Ndoto isiyoelezeka ninapokuwa mgonjwa

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
21,318
50,531
Wasaalamu ndugu, nashindwa nielezee Kwa Maneno Gani Ila ninapokuwa Naumwa Aidha homa au mafua basi napata ndoto fulani ambayo sijajua ni Hisia Gani. Naota kama kuna vitu viwili vinakimbizana na havikamatani, Naota kama hivo vitu vinatakiwa vitimize lengo fulani Ila vinakuwa havitimizi vinaishia njiani na vinakuwa ni endelevu yaani vinaanza upya. Ndoto hiyo haitishi Sana Ila nakuwa katika mazingira mageni kabisa ni kama vile Ubongo unakimbia wenyewe Kwa speed ya JUU Sana. Ni kama kuna fumbo natakiwa nilitatue Ila najikuta natulia nikiamini Ubongo utafanya kazi wenyewe. Kipindi hicho Joto la mwili linakuwa kali Sana. Ni kama vidudu vinakimbizana Kwa speed isiyopimika.. Nashindwa kueleza Kwa Maneno mazuri ni hayo tu ndo nayokumbuka. Ndoto hio huwa haitishi Sana Ila ni lazima initokee hata mara nne - sita Kwa mwaka. Imewahi kukutokea?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom