Vugu-Vugu
JF-Expert Member
- Feb 24, 2017
- 1,344
- 1,531
IKO WAPI TANZANIA YA VIWANDA?:
Ni takribani mwaka mmoja na nusu sasa umepita laki bado ile “Tanzania ya Viwanda” tuliyohubiriwa kwa mbwebwe na msisitizo wa sauti za juu, Pushapu nyingi na za harakahara sio tu haijapatikana mwelekeo wake pia unazua maswali mengi.
Mimi na vijana wenzangu tuliaminishwa viwanda viko njiani na ajira zitakuwa teletele/kedekede tulirukaruka kama ndama tukacheza Singeli huku dadaangu Amina akiweka vidole juu kwa bashasha tukikonyezana mambo si ndio haya.
Nakumbuka nilishangilia sana niliposikia maneno haya wakati wa kampeni, Leo nimeamka sina hata mia nawaza hivi iko wapi Tanzania ya viwanda ? Mimi nilitegemea kupata ajira kiwandani bado sioni dalili hata ya hicho kiwanda, Nimejikuta nawaza kwa sauti “kama Yule mtoto wa Mzee Yusuph jirani yangu sijui anaitwa nani amesomea nursing hajapata kazi mpaka sasa, Musa Toll nae kaenda ualimu nae hajapata kazi mpaka sasa , Peter Kamkono nae kasoma udakitari hajapata kazi mpaka sasa, hata Sudi Mabangi aliyesomea mambo ya biashara pale Dodoma nae hana kazi”
Nasikia wanaambiwa wajiajiri najiuliza hawa manesi na madaktari wajiajiri kwa kujenga hospitali zao ili wafanye kazi? taaluma yao ni kutibu , Na huyu mwalimu ajenge shule yake ili afundishe? Nasikia tu wamefungua kiwanda cha unga ivi kiwanda cha unga si ni mashine ya kusaga? Mara kiwanda cha cha alizeti ivi hii si mashine ya kukamua alizeti tu zile zapale Shelui na Singida mjini?
Je viwanda hivi vinaweza kutuajiri sisi vijana zaidi ya mili 28, Nahisi mimi sikuelewa vizuri maana ya kiwanda kuna vitu viwili hapa kuna (Factory na Industry) sasa nimetambua kuwa kilicho maanishwa ni “TANZANIA YA VIWANDA VIDOGOVIDOGO sema tu waliamua kufupisha nakuwa “ Tanzania ya Viwanda””
Ndio maana mpaka sasa sijasikia mahali serikali ikiweka jiwe lake la msingi kufungua kiwanda chake kama ilivyokuwa kwa awamu ya kwanza vilijengwa viwanda kama Mutex,Mwatex,General tyre na vingine vingi ambavyo Yule mzee wa awamu ya tatu aliviuza kwa hasira baadae akaja kutuomba msamaha Watanzania tukamsamehe, Serikali hii mpaka ikabembeleze wenye pesa waje kufungua viwanda venye mishara kiduchu kwa wazawa ili nao wapate gepu la kuita makamera na kuweka jiwe la msingi kwa mbwembwe kana kwamba ni cha Msema kweli mpenzi wa Mungu kama ni hivi kumbe hata Yule Masai wa Monduli angeweza masikini tulijichanganya sana Watanzania.
Tukaambiwa “Hapa kazi tu” nahatukuuliza kazi gani? Kumbe ni kazi ya kupamabana na wapinzani tu! Maskini tulijichanganya hili hata Yule Mama Mzalendo wa Singida angeweza tena vizuri, Nikiwa pale formu one Mwl wangu aliwahi kuniambia kuwa “ The great thing in this world is not where we are but in which direction are we moving to” akasema swala sio kwanini tuko hapa bali ni wapi tunakwenda!
”Mungu ibariki Tanzania na watu wake”