Ndoto ya Zanzibar katika muungano wa heshima, haki na usawa


Kakke

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Messages
1,862
Likes
694
Points
280
Kakke

Kakke

JF-Expert Member
Joined Dec 4, 2010
1,862 694 280
[h=1][/h]Written by Stonetown (Kiongozi) // 03/12/2013 // Makala/Tahariri // 1 Comment


Na Farrell JNR Foum
Katika sehemu hii ya leo tutatazama namna ya uboreshwaji wa mfumo wa muungano ili uwe na nguvu za kisheria, legitimacy kwa wananchi na pia maendeleo yaliokusudiwa katika uundwaji wake. Kwa sasa mfumo wa serikali mbili kuelekea moja umefeli na kuundeleza ni kuendeleza makosa yalioleta chuki, fitna na ukiritimba mkubwa wa maendeleo nchini.
Sina haja ya kurejea historia ya muungano huu au uasisi wake kwa sababu ya controversies zinazouzonga mfumo mzima wa muungano kuanzia uundwaji wake na miaka karibu hamsini ya uhai wake. Ila tutatazama namna ya kuuboresha na kuhakikisha mfumo ujao utajenga culture ya kuaminiana, kufahamiana na kurejesha heshima iliokuwa kama ni lengo la kuungana hasa kwa namna ya wazanzibari waliowengi walivyoufahamu muundo huu na kuamini kama ndio maudhui makuu ya uundwaji wake. Nasema hivi kwa sababu kumetokea taswira za aina mbili za upokewaji wa muungano, upande mmoja hususan ndani ya mamlaka ya Zanzibar wakiamini uwepo wa nchi ya Zanzibar kama ni paramount katika maamuzi yoyote ya uwepo wa muungano huu wakati upande wa pili ukijijenga zaidi katika safu za kuhakikisha muungano huu utakuwa define kama ni wa nchi moja iliokamilika.
Imani yangu na wazanzibari walio wengi ni kwamba Zanzibar ni nchi iliokamilika na kujiendesha kwa misingi ya kimamlaka yanayoongozwa na ile supreme command ya rais pamoja na serikali alioiunda baada ya kuridhiwa na uchaguzi unaotegemewa kuendeshwa kwa misingi ya demokrasia. Katiba ya Zanzibar hususan baada ya mabadiliko ya 2010 yameonyesha kwa uwazi bila ya kuweweseka kwamba ni nchi na ikaenda mbali zaidi kuhakikisha mamlaka ya mkuu wa nchi hii hayatakuwa na kigugumizi kwa kuingiliwa na nguvu nyengine ndani ya muungano hasa baada ya kuhakikisha kwamba ni rais wa Zanzibar pekee mwenye madaraka na uwezo wa kuigawa Zanzibar katika mikoa bila ya ushauri wa yeyote kinyume na ilivyokuwa awali. Uthibitisho wa haya ni kura ya maoni ambayo so far inatazamwa kama ni mfano wa uchaguzi pekee ulioendeshwa kwa uwazi zaidi huku kundi la yes vote likibeba nguvu ya zaidi ya asilimia 66 ya wananchi walioikubali referendum hio.
Katika manifesto ya CCM ya mwaka 2010 suala la mabadiliko ya katiba halikuwemo na wengi tunaamini kwamba mabadiliko ya katiba ya muungano yamekuwa triggered na mabadiliko ya katiba ya Zanzibar ya 2010 hasa baada ya kuona kwamba katiba mbili haziendani kimantiki hata kisheria na kwa vile referendum ya Zanzibar ilibeba mass kubwa ya wananchi walioipitisha hakukuwa na budi zaidi ya kuifanyia marekebisho katiba ya muungano ili iendane na sauti ya asilimi 66 ya wazanzibari.
Muundo ambao mheshimiwa Warioba na tume yake waliokuja nao umethamini kauli ya wananchi wanaounda muungano huu na kwamba ile dhana ya udogo wa sehemu ikawa ndio kigezo cha kuburura maoni yao iliondoshwa kwa vile msingi mkuu wa muungano ni nchi mbili regardless ya ukubwa au population zao ziliungana na ni lazima mabadiliko yoyote yathamini maoni ya pande mbili independent ya mwenzake ili kupata compromise baina yao na kuunda kitu kitachokiubalika na wote. Ndio maana ukakuta hata baada ya mamilioni ya watanganyika waliotamani serikali moja hayakuridhiwa kuwekwa katika draft ya kwanza ya katiba kwa sababu yalipingana na ya wazanzibar hata wakiwa na population ndogo compare na bara. Maoni yangu ni kwamba Mheshimiwa Warioba ametupa heshima tunayostahili wazanzibari katika muungano huu na pia hope ya kwamba mfumo ujao utaweza kuwa ni kielelezo kipya cha mabadiliko makubwa zaidi katika mfumo wa muungano utaojengwa kwa misingi thabit ya kuheshimiana, kuaminiana, haki na usawa.
Muundo wa muungano
Wengi tunaamini mfumo wowote wa muungano katika ndoto ya wazanzibari iendane na kauli mama ya Zanzibar kama ni nchi na yenye kujiendesha yenyewe kimamlaka. Mifumo butu yenye taswira moja lakini lengo lililojificha halitakubaliwa katika ulimwengu wa sasa wa utandawazi hasa ukizingatia kwamba ari ya kuja na mfumo wa mkataba haukuwa na uasisi wa chama chochote bali wananchi wa kawaida ndani na nje ya visiwa hivi walioona mbali zaidi na kuhakikisha mfumo ujao hautakuwa na kigugumizi chochote juu ya uhalali wa kuwepo kwa taifa la wazanzibari. Hili linawezekana hata ndani ya mfumo wa serikali mbili ikiwa content za yaliomo ndani ya muungano yatazingatia maoni ya wengi yalioweka wazi msimamo wa Zanzibar kama ni nchi yenye kila nyenzo ya kujitosheleza na kujiendesha yenyewe. Mheshimiwa Warioba kafahamu maana kamili ya muungano wa mkataba na ndio maana akaja na draft ya mwanzo ya mfumo wa serikali tatu na ukakuta wengi waliopendekeza mfumo wa mkataba hawakuwa na upinzani wa serikali tatu kwa sababu ya content zilizobebwa ndani ya draft hio iliopunguza mambo ya muungano kutoka zaidi ya 30 hadi kufikia saba. Ndio ukakuta wanamageuzi wakweli hawazingatii jina la mfumo wa muungano bali content zinazobeba muungano wenyewe na kwa sasa nguvu zimeelekezwa katika kuyafuta yale yatayokwenda kinyume na azma ya mamlaka kamili.
Hoja zisizo na mashiko kama gharama za muungano katika mfumo wa serikali tatu zenye kujitegemea zinaelekezwa zaidi kama khofu hususan kwa wazanzibari kama vile nchi hii haitaweza kujiendesha wenyewe wakati wahubiri hawa wanashindwa basi kuwaeleza watu kabla ya muungano huu serikali ilijiendesha vipi? Ukiangalia zaidi kabla ya kifo cha Mzee Karume muungano huu haukuwa na msimiko mkubwa kama baada ya kifo chake na intergration kubwa iliounda CCM ambayo ikabeba dhima kubwa zaidi hata ya mamlaka ya kikatiba ya nchi. Katiba ya nchi ikawa chini ya katiba mama ya chama na gradually tukaona mapungufu ya muungano yakizidi kukuwa na kila alieweza kupayuka kupinga msukumo wa chama wakawa maadui wa nchi. Mpaka leo hii sifahamu iweje Rais wa nchi aliechaguliwa na wananchi, akafukuzwa urais huo ambao aliupata kabla ya hata muungano wa ASP na TANU kwa kutazama matakwa ya nchi yake kwanza. Hakuna justification yoyote zaidi ya ghilba za kupitia mlango wa nyuma kuhakikisha lengo si muungano bali nchi moja bila ya hata maoni ya wahusika wakuu.
Kauli za Zanzibar tunachangia kiasi gani katika shughuli za muungano zisiwe ndio justification ya mfumo wa sasa, sugar coating makosa na kuficha tathmini za kitaaluma zilizoonyesha namna gani Zanzibar inapoteza fursa kubwa za maendeleo katika mfumo wa sasa kwa sababu rahisi rahisi kama hizi ni ukosefu wa vision pamoja na dhana nzima ya uongozi wa misingi ya haki. Masuala ya kujiuliza ni namna gani kwa mfano 4% ya mgao kwa Zanzibar uliofanyiwa tathmini miaka ya 60 wakati population ilikuwa ya watu laki tatu tu lakini ikabaki hiovyo hivyo kwa miaka karibu hamsini wakati population ni zaidi ya watu milioni moja na nusu!
Au tutatazame hizo gharama za uendeshwaji mfano jeshi la wananchi, kati ya nchi ya milioni arobaini against milioni moja contribution itakuwa ya ratio gani? Zanzibar ikiwa na eneo dogo mara mia kuliko bara wapi kunahitajika ulinzi zaidi na hivyo contribution ya Zanzibar itafanyiwa tathmini ya ratio gani? Au tutazame kwa upande wa urahisi zaidi, ikiwa tunaambiwa tuchangie sawa baina yetu jee na mapato tutagawiwa kwa misingi hio ya usawa kama ilivyo kwa uchangiaji? Muungano unajengewa mazingira ya kutishana badala uwazi utakaojenga heshima na kuthaminiana baina ya jumuia mbili zilizokaa pamoja kabla hata ya uhuru wa Tanganyika na hata Mapinduzi ya Zanzibar.
Hatuwezi kuendelea na mfumo wa sasa ambao unamuweka mkuu wa nchi moja katika baraza la mawaziri wa muungano na kutompa heshima yake kikatiba kama ilivyokuwa wakati wa kuasisi muungano huu. Hatuwezi kuendelea kuwa na wazanzibari ndani ya bunge la muungano wanaopiga kura bajeti za wizara zisizo za muungano huku tukiwa na Baraza letu mahsusi kwa ajili yetu wenyewe. Hatuwezi kuendelea na mfumo wa vyama kushika hatamu zaidi hata ya katiba ya nchi na matakwa ya wananchi katika nchi yenye mfumo wa demokrasia. Umma hautatuvumilia tukiwa wepesi wa kulalamika pale yanapotufika lakini tukawa wagumu wa mabadiliko yataondosha kero lukuki zinazorudisha nyuma maendeleo ya wananchi. Kauli ya mheshimiwa Pinda ndio iliozaa mabadiliko ya katiba ya 2010, sasa utawezaje kutamani rais mwenye mamlaka kamili bila ya nchi yenye mamlaka kamili? Watetezi wakuu wa mfumo wa muungano huu ndio hao hao waliosimamia, kuyapitisha na kuyaamini mabadiliko ya katiba ya Zanzibar ya 2010 wakijuwa wazi kwamba ile ni road map ya mabadiliko ya mfumo wa serikali mbili. Miaka 50 ya muungano imezaa kero zaidi badala ya suluhisho, hivyo wanaoamini kwamba mfumo wa sasa unahitaji utatuzi tu wa kero tuseme viongozi waliopita hawakuwa na nia ya kweli ya kutatua kero hizo hata washindwe kwa miaka 50? Hawaoni kwamba tatizo si kero kwa vile kero ni zao la mfumo wa sasa na kinachohitaji kurekebishwa ni mfumo mzima unaozidisha kero na hasama kila kukicha?
Ndoto ya wazanzibari katika mfumo mpya wa muungano tuutakao ni wa uwazi wenye nia ya maendeleo sio kiutawala, unaongozwa kwa misingi ya haki, heshima na usawa. Ikiwa tutatakiwa kuchangia kwa nini tusielezwe kwa uwazi formula itayotumika tukizingatia pia udogo wetu na kwamba input tutayoitia katika muungano ilingane pia na output ya mapato tutayoigawiana. Bunge dogo la muungano pamoja na serikali ndogo ya muungano kwa yale tutayokubaliana na azma kubwa ilenge maendeleo sio mlolongo wa watawala. Wananchi baina ya Zanzibar na bara tumeweza kuishi kwa vizuri kabla ya hata ya muungano, historia inaonyesha hakukuwa na mpasuko wa malumbano na naamini kwamba kinachoulinda muungano huu sio katiba au mfumo wa sasa bali historia ya pande mbili zilizojengeka kwa heshima, maelewano na amani. Tunahitaji mabadiliko ya kweli yatayoondosha kero na kelele za muungano ili tuzijenge nchi zetu kwa kutumia muungano kama asasi ya maendeleo na chachu ya mshikamano wa Afrika nzima.
 
manning

manning

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2013
Messages
3,528
Likes
116
Points
160
manning

manning

JF-Expert Member
Joined Apr 1, 2013
3,528 116 160
Ukiwa mdogo unatamani kuwa mkubwa, ukishakuwa mkubwa unatamani tena kuwa mdogo. Tuuangalie kwa makini muungano huu usije huko baadae ukaleta majuto. Na majuto ni mjukuu.
 

Forum statistics

Threads 1,252,128
Members 482,015
Posts 29,797,514