Ndoto yangu kuhusu kitwete inamaana gani? Watafsiri nisaidieni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndoto yangu kuhusu kitwete inamaana gani? Watafsiri nisaidieni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KIDUNDULIMA, Oct 17, 2010.

 1. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2010
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 773
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Usiku wa kuamkia leo nimeota ndoto. Tulikuwa Mimi na Kikwete kwenye kingo ya mto mmoja mkubwa. Ng'ambo kulikuwa na kundi kubwa la watu wakisikiliza kampeni za kikwete. Kama kawaida yanke akamwaga ahadi yake kwa wale watu kuwa atawajengea daraja mahali pale. Ilipofika wakati wa kuondoka kilichonishangaza ni kuwa huyu Kikwete hakuwa na wasaidizi wala maboardguard. Wakati wa kupanda kingo ya mto aliteleza hivyo nikalazimika kumyanyua mabegani akafanikiwa kutoka na akatokomea bila hata kuniaga. Baada ya muda kidogo zilitelemshwa kamba nyingi na watu ambao siwafahamu ili nikamate mojawapo niweze kutoka kirahisi na kuingia kwenye jengo moja kuwa ambalo lipo karibu na huo mto. Kabla sijakamata ile kamba akatokea mtu mwingine ambaye ni mwanamke akanioshesha njia mbadala ambayo haikuitaji kupanda ile kingo ya mto. Wakati nafikiria ni wapi ili njia aliyonionyesha yule mwanamke itanipeleka, ghafla donto yangu ikaisha.
   
 2. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ogopa sana kutangaza ndoto zako hadharani.Nyengine huwa zinakuhusu wewe mwenyewe na wala si yule unayemuota.
  Wataalam wa ndoto ni sisi waislamu.Nakushauri soma vitabu vidogo vidogo vya ndoto kutoka maduka ya vitabu utaelewa.
  Ibn Seeren ndiye mfasiri mkubwa wa ndoto kutokana na Qur'an na hadithi za Mtume Muhammad swallaLlaahu alayhi wa sallam.
  Kwanza tunakuangalia wewe mwenyewe ni mtu wa aina gani na Hiyo ndoto umeiota muda gani?,ni usiku,mchana,karibu ya alfajiri n.k.
   
 3. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Aisee...hiyo ndoto kiboko!
  Tafsiri yake hii: Kundi la Watu upende wa pili wa mto ndio wananchi na watanzania wanopoteza muda kumsikiliza JK wakati yeye yupo upande wa pili Ukweli, yaani JK na wanaomfuata hawako in sync (hawana dira moja). Na alipokuwa hana walinzi, ni ishara iliyopo ndani ya CCM kulivyoparaganyika, ndio maana amebaki tu na familia yake - kumbe nao wako ktk kampeni kwingineko. Na alipomaliza ahadi akateleza akatumbukia ukamwokoa ni ishara kuwa mwaka huu hana jinsi, ataachwa na CCM wenzake na mafisadi wake, ataokolewa naasiowathamini, ila bahati mbaya, alivyo na dharau na kujisikia, ametimka bila hata kukupa ahsante au kukuaga, kama anavyo wafanyia Wanzania na CCM wenzake, ila njia ya kuwaokoa imekuwa rahisi (ambayo ilikuwezesha kutokea), ndio CHADEMA, na Huyo mwanamke ni ishara tu ya Malaika mkombozi anayeifikia Tanzania kwa sasa kuwaelekeza kupata ukombozi...!
  aisee, usije ukadhani mie sheikh Yahya mdogo, yaani sitaki hata kusikia hilo jina la pepo wachafu....! PAMOJA DAIMA.
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,548
  Likes Received: 18,218
  Trophy Points: 280
  KIDUNDULIMA, hiyo ndoto yako iko too direct. Inawezekana uliwish sana JK ashindwe, hivyo hiyo ndoto imejust grant your wish.

  Kuna ndoto huwa ni za ukweli zinaitwa 'preamunition' kwa jambo litakalotokea kabla halijatokea lakini hizi ndoto huwatokea mabwana wa ndoto kama Yusuph/Joseph. Jee wewe KIDUNDULIMA, uu mmoja wa mabwana wa ndoto?. Jee kuna kitu uliwahi kukiota halafu kikatokea?. Kama hujawahi, then ni ndoto tuu kama ndoto, kama uliota kikatokea, basi JK ni safari.

  CCM wana waunderestimate sana Watanzania, kwa kutoa hizo fulani, kofia na kamshiko kidogo, this time hatudanganyiki tena, fulana tunavaa, nauli tunapokea, mikutano ya kampeni tunahudhuria, lakini siku ya siku tunajua kura tutapeleka wapi!.
   
 5. h

  hagonga Senior Member

  #5
  Oct 17, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 141
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Msaki001, safi kabisa inaelekea wewe mfasiri kwelikweli, naona umepatia.
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kidundumila,
  Unamkumbuka Yusuf katika Biblia? Na ndoto alizokuwa nazo tangu utotoni? Naomba usome tena historia ya Yusufu, hasa pale anapomwambia
  yule jamaa aliyenyongwa na mfalme kipi kitakachomsibu na hakumwamini. Hapo utapata jibu la ndoto yako.
   
 7. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Na iwe hivyo
   
 8. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  sema tu wataalamu wa ndoto nyie kina shekhe yahya
   
 9. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #9
  Oct 17, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
 10. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ulikuwa baharini. Na huyo mwanamke ndilo jini la KIKE alilosema Shehe Yahya. Lilikuwa linataka kura yako. Sasa fanya maombi ili upige kura yako kwa busara...Slaa for president
   
 11. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #11
  Oct 18, 2010
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 773
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Sikuwa baharini, nilikuwa kando ya mto
   
 12. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #12
  Oct 18, 2010
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 773
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Ndoto zangu mara nyingine huwa zinakuwa za kweli sasa sijajua hii kama ni ya kweli au la ndio maana nimeomba msaada wa taalamu wa kutafsiri
   
Loading...