Ndoto ya tanzania kuingia kwenye machafuko - iyooo yaja

Mwamba Usemao Kweli

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
744
186
Tanzania imekwama tulipo si pazuri tena nawatahadharisha mlitambue hilo watanzania wenzangu. Kinachofanyika sasa ni kama kuwaandaa watu waanze kuwa waasi ndani ya taifa lao. zinajengwa chuki dhidi ya watawala, polisi n.k. Kinachokuja muda mfupi ujao kitakuwa majuto kwa nchi yetu. Hii ndio ndoto yangu kwenu leo.

Ombi langu kwenu ni kuwa: -

Matokeo yoyote yatakayotokea kuanzia sasa kuhusu kuvurugika kwa amani ya nchi yetu, ni vyema viongozi mliopo sasa wote wa serikali, CCM na jeshi la Polisi mtambue kuwa, nyinyi ndo mtakao kuwa washitakiwa wa kwanza katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu dhidi ya binadamu.

Jiandaaeni kukabili mashitaka ya uhalifu dhidi ya bindamu muda si mrefu. Damu mnayoimwaga sasa lazima itawarudia tu.
 
Viongozi wetu wameziba masikio yao kwa pamba,na wala hata hawataki tena kuuzingatia wosia minimum sana,alioutoa mwalimu Nyerere kuwa,tusijidanganye waTZ,kuwa tunaweza kuwa na amani milele,wakati misingi muhimu sana ya kudumisha amani hiyo tunaipuuza.

Miongoni mwa misingi hiyo,ni watawala kuongoza nchi kwa misingi ya haki,bila ya kufanya ubaguzi wowote ndani ya jamii.

Mfano mmojawapo,wa watawala wetu na c
vyombo vya dola kutotenda haki,ni pale Mwigulu Nchemba,alipohutubia mkutano wa kampeni huko Arusha,alipowaonya wakazi wa huko kuwa wakileta jeuri ya kuikataa CCM,kwenye uchaguzi wa msdiwani kuwa hakika watakufa.

Ingawa ni kweli,wakazi wa huko wamekufa kweli kwa kulipuliwa na bomu,hadi leo,jeshi la polisi limeendelea kumgwaya kumtia mbaroni,Mwigulu Nchemba,akiwa ni mtuhumiwa mkuu,kwa tukio hilo la bomu la Arusha.

Mfano mwingine ni kauli iliyotolewa na mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe,kuwa wanao ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa Polisi ndiyo waliorusha bomu hilo,ila wataweza kuupeleka ushahidi kwenye chombo huru,lakini siyo kuupeleka polisi,kwa kuwa wao ndiyo watuhumiwa wakuu,kauli ambayo ilimfanya kamishana Chagonja,wa jeshi la polisi,kuja juu na kusema,jeshi lao la polisi litamlazimisha Mbowe ili aupeleke ushahidi huo kwao.

Lakini Nape Nnauye naye alisema anao ushahidi kuwa Chadema wenyewe,ndiyo waliojilipua wenyewe kwa bomu.

Ingawa Nape naye ameukalia ushahidi huo na hajaufikisha polisi,lakini cha kushangaza hajatokea kiongozi yeyote wa ngazi ya juu jeshi hilo,aliyemlazimisha Nape,aupeleke ushahidi huo Pollsi!!
 
Back
Top Bottom