Ndoto ya Marehemu baba yangu inanitesa

UNIQUEMAN1

JF-Expert Member
Mar 20, 2018
378
448
Ni miaka 4 tangu baba yetu atutoke. Mara nyingi amekuwa akinitokea ndotoni. Alikuwa na kawaida ya kutuachia chakula au tukirudi kutoka shule anatuambia ingia ndani kwenye kabati kuna msosi mle.

Sasa, nimekuwa naota anatukusanya watoto wake anaanza kutupa maneno ya kuishi na watu vizuri n.k. Mara nyingine naota ndio anafariki na tunaenda kumzika kwa uchunguzi mkuu (na kiuhalisia ameshafariki since2016).

Jana nmeota tumechinjiwa nyama yake tukala . Nimeumia sana mpaka sasa sina furaha. Nifanyej nisimuote tena marehemu baba?

R. I. P mzee wetu, hakika ulitupenda ulitusomesha ilihali ulikuwa huna kitu. huku subiri matunda yako wote 7 uliowasomesha kwa kuuza kuni. Nilipata kazi tu ukafariki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Polee aiseee. Ila still kuna link kati yako na yeye.
Either kuna sombdy, spirit inatumia kivuli na taswila yake kuchukua attention yako, kupitisha Vitu ndani yako.

Some times watu wa rohon wakiona kuna ugumu kwako katik kuruhusu au kupokea kitu, huja na sura ya mtu unae mpenda na kumwamini sana, automatically nafsi yako itapunguza UKUTA ulioweka, na wao kufanya yao.

Aliyekufa ni kafa. Wafu hawajui lolote, ila kuna ishu mbili, wanataka advantage ya uhusiano wako wa na dingi yako. Wao wanakuja hivo. Au dingi alifanyiwa harakati yupo ktk dimension nyingine, kahamishwa.

Uliza ndugu zako kama wanapata ishu kama yako? Au angalia vutu gani strange vinvyo tokea misimu ya uotaji wa hizo ndoto, chunguza utapata muunganiko.

Kuna baadhi ya Makabila, mtu akifiwa na mtu aliye mpenda na kumwamin sana, wanajua huu mlango huwwza kutumika, so hufanyiwa mila, na wengine kugungwa Vitu flan flani vya dawa, kuzuia mashambuliz hayo.


Fight hiyo hali kwa imani yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu, kama ilivyo maana ya ndoto, ni marejeo ya mambo au matukio yanayotokea, kufanywa,kuzungumzwa, ama kufikiriwa sana na muhusika hasa kabla ya kulala, i know its hard lakini nakusihi punguza sasa kumfikiria sana mzee, ameshaondoka na hakuna namna ya kumrudisha kwenye huu ulimwengu wa nyama, kutokana na imani yako ebu jaribu kumkumbuka kwa dua/sala mbalimbali ili Mungu ampunzishe salama huko alipo, Ahsante.
 
Pole Sana ndugu ata Mimi nilifiwa na baba yangu mwaka huo huo Kuna kipindi nilikuwa namuota Sana unakuta naota kafa naota tuponaye msibani naota yupo kwenye maji machafu nilikuwa naota mambo mengi Sana kuhusu yeye Sasa hivi simuoti tena ile hali imepotea tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bebeni kitu au vitu alivyokuwa anapenda sana nendeni kaburini kwake mkafanye dua au misa au tambiko... Pateni ushauri wa wazee
 
baba yako kalala usingizi wa kifo ajui lolote la huku duniani
ndoto yako inaweza kuwa ni kutoka kwa mungu anakupa ujumbe litakalo tokea mbeleni,ivyo tafuta mtu wa kukutafsiria ,pia fanya maombi kama we mkristo,,au

roho chafu ambazo zimeshikiria ukoo wenu(mizimu) zinakuja kwa umbo la baba yako, mara nyingi hizi roho huwa zinakuelekeza ufanye mambo ambayo yanakuunganisha na kuzimu, kamwe hautafanya jambo lolote lililo jema machoni wa mungu..
 
Back
Top Bottom