Ndoto: Sehemu muhimu kwa afya ya hifadhi ya akili

Hata mm nilitaka kusema jamani kuna ndoto zingine ukiota ukija kushtuka unaogopa hadi kulala
Unajua ndoto zote zinatokana na sisi wenyewe... Yani huwezi kuota kitu ambacho hakipo hujawahi kukiona, hujawahi kukiwaza, kukisoma kukisikia ama kusimuliwa popote.... Sisi ndio mizizi na chanzo
 
Unajua ndoto zote zinatokana na sisi wenyewe... Yani huwezi kuota kitu ambacho hakipo hujawahi kukiona, hujawahi kukiwaza, kukisoma kukisikia ama kusimuliwa popote.... Sisi ndio mizizi na chanzo
Kwa hiyo hata nikiwa naoata nagegeda mimi ndio nimetaka iwe hivyo??

Maana nimeona umecomment kwamba kuota una gegeda ni matendo ya wachawi
 
Kwa hiyo hata nikiwa naoata nagegeda mimi ndio nimetaka iwe hivyo??

Maana nimeona umecomment kwamba kuota una gegeda ni matendo ya wachawi
Hapana ndoto hazina tafsiri moja... Ndoto zina connection na ulimwengu wa roho ambao uko vast n very deep
 
Wafu pekee ndio hawaoti na hawaoti kwakuwa hawana kumbukumbu tena na hawana kumbukumbu tena kwakuwa hawana uhai tena.

Kila binadamu kamili lazima awe na vivuli vitatu kukosa kuwa na vivuli vyote vitatu ni ulemavu wa kiroho sawa tu na kukosa kuota kabisa.

Ndoto za kawaida ni uchambuzi wa matukio ya siku nzima tuliyowaza kunena na kutenda, jana leo na mbeleni.

Ni katika mchakato wa kuchuja matukio ya kuhifadhi kwenye database ya ubongo ndio watu huota wakati huo mwili ukiwa katika dormance state. Ni vitu vinavyotokea bila ridhaa ya mhusika.

Mchakato mwingine wowote ufuatao wa ndoto za aina nyingine zile za wanga, wachawi, maono na taarifa msingi wake ni hizi ndoto asili ni katika mchakato wa huo wa kuchuja na kuchambua matukio ya kuchukua na kuacha ndio binadamu ama niseme kiumbe hai hupata mtimbwiliko uitwao ndoto.

Ni katika mnyambulisho huo wa matukio kunakuwa na matukio ya uhifadhi wa muda mfupi, muda wa kati na muda wa kudumu.

Matukio ya uhifadhi wa muda mfupi huishia katika mlango wa tano wa fahamu sawa na ndoto zake. Matukio ya muda wa kati huishia katika mlango wa sita sawa na ndoto zake. Angalia kuna ndoto za mwaka jana unaweza kuzikumbuka vizuri sana tofauti na ndoto za wiki iliyopita.

Vile vile na matukio ya kudumu huhifadhiwa kwenye mlango wa nane wa fahamu yakiwa yamechujwa hasa kwenye mlango wa saba na kuchambuliwa kwenye mlango wa sita matukio haya na ndoto zake huwa ni ya kudumu bila kujali umri wake.

Je ni kwanini kuna mchujo mkali kiasi hiki?

Chukulia database ya inavyowekewa ulinzi ili isiathiriwe na kirusi chochote.Basi hivyo ndivyo hali ilivyo kwenye software ya database ya ubongo.

Ubongo wako ndio data center, database ya kumbukumbu zako zote. Ukidisturb hiyo umekwisha.Vichaa na mwendawazimu huchezewa hapa, pakiguswa hapa ama pakiwa over loaded kuchanganyikiwa ni lazima.

Kwa ufahamu usiojua ni kwamba ndoto ndio maabara ya kupima kuchuja, kuchambua kuweka katika makundi husika aina za kumbukumbu za kutunzwa na ubongo. Asiyeota hana kumbukumbu na tafsiri yake ni moja tuu maabara yake haifanyi kazi.
Hebu niambie hii ni nini?
Kuna mazingira naweza kukutana nayo either ya kazi, kijamii au mapenzi. Lakini wakati tukio hilo likiendelea (lolote ktk mazingira niliyoyataja hapo), huwa nahisi kama linajirudia yaani najiwa na kumbukumbu yenye uhakika kabisa kuwa tukio hili lilishawahi kutokea.

Sometimes huwa najiuliza lilitokea wapi lkn faster napata jibu kuwa niliwahi kuota. Mara nyingi ni mambo yakawaida tu.
Kwamfano:
Nilikwenda Kigali, Rwanda last week na nimerudi Dar usiku wa juzi ijumaa (13/4/2018). Wakati tupo njia tukirudi (tukiwa upande wa Rwanda) dereva wetu alichoka sana, akaegesha gari eneo ambalo hapakua na maegesho, ilikua muda wa saa 6 usiku.

Tukakunaliana sote tulale japo dalika30 kwakua sote tulichoka. Kuna mtu tulimpa lift alikua anaenda kigoma, wenzangu walilala lkn mimi sikulala nilitoka nje ya gari nikawa nalizunguka kukagua mzigo na usalama wa gari japo SIHUSIKI NA HUO MZIGO, NA HATA UKIPOTEA SIULIZWI WALA SITAHUSIKA KWA LOLOTE ila wenye mzigo wamelala fofofo....!

Kulikua na wanyarwanda wakipita mojam1 kwa mbali, Baada ya masaa mawili (yaani saa8 usiku) nikawaamsha tuendelee na safari coz maeneo yale sikuyaamini kutokana na mazingira niliyokua nikiyaona nikiwa nje wakati wenzangu walilala ndani ya gari.

Tulipokua tutaendelea na safari ile tukio lote likawa linajirudia kwenye akili, yaani nikawa nalikumbuja kabisa kuwa lilishawahi kutokea.
Niligundua niliwahi kuliota baada ya kuwa na uhakika kuwa ilikua ni mara yangu ya kwanza Kwenda Rwanda.

Huo ni mfano mmoja tu, ila mengi nakutana nayo nilishayaota.
 
Hebu niambie hii ni nini?
Kuna mazingira naweza kukutana nayo either ya kazi, kijamii au mapenzi. Lakini wakati tukio hilo likiendelea (lolote ktk mazingira niliyoyataja hapo), huwa nahisi kama linajirudia yaani najiwa na kumbukumbu yenye uhakika kabisa kuwa tukio hili lilishawahi kutokea.

Sometimes huwa najiuliza lilitokea wapi lkn faster napata jibu kuwa niliwahi kuota. Mara nyingi ni mambo yakawaida tu.
Kwamfano:
Yeah mada hii ina jibu lako naomba rudia kusoma tena
 
Tafsiri ni Kwamba kuna Mahali kwenye Maisha yako Umekwama na Unahitaji Maandalizi ya Kifikra Ili uweze Kuvuka..

Swali la kujiuliza Ni Je?? Katika hiyo ndoto Kuna Watu gani?
Je Uko mwenyewe au uko na Wenzako?
Na Hao Ulionao Unawafahamu?

Kati ya Vitu ambavyo Tunapuuzia na Vinakwamisha maisha ya watu wengi ni Suala la Ndoto...

Na Kwa Maelezo ya Ndoto yako ni lazima Kuna Mahali kwenye Maisha yako Umekwama na Unatafuta kila namna Kutoka hapo na Huwezi...
Asante sana Nature kwa nyongeza iliyotulia
 
Nashindwa kupata jibu kwakua umesema ndogo ni matukio yaliyopita, ila mimi naanza ndoto halafu linakuja tukio husika, kama nilivyosema sikuawahi kufika Rwanda kabla lkn tukio lilitokea Rwanda nilishaliota.
Tuna replica katika maisha yetu... Wewe mko zaidi ya mmoja kiroho lakini mnashare server moja.. Lakini pia kuna kitu kinaitwa foreseer... Roho inakutangulia kukuletea matukio yatakayofanyika si kila mtu ana huu uwezo... Kwa msaada zaidi tafuta hiki kitabu A GIRL FROM TOMORROW
 
Kuota Unachapwa viboko tafsiri yake iko kwenye Biblia na imeandikwa...
"Tafsiri yake ni kwamba kuna Upumbavu ndani yako"

Kwa maana nyingine wewe ni Mpumbavu
Mpumbavu Siyo Tusi Kwa Mujibu wa Biblia...
Kwa Hiyo kuna Adhabu utakayopata Kutokana Na Upumbavu Ulionao...

Kwahiyo inategemea anayekuchapa ni Nani?

ni baba, kwa hiyo inamaana ntapata matatizo
 
Hapo Sawa..
Sasa kama weweni Mkristo uwe na Uhakika Ya Kuwa Kila ndoto Haijalishi Chanzo Chake ni Mungu au shetani Tafsiri Sahihi ya Ndoto Yako Inapatikana Kwa Mungu Katika Yesu Kristo....na Tafsiri sahihi Iko Ndani Ya Biblia.

Ndio Maana kila Mtu anayejaribu Kukutafsiria Ndoto ni Lazima Akupe Tafsiri iliyoko katika Biblia Na Si vinginevyo kwa Maana Hakuna Ndoto ambayo haina tafsiri ndani ya Biblia...

Narudia tena na Uamini ya Kuwa Hakuna Ndoto Ambayo Tafsiri yake haimo katika Biblia....
Tatizo ni kwamba watu wengi shetani Amewafunga Fikra zao hawajui siri na Hazina Iliyomo ndani ya Maandiko Matakatifu

Sasa turudi kwenye Ndoto yako ya Kuota Unachapwa Viboko...na Baba Yako
Mgongoni na Miguuni...Tafsiri yake ni Kwamba Kuna Adhabu inayokuja Kutoka Kwa Baba yako ambayo inasababishwa na Ujinga na Upumbavu wako...na Ukumbuke Mzazi anapokuchapa maana yake kuna Upumbavu na Ujinga ulioko ndani ya Mtoto...

Sasa haimaanishi kwamba baba yako atachukua Fimbo akuchape kwa namna ya kawaida..hapana ila kuna Adhabu itakayotoka kwa Baba yako..
Ndoto yako Tafsiri yake imo kwenye Biblia

Sasa itabidi usome biblia yako na Utafakari
Mithali 26:3

Halafu ukimaliza Usome
Mithali 22:5

Halafu Soma
Mithali 23:13-14

Halafu usome
Mithali 29:15
Soma na uitafakari kwa Makini hii mistari...
Asante sana Nature kwa masomo mazuri.. Nimejikuta nakuwa mwanafunzi
 
Mimi ninahistoria ndefu ila kuna ndoto zinanitatiza sana uwaga naota nipo kwenye nyumba polini kuna majani malefu nikichungulia nje nashindwa kutoka maana ata njia hamna ila nahisi kuna. Mtu mwingine ndani ila sijawai muona kila nikiota ndoto hiyo na nimeota kama mara 3 zinapishana atamiaka ila nakuwa kama kweli nipo alafu ni usiku hii inanimaanisha nini,ila ndoto zangu chache ndio zilinipa ukweli
 
Mshana mimi kuna ndoto zinaniuzi sana.
katika week lazima siku4 nitaota kama sio niko shule na wanafunzi niliosoma nao sekondari basi shule ya msingi.
Inanitesa sana na kielimu niliishia sekondari, saa zingine inaniathiri sana kwasababu sikutegemea kufail namna ile.. ila sio kila wakati nna mawazo hayo kusema ndio matokeo ya mawazo.

wakati mwingine napata maono navutwa na kitu nisichokiona na mara nyingi nakuaga siku nikillala na hofu sana,hilo jinamizi linanijia
 
Mshana mimi kuna ndoto zinaniuzi sana.
katika week lazima siku4 nitaota kama sio niko shule na wanafunzi niliosoma nao sekondari basi shule ya msingi.
Inanitesa sana na kielimu niliishia sekondari, saa zingine inaniathiri sana kwasababu sikutegemea kufail namna ile.. ila sio kila wakati nna mawazo hayo kusema ndio matokeo ya mawazo.

wakati mwingine napata maono navutwa na kitu nisichokiona na mara nyingi nakuaga siku nikillala na hofu sana,hilo jinamizi linanijia
Changamoto katika maisha yako ya kawaida zikoje!? Mahusiano kipato kazi nk!? Kwakuwa kwa ndoto za namna hiyo kuna ishara ya mikwamo mingi.. Most likely I am right
 
Back
Top Bottom