Ndoto za Afrika Kuwa Nchi Moja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndoto za Afrika Kuwa Nchi Moja

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SolarPower, Apr 14, 2011.

 1. S

  SolarPower JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 226
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yamesemwa mengi lakini bado naona giza nene na sioni matumaini ya Afrika kuwa nchi moja hata baada ya miaka 1000 ijayo.
   
 2. N

  Nonda JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu.

  Hii dhana ya Afrika kuwa nchi moja ni dhana dhaifu.

  Ukiangalia ukubwa wa Afrika kieneo. Miundo mbinu yake, mifumo ya utawala inavyotafautiana, wingi wa wakaazi wake, makabila na lugha zinazotumika hii kitu, Afrika kuwa nchi moja ni mradi hewa.

  Wala Afrika haihitaji kuwa nchi moja.

  Nionavyo mimi Afrika inahitaji stable countries ambazo zitaunda regional blocks, 3,4 hivi ambazo zitafanya kazi ya kuboresha ushirikiano wa kikanda na ukuzaji wa biashara miongoni mwao ili kupunguza utegemezi wa US na Europe.

  Lakini katika kuelekea kuwa na strong blocks ni lazima zifate hatua baada ya hatua sio kutaka kuruka kabla ya kutembea na zisiendeshwe kwa mtaji wa kisiasa tu kama tunavyofanya maamuzi ya EAC. kuharakisha kila kitu. Fasta fasta! Hatutafika mbali.
   
 3. w

  warea JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2011
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata afrika mashariki haipaswi kuwa nchi moja. Ni matatizo matupu badala ya kujenga kipya, tunakaa kuziba nyufa kama za Tanzania
   
 4. S

  SolarPower JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 226
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante Mkuu Nonda kwa maoni yako. Binafsi ningetemea tuanze kwanza na mambo yafuatayo katika kuwafanya watu wa Afrika kuwa karibu zaidi kabla hata ya kufikiria kuziunganisha nchi zote za Afrika kuwa nchi moja. Baadhi ya mambo hayo ni

  1. Kuwa na Lugha moja ya kutuwafanya Waafrika tuweze kuwasiliana kwa karibu na kwa urahisi zaidi. Bahati nzuri miaka 6 iliyopita viongozi wetu wa Afrika walikubaliana kwa pamoja kuwa ifikapo mwaka 2020 Kiswahili ndiyo kitakuwa lugha kuu na rasmi ya Afrika. Je tunafanya nini katika kutimiza ndoto hii. Sidhani kama Tanzania tuna mkakati wote katika kuhakikisha ndoto hii inatimia.

  2. Tuanzishe AFRICA GLOBAL TELEVISION NA KWAME NKRUMAH FUND FOR THE UNIFICATION OF AFRICA.

  3. tuanzishe Africa Tele-Universities (tujifunze toka Cuba) na Africa PostGraduate na PhD Universities angalau 5 kila baada ya miaka mitatu.

  4. Tuanzishe Africa High Tech Secondary Schools ambazo zitachukua wanafunzi toka kila nchi ya Afrika na wanafunzi wetu kusoma pamoja. Pendekezo ni kuwa ifikapo mwaka 2030 tuwe na angalau shule 1000 za namna hiyo ndani ya bara letu la Afrika

  5. Pia tunahitaji kuwa na Africa Tele-High Schools kwa masomo kama Hisabati, Fizikia, Hisabati, Jiografia, Biolojia, Kemia, Mazingira, Kingereza; Kifaransa; Kichina; Kireno; Kiarabu na Kispania.

  6. Tuliunganishe bara letu kwa kutumia Optic fibres.
   
 5. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,738
  Likes Received: 1,450
  Trophy Points: 280

  Nonda asante. Very well nailed!!
  Hizo ni ndoto za wafu
   
Loading...