Ndoto ya mume wangu inatuumiza mioyo, hatuelewi

Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
7,689
8,844
Salaam.
Kwa wale walio Dar Es Salaam, hongereni na poleni kwa mvua.
Usiku wa kuamkia leo, mume wangu kaota ndoto ambayo kwakweli imetuacha vichwa vikiuma.
Ameota alikuwa anafanya mapenzi na shemeji yake (mke wa kaka yake) walikuwa wanafanya mapenzi hadharani kwenye garden huku watu wakishuhudia.
Baada ya hapo, akaanza kukiharishia, watu wakawa wanamshangaa.
Akashtuka usingizini huku akitweta Sana.
Kwenye ulimwengu halisi, huyo Dada, mke wa kaka yake yuko jela mwaka wa nne Sasa kwa kukamatwa na madawa ya kulevya.
Naombeni hekima yenu kwenye tafsiri ya ndoto hii
 
Inawezekana mchana alikuwa anamuwaza.
 
inaonyesha kuna jambo la fedheha lina kuja.

Awe makini.

ila kwenye hizi ndoto kuna upande wa pili yaani utatuzi alipewa mwambie akuambie ilivyoendelea awamu ya pili alionyeshwa nini?
 
Unachotakiwa kujua cha kwanza ni kuwa shetani anaweza kutumia lango la ndoto kupandikiza vitu vyake.
Unachotakiwa ni kuomba toba na kunyunyuzia damu ya Yesu katika lango la ndoto ili shetani asiweze kulitumia tena,
Maana ya kwanza ni kuwa
Ukiota ndoto unazini au unafanya uasherati na ndugu yako inamaana kwamba tendo la kusali limekufa kwako,
Ulikua unasali na kujikabidhi kwa Mungu wako lakini umeanza kupata ugumu katika swala la Kusali.
Maana nyingine ni kuwa
Umeunganishwa kiagano na pepo la uzinifu.[

Note: ukizini na mama yako au baba yako maana inabadilika, au ukizini na mnyama maana inabadilika.
Amen, ntashukuru Sana.
 
Hio ndoto ni ishara kuwa.
1. Huyo ndugu yenu aliyepo prison ataachiwa siku si nyingi na takuwa huru.

2. Akitoka jera ashauriwe kuwa makini maana linaweza kumsibu janga lingine.
 
Back
Top Bottom