Ndoto inanitabiria mabaya

Master SM

Member
May 29, 2020
55
54
Habari wanajamvi, naimani mko poa,

Moja kwa moja kwenye mada, Kuna kipindi niliota ndoto ya namna hiii, ndoto yenyewe ni ya shule yaani niliota Niko shuleni Advance, sikuwa na imani mbaya na ile ndoto mpaka ilipokuwa inajirudia.

Hapo ipinishtua nakuanza kuulizia maana yake ni ipi, majibu mengi nilioyapata ni kwamba kunadalili za kurudi nyuma kimaisha, asee huwezi amini sehemu ambayo nilikua nafanya biashara Mambo yalienda kombo mpaka stage ya kurudi kijijini.

Sasa baada ya muda Tena hali imejirudia mbaya zaidi nimeota nimerudi level za chini zaidi (latatu B) hali inayonifanya niwaze lipi linaenda kunikumba tena. Nakaribisha ushauri wenu wanajamvi.
 
P - ray
U - ntill
S - omething
H - appens

Omba, omba, omba, omba, omba kwa bidii, utahamisha kila mlima mbele yako.

Kwa kupata hiyo ndoto tu, nina imani una chembe chembe za kumfahamu Mungu ndiyo maana nimekuandikia nilivyoandika. Puuzia kuomba ushushwe kweli hadi hiyo la 3b.
 
Nje ya mada.

Kwani ukiota uko o level inamaanisha ndo kurudi nyuma kimaendeleo ya uchumi? Elimu? Siasa au mapenzi?
 
Unaanza upya sasa unaanza kuelekea juu upya.Kila la heri katika mafanikio yako
 
Maisha yetu hasa vijana kwa kiasi kikubwa tumeyafanya tukiwa shule, hivyo sio kitu cha ajabu kuota ukiwa shule ni vile ubongo una memorise tu.

Mfano mimi leo tu nimeota ndoto nimeajiriwa kama mwalimu shule Moja ya kanisa (hapo nimesomea ualimu na sina ajira rasmi). Nikashituka nilipolala tena nikaota nimerudi tena shule kama mwanafunzi ninayerudia advance.

Ukianza kuhusisha mambo ya ndoto na maisha utateseka sana.
 
Ndoto za hivyo ni mbaya Sana.

Hila kwa upeo wangu katika umri huu.

Ukipata changamoto nyingi, mbele Kuna mafanikio makubwa mnooo, amini 100%
 
Soma ISAYA 7:7 omba sana huku ukisimama katika andiko hilo kataa kila aina ya ndoto iliyo kinyume na mpango wa Mungu maana hata wachawi hutumia mlango huo wa ndoto kutimiza mambo yao, pia jiwazie mema kataa hiyo hali ya kushindwa usikubali kuangushwa au kurudishwa nyuma kataa kataa dear, amka saa tisa usiku sali maana anga linakuwa wazi na tulivu la ukishindwa fanya saa tatu , ukiweza pia funga hata tatu kavu huku ukiomba kwa kumaanisha hakika utavuka hapo
 
Maisha yetu hasa vijana kwa kiasi kikubwa tumeyafanya tukiwa shule, hivyo sio kitu cha ajabu kuota ukiwa shule ni vile ubongo una memorise tu.

Mfano mimi leo tu nimeota ndoto nimeajiriwa kama mwalimu shule Moja ya kanisa (hapo nimesomea ualimu na sina ajira rasmi). Nikashituka nilipolala tena nikaota nimerudi tena shule kama mwanafunzi ninayerudia advance.

Ukianza kuhusisha mambo ya ndoto na maisha utateseka sana.
Usidharau ndoto hata siku moja hapo mlango wa ajira unataka kufunguka ila kuna nguvu zinarudisha nyuma au kuzuia mlango huo kufunguka omba sana kemea hio ndoto utaona matokeo
 
Asante Sana kwa ushauri wako
Soma ISAYA 7:7 omba sana huku ukisimama katika andiko hilo kataa kila aina ya ndoto iliyo kinyume na mpango wa Mungu maana hata wachawi hutumia mlango huo wa ndoto kutimiza mambo yao, pia jiwazie mema kataa hiyo hali ya kushindwa usikubali kuangushwa au kurudishwa nyuma kataa kataa dear, amka saa tisa usiku sali maana anga linakuwa wazi na tulivu la ukishindwa fanya saa tatu , ukiweza pia funga hata tatu kavu huku ukiomba kwa kumaanisha hakika utavuka hapo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom