Ndoto ya mke wangu imepunguza upendo na amani kwenye nyumba yetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndoto ya mke wangu imepunguza upendo na amani kwenye nyumba yetu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Humphnicky, Dec 6, 2011.

 1. Humphnicky

  Humphnicky JF-Expert Member

  #1
  Dec 6, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 1,808
  Likes Received: 526
  Trophy Points: 280
  Mke wangu mwezi uliopita aliota ndoto. Ndoto yenyewe ni hii:-

  eti alikuwa ameniudhi, kwa hasira nikamwambia utanikoma.
  Nikaondoka kwa hasira, niliporudi nikarudi na nyoka mkubwa sana aina ya cobra, akawa ananisihi nisimdhuru na huyo nyoka.
  Kwa hasira nikamuwekea huyo nyoka kwenye mkono wake.

  Nyoka akawa anamtafuna mkono na hakuwa na mtu wa kumsaidia.
  Watu wote walikuwa wakimshangaa, na mwishoni akasaidiwa na shehe mmoja.

  Tangu ameota ndoto hiyo upendo umeshuka sana ndani ya nyumba, hamna amani, muda wote ni mnyonge na hana raha kabisa.
  Muda wote amekuwa akibubujikwa na machozi na amepoteza kabisa hamu ya tendo la ndoa.

  Wapendwa naomba msaada wenu, je nifanye nini ili kurudisha furaha na upendo, pia imani na amani vilivyo potea??
  Je hiyo ndoto ina tafsiri au maana gani?

  Naamini JF ni kisima cha hekima nitapata msaada wa kutosha kutokana na busara na hekima zenu.
   
 2. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  huwa sijishughulishi kutafsiri ndoto, muhimu ni kufanya maombi kwa imani zenu. mumkemee shetani na kuharibu nguvu zake, na kurudisha uwepo wa Mungu kati yenu. mnaweza kuongea na kiongozi wenu wa dini pia kwa sala na ushauri,
  pole sana
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Dec 6, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,694
  Trophy Points: 280
  Pole sana sikutegemea kama ndoto zinaweza kuwa na athari kubwa namna hii. Nadhani ushauri aliokupa King'asti ni mzuri sana hivyo ufanyie kazi labda utarudisha hali ya hapo nyumbani kama ilivyokuwa mwanzoni kabla ya ndoto hiyo.
   
 4. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #4
  Dec 6, 2011
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Mzee, kama una nyumba ndogo uipige chini, sio njema kabisa waifu awe ananung'unishwa na vibanda vyako, maana na hilo joka laweza kuwa gono, kwa sababu mwisho lilitolewa, angeumwa hadi kufa tungesema ni ukimwi
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Dec 6, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Kwa elimu yangu ya Ndoto ni kuwa huyo nyoka kama ni Mkubwa ni dalili ya kuwa Mke wako ana Pepo mbaya ndani ya mwili wake na huyo Shetani ni dume huwa anamjia katika usingizini kwa njia ya ndoto. Na itafika wakati atakuwa akilala na wewe kwenye kitanda huyo mke wako atakuwa analala kwa ubavu kwa pembeni hataki muwe pamoja na wewe mtakuwa mnalala kitanda kimoja na

  hamfanyi tendo lenu la mapenzi tunaweza kusema ana shetani Mwanamme huyo mke wako itafika wakati hata kama utakuwa unafanya nae mapenzi atakuwa hajisikii raha ndani ya mapenzi yenu. Na atakuwa akiamka asubuhi mke wako atakuwa anajisikia kama

  kuumwa na kichwa kwa wakati mwengine atakuwa ni mchovu wa mwili kama vile aliyefanya kazi nzito wakati wa usingizini usiku. Nakushauri fanya hii dawa kwanza kwa muda wa kama siku 3 upate magamba ya vitunguu saumu uchanganye na maji kila anapolala
  usiku awe anajipakaa yale maji yaliyochanganyika na magamba ya vitunguu saumu ili kumfanya yule shetani dume amkimbie ili ndoa yenu idumu atumie hiyo dawa kwa muda wa siku kama 3 kila usiku anapolala ajipake hayo maji ya magamba ya vitunguu

  saumu kwa huo muda wa siku3. Na kama wewe na mke wako ni wakristo mpeleke kwa Mchungaji akamuombee dua la kama wewe ni Muislam mpelkee kwa Sheikh amuombee dua ili huyo shetani mbaya amtoke ndani ya mwili wa mke wako asante. Huo ndio ushauri wangu.
   
 6. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #6
  Dec 6, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  mmmhhh???
   
 7. ossy

  ossy JF-Expert Member

  #7
  Dec 6, 2011
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 877
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  pepo hilo mkuu! Kemeeni katika jina la imani yenu kaka!!!
   
 8. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #8
  Dec 6, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
 9. Humphnicky

  Humphnicky JF-Expert Member

  #9
  Dec 6, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 1,808
  Likes Received: 526
  Trophy Points: 280
  Amen, hakika ni pepo limejiinua.
   
 10. Humphnicky

  Humphnicky JF-Expert Member

  #10
  Dec 6, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 1,808
  Likes Received: 526
  Trophy Points: 280
  Mkuu, sina nyumba ndogo wala mwanamke wa pembeni
   
 11. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #11
  Dec 6, 2011
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Kimsingi mimi ninachifahamu ndoto ni ndoto na kwa kawaida ni reflection ya mambo au mawazo yaliyofanyika mchana uliopita. Ungejitahidi kumuelewesha mkeo kuwa hiyo ni ndoto tu na kamwe haina uhusiano na tukio lolote la kweli.
  Ukiona hali inaendelea nenda kwa viongozi wa dini wakusaidie.
   
 12. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #12
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  naanini kuna ndoto zina maana japom si kila ndoto ina maana, mwotaji hujua ndoto yenye maana kutokana na kuzongwa na ndoto hiyo.

  Kikubwa zaidi ya ndoto hizo ni maombi.
   
 13. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #13
  Dec 6, 2011
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  ulikuwa ni ushauri tu, wala sikuwa na nia ya kukutoa mapovu.
   
 14. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #14
  Dec 6, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Duuuuu!!!!!!!!
   
 15. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #15
  Dec 6, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mmmmh!ana haki ya kuogopa mie mwenyewe tu kwa kusoma nimeogopa mpaka nimetizama pande zote za hapa ofcn km kuna kitu!
  Nawashauri uende mkaombewe na kumkemea huyo pepo,
  Na muwe na utaratibu wa kufanya ibada fupi na kusali kabla ya kulala!
   
 16. Humphnicky

  Humphnicky JF-Expert Member

  #16
  Dec 6, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 1,808
  Likes Received: 526
  Trophy Points: 280
  huwa tunasali kila siku kabla ya kulala, lakini mwenzangu tangu aote ndoto hiyo hataki hata kusali na mimi.
   
 17. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #17
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  usimwadithie mtu ndoto yako ni hatari..by M Mpoto
   
 18. C

  CLEMENCY JF-Expert Member

  #18
  Dec 6, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 211
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mkuu, kwa upeo wangu wa kiimani, huyo ni pepo. Tafuta mchungaji wa ukweli mkaombewe kisha na nyie msimame katika neno.

  Mapepo huwa yanajiinua kwa njia nyingi. Kuna kitu kinaitwa affliction. Unaweza ukaota kakayo au mamayo au mtu yeyote unayemfahamu anakufanyia kitu kibaya. Ukamchukia na kumsema kuwa ni mchawi. Kumbe ni wachawi wanatumia sura ya huyo mtu katika kukutorment.

  Sali Zaburi ya 91 kila siku kabla ya kulala. Ni Zaburi ya ulinzi. Barikiwa sana
   
 19. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #19
  Dec 6, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ndoto ni reflection ya maisha ya mtu,sometimes huwa kama inakutaadharisha na jambo lijalo. Lakini pia huwa ni reflection ya yale uyawazayo. Vyovyote ilivyo tunashauriwa unapoota ndoto mbaya kemea imediately na uombe MUNGU akuepushie.
   
 20. Humphnicky

  Humphnicky JF-Expert Member

  #20
  Dec 6, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 1,808
  Likes Received: 526
  Trophy Points: 280
  asante sana kwa ushauri
   
Loading...