Ndoto za kupaa na kuelea hewani zinaashiria nini?

mkuu ushawahi kujaribu kupaa kikweli kweli nje ya ndoto!?
siku moja panda benjamini tower pale posta ukifika juu jiachie
 
Mmeshindaje wakuu,

Mara nyingi nimekuwa nikiota ndoto kama napaa hewani, imetimia miaka miwili sasa toka nianze kuota ndoto ya namna hii. Ndoto hii ninaiota atleast mara moja kwa mwezi, naota nikiwa katika mazingira tofauti nikawa nipo mitaani tu napaa hewani watu wananishangaa nikifika kwenye nyaya za umeme nina zikwepa nazidi kwenda juu zaidi.

Siku nyingine naota nipo kwenye ndege halafu ndege imepata ajali wengine wanapata madhara lakini mimi ninaendelea kuelea angani. Ili nipae angani huwa natakiwa niinyooshe mikono hewani dnipo napaa hewani zaidi na nikitaka kushuka chini nashusha mikono chini nikitaka kwenda angani tena nanyosha mikono juu.

Muda huo nikiwa angani huwa nakuwa na furaha sana na hatimae nikiamka asubuhi siku yangu huwa ya furaha sana.

Michango yenu wakuu, ni kawaida kuota ndoto inayojirudia rudia mara nyingi? Ndoto hii ina maana gani?
ASANTE ukiota unapaa maana Yale kama kunajambo Lina kutatiza utavuka salama tena kwa mafaanikio au utasafiri.
 
Mmeshindaje wakuu,

Mara nyingi nimekuwa nikiota ndoto kama napaa hewani, imetimia miaka miwili sasa toka nianze kuota ndoto ya namna hii. Ndoto hii ninaiota atleast mara moja kwa mwezi, naota nikiwa katika mazingira tofauti nikawa nipo mitaani tu napaa hewani watu wananishangaa nikifika kwenye nyaya za umeme nina zikwepa nazidi kwenda juu zaidi.

Siku nyingine naota nipo kwenye ndege halafu ndege imepata ajali wengine wanapata madhara lakini mimi ninaendelea kuelea angani. Ili nipae angani huwa natakiwa niinyooshe mikono hewani dnipo napaa hewani zaidi na nikitaka kushuka chini nashusha mikono chini nikitaka kwenda angani tena nanyosha mikono juu.

Muda huo nikiwa angani huwa nakuwa na furaha sana na hatimae nikiamka asubuhi siku yangu huwa ya furaha sana.

Michango yenu wakuu, ni kawaida kuota ndoto inayojirudia rudia mara nyingi? Ndoto hii ina maana gani?
ASANTENI.

CC: MziziMkavu Pasco

Unaelekea kuwa popobawa.
 
Last edited by a moderator:
5: Bora Tu Ungesema TIYARA Tukajua Moja Unahadithia Na Chumvi Za Watoto.. kwamba Warusha Tiara... Sio Majini Tu Na Nafsi Za Watu Zinachangia na Kikubwa ni Akili..... hayo madubuasha yapo ila matatizo mengine ya kwenu wenyewe mnasingizia mizuka..

"Rakims"
Amini au usiamini hilo silo suala langu kazi kwako.
 
Mimi nikiota mtu ninae mfahamu amevaa nguo nyeupe au shela za harusi kwa mwanamke basi mtu huyo atafariki, imeshanitokea hii zaidi ya mara nne,
 
Waugwana na hii ya kumfikiria mtu au kitu chochote na baada ya muda mfupi ukakiona au ukamwona huyo mtu uliyekuwa unamfikiria, hiyi nayo imekaaje? Msaada tafadhari kwa anayejua utafafanulie.
 
ukiwa nae huyu Jini Twiyara anakuwa anakurusha kila siku unapolala na kukuharibia mambo yako ya kimaisha baadae ana geuka kuwa jini mahaba na unakuwa kila ukipata pesa hazikai kama ni wewe ni mwanamme huwezi kukaa na mwanamke au kama wewe ni mwanamke huwezi kuishi kwenye ndoa utakuwa unaolewa na kuachwa kila mwaname au kama una mpenzi wa kiume kila wakati mutakuwa munagomban kila wakati. Sio Jini mzuri ni Jini mbaya huyo.

Brother kusema ukweli mimi mwenyewe huwa naota naruka juu kama wewe na feeling zote unazoziota na mimi huwa zinanitokeaga,niliwahi kuota nipo sehemu flani kuna baridi kali lakini pametulia na ni pasafi sana.Baada ya miaka kama 5 nikajikuta nipo sehemu hiyo physically ilikuwa San Francisco USA sasa baada ya kufika hiyo sehemu nikapaona kama siyo sehemu ngeni wakati nilikuwa sijawahi kufika USA then baadae ndiyo nikakumbuka kuwa sehemu hiyo ilishawahi kunitokea kwenye ndoto.

Sasa hivi nasumbuliwa na ndoto ya kuwa darasani nasoma ama nafanya mitihani lakini kila siku navoota ndoto hiyo najiona kama nastrugle yaani inafika kipindi mwalimu anasema pen down mimi nakuwa nimejibu maswali 4 kati ya maswali 20 na bahati mbaya muda unaisha wakati maswali yote nayafahamu lakini siwezi kuyajibu either kalamu inagoma kuandika ama najikuta nimechelewa kuingia kwenye chuba cha mtihani ama nakosa chumba cha mtihani mpaka zikiwa zimebaki kama dakika 20 ndiyo naona venue ya mtihani.Kusema ukweli ndoto hii siijui hata kidogo na inanisumbua sana

Mmh hiyo ni rahisi sana ,haikusumbui ila tahadhari. Waweza kuchelewa jambo,unalofanya sasa fanya Kwa moyo na umakini
 
Amini au usiamini hilo silo suala langu kazi kwako.

Mkuu Sina Vita Vya Maneno Isipokuwa What I Wanna Tell You Is Dat

"Unatakiwa Uwe Unaangalia Both Sides Light(mwanga/mwenyezi mungu) & Dark(Giza/Shetani)"

Sio Kila Ndoto Ni Ya Majini Naimani Hata Kitabu Chako Kinasema Kuna Ndoto Aina Mbili

1: ndoto minnah llahi..! ndoto ya mwenyezi mungu..

2: ndoto minna Shaitwani..! ndoto ya shetani...

sikufundishi mkuu maana huta kubali tufanye nakukumbusha tu, maana najua unajua ni kweli..

"Rakims"
 
Mkuu Rakims na MziziMkavu hivi ndoto za asili ya "damu " zina maana gani?

Yaan umeona damu kwa njia yeyote ile???

Mkuu Ndoto Inatafsirika Baada Ya Mtu Kusema Alivyoiota...

hilo swali sawa na kuuliza hivi ndoto ya maji inamaana gani binafsi siwezi kukujibu labda Mzizi Apo.. Mimi Takujibu Pale Utakapo Niambie Umeota Damu Ipi Na Vipi...

mfano wa maji kuna maji ya mvua maji ya kisima maji ya chooni maji ya madafu... umeelewa?

yani tuje damu

damu kunywa? damu kutoka? dam kutiririka? damu kuvuja? damu kuzagaa? sijui umenifahamu ninacho maanisha?

hapo hata huyo MziziMkavu Akikupa Jibu La Moja Kwa Moja Kwamba:

"Damu Inamaanisha Hivi Pamanent Tampinga Tena"

"Rakims"
 
Last edited by a moderator:
Waugwana na hii ya kumfikiria mtu au kitu chochote na baada ya muda mfupi ukakiona au ukamwona huyo mtu uliyekuwa unamfikiria, hiyi nayo imekaaje? Msaada tafadhari kwa anayejua utafafanulie.

Hiyo Ni Aina Ya Uwezo Wa Mtu Binafsi Will/Brain Power Pita Kwa Pasco "Psychic Powers Ni Nguvu Za Kufanya Miujiza ukajifunze hii yako

"Rakims"
 
Huwa siamini katika majini na mizimu mkuu, lakini suala la kuota ndoto za kweli huwa linanitokea. Kipindi hicho nipo form six niliwahi kuota mwalim wangu mmoja amekufa lakini kwa wakati huo mwalimu yule alikuwa mzima kabisa na haumwi lakini wiki moja badae yule walimu alikufa, mahali ambapo ninafanya kibarua sasa niliota ninafanya kazi hapa kipindi hicho kabla sijamaliza chuo, kuna kipindi niliota nipo nchi za magharibi miezi sita badae nikasafiri. Ni mengi sana mkuu, kuna kipindi naota nikiamka nakuwa nimesahau lakini siku kitu kimetokea kumbukumbuku zinakuja kuwa nilishawahi kuota kitu cha namna hii.

Mkuu hebu mpokee Yesu atakuonyesha mambo makubwa zaidi ya hayo. ...
Hapo upande wa pili ndo unakutumia kwa karama ileile ambayo Mungu amekujaalia....
 
Back
Top Bottom