Ndoto yangu kuhusu bomu la Nyukilia la Korea Kaskazini

b191

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
742
1,031
Nawasalimu wanajamvi wote na ninaamini wote ni wazima. Kwa wale wenye matatizo Mungu awasaidie kadiri ya mahitaji yao.

Wapendwa someni kwa makini halafu mnisaidie kiroho, hii inamaanisha nini.

"Jana nilipita Kanisani (sikuwa na shughuli maalum) na nilipofika nilikuta waumini wanajiandaa kwa ajili ya sherehe ya leo kwa kufanya usafi. Niliona Kanisa ni chafu na nikaamua kuchukua tambala la deki na kuanza kudeki baadhi ya sehemu. Baada ya kumaliza nikatoka nje ambapo nikakuta kuna uchafu pia, nikawashawishi waumini wenzangu tufanye usafi ili kanisa liwe safi. Tulifagia pamoja kwa muda mfupi na wakaondoka, kiukweli nilifanya usafi vizuri sana peke yangu. Baada ya kumaliza usafi niliamua kurudi nyumbani (nilikuwa kwa mguu) njiani rafiki yangu akanipa lift ya gari (Double Cabin) na nilipokaribia nyumbani Mwanangu akataka kushuka (ila sijui gari alipandia wapi) ili akacheze na watoto wa jirani yangu nikamzuia. Tulienda wote hadi nyumbani na rafiki yangu na tukakaa nje kwenye kivuli cha turubai huku tukiangalia habari na familia ikiwa ndani, tukaambiwa kuwa kuna Bomu la Nyuklia kutoka KOREA YA KASKAZINI kwenda MAREKANI linapita angani hivyo tuangalie ili tulione. Mimi na rafiki yangu tukaangalia na kuliona bomu likipita. Ghafla bomu liligeuka na kuanza kushuka kuelekea pale tulipo, tulikimbilia nje ya fensi ili kujiokoa. Bomu lilikita palepale tulipokuwepo na kwa bahati nzuri au mbaya halikuzama lote. Nilipokuwa nje nikajipa ujasiri, nikasema lazima nirudi na nikifika haliwezi kulipuka na kuteketeza familia na watu pia. Nilipofika nilikuta lina kama maji yanayochemka tayari kwa kulipuka. Kwa kusimama pale taratibu yale maji yakatulia na bomu halikulipuka"

Hapo nikaamka kutoka usingizini na nikamuomba Mungu kama hiyo ndoto ni neema na itokee ila kama ni balaa na isitokee.

NINACHO JIULIZA HII NDOTO INA MAANISHA NINI?
 
Maana yake wale waumini wenzio ndio watakao late maneno juu yako kwa kujitoa kwako kanisani.Adui yako yuko humohumo kanisani ila Mungu anakulinda.Omba ili Mungu akuonyeshe.
 
mkuu tafuta mtu akulalie, wewe usiludie tena kulala north korea wana visa wewe ndo maana wamekupa onyo,nakushauli nenda huko kwao mkalipuane wenyewe wengine tusije tukalipuka kwa mambo yasiyotuhusu,haiwezekani bomu la kwenda kwa trump lije kwako kuwa makini.
 
b191 ingia kwenye maombi ili Roho Mtakatifu akufunulie siri ya Ndoto yako.
Humu utapata tafsiri tofauti za miungu ya ajabuajabu ambazo ziko kinyume na kusudi LA MUNGU aliye hai. Kumbuka, shetani ni baba wa uongo, ataipindua tafsiri ya Ndoto yako na kupoteza kabisa ujumbe/ uthamani wa Ndoto hiyo
 
mkuu tafuta mtu akulalie, wewe usiludie tena kulala north korea wana visa wewe ndo maana wamekupa onyo,nakushauli nenda huko kwao mkalipuane wenyewe wengine tusije tukalipuka kwa mambo yasiyotuhusu,haiwezekani bomu la kwenda kwa trump lije kwako kuwa makini.
Usirudie,
nakushauri
 
Back
Top Bottom