flulanga
JF-Expert Member
- Jul 1, 2016
- 4,861
- 6,342
Wakuu habari..... Usiku wa kuamkia leo nimeota ndoto nimekufa nikajizika mwenyewe juu ya kaburi la mtu mwingine. Nikajiandaa mwenyewe hapo kaburini kwa kujilaza chali....... Ila jamaa yangu mmoja akaja kunitengeneza na kunigeuza na kunilaza kifudifudi. Ila kaburi lilikuwa na kina kifupi kwahiyo udongo ukuweza kunifunika mwilini so nilikuwa kama nimejilaza juujuu tu....... Kama nilivyotangulia kuandika hapo juu nilijizika juu ya kaburi la mtu mwingine.
Nilipo maliza kujihifadhi niliondoka na kuuacha mwili wangu pale umelala yaani ni kama vile nilikuwa na miili miwili...... Mwili mmoja niliuacha pale kaburini na mwingine ndio nilikuwa nao na kuondoka nao.
Wakuu hii ndoto ni mara ya pili naiota ndani ya mwezi huu mmoja. Kama kuna mjuvi wa mambo haya naomba uelewa TAFADHALI.
Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app