Ndoto yangu na ushauri kwa mnaotaka kuhama vyama baada ya kutoteuliwa kugombea nafasi za kisiasa katika vyama vyenu

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
295
679
Zaituni Stephen

Nikiwa mwananchi wa kawaida ambaye ninafuatilia mwenendo wa siasa za Tanzania, nimeoteshwa ndoto kubwa kuwa baadhi ya watu ambao walitarajia kuteuliwa kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa wanakimbilia vyama vingine mbadala ili wakagombee.

Kugombea si kosa ila unapoachwa kisha unakimbia haraka upande mwingine ni ishara kuwa huko ulikokuwa hukuwa kwa sababu ya mapenzi ya Chama hicho bali Chama hicho kilikupa fursa ukapata nafasi na kupata hela.

Leo nilipokuwa Kanisani nimesikia kwa uhakika kuwa baadhi ya Wazee wa CCM wameanza kuzungumza na Wapinzani wa Serikali ambayo wao walikuwa ndio wanaiongoza ili wahamie kwao. Hii kitu ni hatari sana kwani wakishakwenda na wakakosa ndio basi tena!

Ninavyojua mimi, huwezi ukahama ukaenda upande wa pili ukashinda kirahisi kwani kule unakuwa ni mgeni sana kisiasa.

Wapo Wazee waliodumu kwa muda mrefu ndani ya CCM ambao ukitazama kwa umri wao wanahitaji kula pension tu hadi Mungu atakapowaita. Wanapaswa kuachana na frustration za Siasa na kuwa kimbilio kwa Chipukizi wanaotaka kuingia katika siasa.

Amewahi kusema Makongoro Nyerere; kuna watu tangu awamu ya kwanza wao wapo. Awamu ya pili, wapo! Awamu ya tatu -wapo! Awamu ya nne - wapo na sasa awamu ya tano wanataka waendelee kuwepo tu.

Kuna wakati ni muhimu kuachia fursa kwa watu wengine na mpate fursa nyingine za kulitumikia Taifa. Nchi hii inahitaji watu wazalendo. Kuwepo watu wengi wazalendo kutaongeza ufanisi katika shughuli za kuleta maendeleo na kuitetea nchi yetu dhidi ya watu wasiotutakia mema.

Katika masuala ya siasa ndani ya vyama kuna suala linalohusu wananchama kukubali mabadiliko ndani ya chama kwa mujibu wa katiba ya vyama yanayolenga kuleta maslahi mapema ndani ya chama ambapo wanachama ulazimika kuunga mkono mabadiliko hayo kwa maslahi ya chama.

Kitendo cha baadhi ya watu kuanza kuwaza “mauzo”, yaani kuuzwa upande mwingine sio dili sana wakati huu. Ni au unapoteza au ndio unajizika kisiasa.

Katika suala hili sitowataja baadhi ya wanachama wa CCM ambao wameanza mazungumzo ila kwa heshima yao nimeona nianze kuwapa ndoto yangu na ushauri kwanza.

Wito wangu kwa wanachama wa CCM wanaotaka kikihama chama hicho wakumbuke kuwa kulingana falsafa za chama hicho kwamba japokuwa hawajateuliwa na chama kugombea wanapaswa kuwaunga mkono waliopitishwa ili kuhakikisha chama kinapata ushindi, la sivyo wataonekana kuwa walikuwa ndani ya chama kama mamluki wenye maslahi yao binafsi.

Katika mpango huo wa kuhama chama hicho ninawaonea huruma wazee waliodumu ndani ya CCM kwa muda mrefu kwani watafanikiwa kuhama na kwenda huko wakadhani kunafaa ila wakumbuke kuwa watazikwa kwa aibu kwani vyama hivyo watakavyohamia haviwezi kuwastihili kulingana na heshima yao yaliyoijenga ndani ya CCM na Taifa kwa ujumla.
 
Tatizo sio kuhama, tatizo ni kutotendewa HAKI. UONEVU unauma we acha tu, haiwezekani ukatwe kwa sababu ya takwa la mtu mmoja tuu tena kwa utashi wake yeye. NDUGU KAA KIMYA MAANA WEWE HAYAJAKUKUTA.
 
Hii Nchi kuna watu wanaijenga matumbo yao yakiwa yamejaa wakati kuna wengine wanajenga matumbo yakiwa tupu.
 
Tatizo sio kuhama, tatizo ni kutotendewa HAKI. UONEVU unauma we acha tu, haiwezekani ukatwe kwa sababu ya takwa la mtu mmoja tuu tena kwa utashi wake yeye. NDUGU KAA KIMYA MAANA WEWE HAYAJAKUKUTA.
Tulia acha kulia lia isome namba kwanza
 
Ulipokuwa Kanisani ulisikia baadhi ya Wazee wanazungumzia kutaka kuhamia Upinzani; Je huko kanisani Mnakwenda Kumwabudu Mungu au Mnakwenda kupiga siasa? Kanisani na habari za kuhama vyama wapi na wapi?
 
Acha uhuru na demokrasia vifanye kazi ccm haikubaliki isipokuwa kwa wanaofaidika nayo kiuchumi.
 
Back
Top Bottom