Ndoto zangu siyo za kuishi Tanzania

Prince Mhando

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
7,401
7,458
Ndugu zangu, kijana wenu mpambanaji nimepambana sana nikiwa hapa nyumbani, nimehangaika sana, nimetafuta kazi ya ndoto zangu bila mafanikio. hapo mwanzo kipindi nakua ndoto zangu haswa zilikuwa kujiunga na jeshi la Polisi lakini bahati sio yanu kabisa ndoto hiyo nimeisubiri sana kwa takribani miaka 15 sasa ila sioni dalili ya kufanikiwa kupata hiyo nafasi. nakumbuka nimewahi hadi kuweka thread humu yenye jina OFA YA KIWANJA KWA ATAKAENISAIDIA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI

nimekaa niwaza sana kwa sasa nina kazi nimejishikiza kwenye sekta ya Ulinzi wa makampuni binafsi GARDAWORLD ajira hii inanipa mawazo makubwa sana kila kukicha, tunaibiwa mishahala, muda wa kazi ni mwingi, matumaini ya kupanda daraja/cheo hakuna kwa sababu kampuni zetu hizi mambo ya kujuana yametamalaki kwakweli, haswa usipokuwa kabila moja na viongozi. kwa kifupi nchi yetu haina mfumo mzuri wa ajira hivyo kitu kama cheo imekuwa kama zawadi hivi. unaweza ukafanya kazi hata miaka 10 lakini kijana atakae jiunga kazi hiyo hiyo leo ukalingana nae mshahala na pengine akapandishwa na cheo wewe ukabaki palepale. {kampuni zote za Ulinzi Tanzania ni wanyonyaji wa maslahi ya wafanyakazi} na sekta binafsi alimia 95 zilizopo Tanzania ni wanyonyaji wakubwa wa haki za wafanyakazi yani ukishakuwa mfanyakazi wa sekta binafsi ni kama unakuwa huna haki kabisa unaonekana kama MTUMWA tu.

nimeishi kwa mawazo sana, hivyo nimeona pengine hii nchi mimi sio yangu, wapo wenye nayo niwaache waendelee kuifaidi. nimeomba nafasi za kazi zaidi 1000 ambazo ninakidhi vigezo lakini sikuwahi kuitwa hata kwenye interview. ajira ambazo huwa ninajiona ninabahati ya kuitwa interview haswa za serikalini huwa mara zote naangukia pua vibaya, pesa yangu nyingi sana nimeitumia kusafiria mikoa mbali mbali kuhudhuria interview ambazo mwisho wa siku siambulii chochote. nimehudhunika sana kwakweli.
382-381.jpg

lengo langu hivi sasa ni kuihama kabisa Tanzania, nimepanga niende nchi zenye fursa ya ajira haswa nchi za Uarabuni, kisha Marekani.

katika safari yangu hii ya kutafuta maisha nitaanzia kwanza nchi za kiarabu ambako nitafanya kazi usiku na mchana nimahifadhi pesa, nikisha imalika kiuchumi nitatengeneza safiri za nchi za Ulaya, nikifanikiwa kuikanyaga ardhi ya Ulaya haki nawaambia nitaitupa passport yenu ya kitanzania, nitaishi Ulaya hadi mwisho wa maisha yangu. mkipenda mtakuja kuichukua maiti yangu muizike huku...ila mimi kurudi Bongo haki vile itakuwa bahati mbaya sana kwangu.

1656513405054.png


post zangu za nyuma
 

mpwayungu village

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
5,964
8,926
Shida hujiamini na qualification ulizonazo wewe unaamini katika connection tu mara utoe kiwanja mara hivi. Skia dogo Kuna watu humu wanatafuta laborers ila wakiona wewe upo kikoneksheni wanaku~dump, anyway mwombe mungu utatoboa
 

Prince Mhando

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
7,401
7,458
Shida hujiamini na qualification ulizonazo wewe unaamini katika connection tu mara utoe kiwanja mara hivi. Skia dogo Kuna watu humu wanatafuta laborers ila wakiona wewe upo kikoneksheni wanaku~dump, anyway mwombe mungu utatoboa
NASHUKURU....
 

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
9,681
11,366
Pole sana kwa hilo! Nilifikiri unatafuta kazi zisizopatikana nchini ndio maana unataka kwenda nje. Kwa aina ya kazi zako unaweza kuzipata hapa nchini, usife moyo endelea kutafuta utapata. Fanya connection na watu pia omba sana Mungu kazi unayotaka atakupatia kwa uwezo wake.
 

Kv-london

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
2,604
3,837
Mdogo wangu anza kusave pesa kwanza kwa ajili ya passport
200000
Flight fare 570$
Visa 600000 hapo kariakoo
Self support dollar 800
Ukishazichanga hizo ndio uamue uende uarabuni au ubaki bongo ufungue business
 

BUKOBA LAND

JF-Expert Member
Dec 26, 2017
7,306
14,548
Take risk or rose change that is my rule number 01 most of peoples we go through tough moment but we know nothing last ....In God we trust.
 

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
23,124
23,144
Bongo changamoto nyingi sana.
Ila nenda EU, Canada, Australia au US.
Kwingine itakuwa kupoteza muda tu na hutafikia malengo yako.
 

Prince Mhando

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
7,401
7,458
Pole sana kwa hilo! Nilifikiri unatafuta kazi zisizopatikana nchini ndio maana unataka kwenda nje. Kwa aina ya kazi zako unaweza kuzipata hapa nchini, usife moyo endelea kutafuta utapata. Fanya connection na watu pia omba sana Mungu kazi unayotaka atakupatia kwa uwezo wake.
Nashukuru sana Nitaufanyia kazi ushauri wako
 

LOLA70

JF-Expert Member
Dec 18, 2020
431
492
Canada wanachukua watu , nenda kwenye official website yao, fuata maelekezo. Holland wanachukua watu, kwa season uk wanachkua watu pia, fuatilia
 

Prince Mhando

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
7,401
7,458
Mdogo wangu anza kusave pesa kwanza kwa ajili ya passport
200000
Flight fare 570$
Visa 600000 hapo kariakoo
Self support dollar 800
Ukishazichanga hizo ndio uamue uende uarabuni au ubaki bongo ufungue business
passport ipo mbioni....ndugu yangu mshahala...hauwe image nalipwa 300,000/= lakini hiyo pesa inanisababishia madeni inaisha kabla sijaipata...nina mke nina mtoto anasoma. mama na baba yangu wananitegemea...kwa pesa hiyo hiyo...kichwa kinauma hadi naisi kuchanganyikiwa....
 

Prince Mhando

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
7,401
7,458
Canada wanachukua watu , nenda kwenye official website yao, fuata maelekezo. Holland wanachukua watu, kwa season uk wanachkua watu pia, fuatilia
nashukuru nitaufanyia kazi ushauri wako...ungenisaidia tovuti yao ingekuwa poua sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

9 Reactions
Reply
Top Bottom