kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,298
- 12,600
- Thread starter
- #41
Mimi ni mtanzania namba moja mpenda nchi yangu. Ila ninachojua mimi misaada na mikopo mingi ni chanzo kikubwa cha kupoteza uhuru wetu na kutenda mambo ambayo hujayapanga kuyatenda huko mbeleni kutokana na madeni makubwa ya nchi. Hii ndiyo maana Mzee Makamba alimfukuza Matonya katikati ya mji. Hata akinamama wa vikoba wanafahamu sana ubaya wa mikopo mingi. Ni heri kwa pamoja tukashirikiana katika kuamua hatima ya nchi yetu kuliko kutegemea mtu au kikundi cha watu. Turudi nyuma tuangalie upya katiba yetu na vyanzo vyetu vya mapato vilivyoko.Kama wewe (mleta mada) siyo mtanzania una haki ya kuuliza swali hili. Lakini kama ni mtanzania hasa, yaani ni raia wa Tanzania lazima ujiulize kama unasifa stahiki kuitwa mtanzania. Pia ujiulize kama kuna faida yoyote ya wewe kujihusisha na utanzania wakati hufikiri nchi hii itajikwamuaje na utegemezi; zaidi wewe unawaza kukebei juhudi za wale wanaotaka Tanzania yenye nguvu kiuchumi na kijamii.