Ndoto: Usafi wa jiji la Dar chini ya mfumo wa madiwani labda mwaka 2025

Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,694
787
Ndugu,

Kama kuna kitu sikiamini ni kuongoza jiji la Dar es Salaam kwa kutumia madiwani. kwa hakika hii ndio price ya demokrasia. Kumbukeni jiji lilivyokuwa chini ya Keenja.

Nitoe mfano wa jambo moja tu nalo ni usafi!

Hivi unawezaje kumwambia mtu mchafu afuatilie usafi kwa wananchi wengine?

Mimi namwomba mheshimiwa Rais kwa kutumia vyombo vyake vya dola... awaambie watu wake wakapige picha za video za mazingira wanapoishi madiwani na wabunge wake wote wa Dar es Salaam...

Baada ya hapo ajiulize hivi jiji la Dar es Salaam linaweza kuwa safi likisimamiwa na watu ambao wenyewe ni wachafu?
 
Back
Top Bottom