yenu ndugu zangu.