Ndoto za Hayati Magufuli na Tanzania Mpya

Maxmillian Samike

New Member
Jul 16, 2021
2
0
Hayati John Pombe Joseph Magufuli, ni mzaliwa wa chato mkoani Geita, pia alikuwa mbunge, naibu waziri na waziri katika nyakati tofauti, tofauti enzi la utawala wa Benjamin Mkapa na Rais mstaafu wa awamu ya nne Mh. Jakaya kikwete, hatimaye mnano mwaka 2015 alijitosa kugombea urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha mapinduzi.

Hatimaye alifanikiwa kushinda kiti Cha urais na kuapishwa kuwa Rais mnamo mwezi November 2015 kuwa Rais wa jamhuri ya muungano wa TANZANIA.

Baada ya kuapishwa alikuja na Sera mbalimbali nyingi na nzuri za kuipaisha Tanzania kiuchumi katika duru za kimataifa, alikuwa na mikakati mbalimbali ikiwemo, kubana matumizi ya fedha za serikali, ujenzi wa viwanda,ujenzi wa miundo mbinu, Barabara za fly over katika jiji la dare es salaam, mapambano dhidi ya ufisadi na rushwa, ujenzi wa vituo vya afya, zahanati na hospital za wilaya na mikoa Tanzania nzima.

NDOTO ya hayati John Magufuli ilikuwa kuifanya Tanzania kuwa mpya na yenye kuhudumia wananchi wake wa Chini na wenye Hali duni.

MAPAMBANO DHIDI YA RASILIMALI ZA TANZANIA
Hayati John Magufuli alipambana kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya mfano wa kuigwa barani Africa hata ulaya. Alilinda rasilimali za nchi,kwa nguvu zake zote, mfano alizuia makinikia yasipelekwe nchi za nje kwenda kusafishwa,alijenga ukuta kuzunguka mgodi wa Mirerani Arusha kuzuia kutoroshwa madini ya Tanzanite. Alihimiza kufanya kazi kwa bidii,na kusisitiza ulipaji wa Kodi na kudai risti.

MAPAMBANO DHIDI YA UGONJWA WA CORONA (COVID-19)
Hayati John Magufuli alipambana na UGONJWA WA CORONA COVID-19,kwa huwahimiza wananchi kuchukua Tahadhari zote na kuuchukulia Kama ugonjwa wa kawaida.

ambapo alitibu kabisa kuondoa hofu kwa wananchi vile vile,alifanya specimen ya kuchunguza huu ugonjwa na kupeleka sample zake maabara kuu ya taifa na kugundulika kuwa mapapai, mbuzi, fenesi na kondoo kuonekana wana maambukizi ya Corona.

Mwisho, hayati JPM alikatika TU kama mshumaa na kuacha giza Nene na pengo lisilozibika kwa watanzania.
bado tuna vidonda mionyoni mwetu.

Lala salama JPM.
 
Back
Top Bottom