Ndoto 40 hatari tunazoota zenye maana maishani chukua hatua

Ramea

Ramea

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2015
Messages
1,411
Points
2,000
Ramea

Ramea

JF-Expert Member
Joined Mar 19, 2015
1,411 2,000
Mimi kutafsiri ndoto alinifundisha mzee wangu. Kwenye yote hayo umegusa moja tu, ishu ya kupanda mlima. Kupanda kwa shida au kuanguka mlimani, ghorofani, mtini.. hiyo ni ndoto yangu kuu inayonipa mwelekeo wa mafanikio au anguko kimaisha na huwa hivyo kwa 100%.

Ndoto nyingine alonifundisha mzee wangu kuwa ni mbaya na ndiyo inayo determine siku itaishashe ni kuota una sex na mtu ambaye si mwenza wako. Au kuona uchi wa mtu flan ndotoni. Hatariii. Siku nikiota ndoto kama hiyo siku inayofata kuna kamkosi nitaupata 150% bila chenga.

Nyingi hapo ni porojo, umefananisha tu matukio (lugha ya picha). Soma ndoto za kwenye biblia zilizotafsiriwa na kina YUSUF, hazikuwa za kiramli kama hizo zako. Nitaiandaa mada ya tafsiri za ndoto, siyo huo uongo wako.
 
goroko77

goroko77

Member
Joined
Jul 9, 2019
Messages
37
Points
95
goroko77

goroko77

Member
Joined Jul 9, 2019
37 95
Hii ya kula chakula na kufanya mitiani na kuota nifanya mapenzi had napiss hii inanisumbua na kunitezaa. Wacha nikaze maombi
 
F

FUSO

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Messages
15,896
Points
2,000
F

FUSO

JF-Expert Member
Joined Nov 19, 2010
15,896 2,000
Ukiota unapaa hatareeee, unavuka mito na bahari juu kwa juu
 
F

FUSO

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Messages
15,896
Points
2,000
F

FUSO

JF-Expert Member
Joined Nov 19, 2010
15,896 2,000
Hii ya kula chakula na kufanya mitiani na kuota nifanya mapenzi had napiss hii inanisumbua na kunitezaa. Wacha nikaze maombi
usilale kifudifudi....lazima utapizi tu sababu umelakia via vyako vya uzazi hasa kwa mwanaume.....
 
D

doughter

Senior Member
Joined
Jun 27, 2019
Messages
179
Points
250
D

doughter

Senior Member
Joined Jun 27, 2019
179 250
mi naotaga sana ndoto mbili moja ile ya kupaa angani ila sifiki popote ya pili naotaga naokota shilingi yaan pesa sarafu chini zinakua nyingiiii mia mia mia mbili ivo yaan ila ndo sielewagi maana yake izo ndoto anaejua anisaidie.
 
jay311

jay311

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2012
Messages
2,465
Points
2,000
jay311

jay311

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2012
2,465 2,000
NI UKWELI KABISA MFANO NAMBA 21 KWENYE MAMBO YA UZINZI UNAOTA UNANG'ATWA NA MBWA KAMA NIGHTMARE.
 
theohphilly

theohphilly

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Messages
246
Points
500
theohphilly

theohphilly

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2013
246 500
Ndoto ni muendelezo wa mawazo ukiwa umelala. Sema kipindi umemalala mwili unanafanya mmaamuzi ambayo sio consious.. Sidhani kama uancho sema ni sahihi..tukisema tufatilie kila ndoto tunazoziota tunaweza changanyikiwa
 
Adharusi

Adharusi

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2012
Messages
13,365
Points
2,000
Adharusi

Adharusi

JF-Expert Member
Joined Jan 22, 2012
13,365 2,000
Je nikiota chadema imechukua dola ni ishara ya nini
 
Aqua

Aqua

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2012
Messages
1,485
Points
2,000
Aqua

Aqua

JF-Expert Member
Joined Jul 23, 2012
1,485 2,000
SOMO: AINA YA NDOTO 800 HATARI AMBAZO UKIOTA UNAPASWA KUINGIA MAOMBI YA VITA.

Ukiota ndoto za namna hiyo hapo Juu yakupasa kuchukua Hatua za Kuomba Maombi ya Vita.
+255755554559 piga simu kwa maombi pia unaweza kutuma iyo ndoto yako kwa meseg WhatsApp
Na ukituma ndoto ili kupata tafsir jitambulishe kisha andika ndoto inayokusumbua

AINA YA NDOTO HATARI AMBAZO UKIOTA UNAPASWA KUINGIA MAOMBI YA VITA.

👉Kuota Unakunywa maji machafu(Ni ishara ya kupewa sumu katika ulimwengu wa roho na kuondoa moto wa Roho Mtakatifu)

👉 Kuota unakoroma na unalia kwa uchungu(Ni Ishara kuwa adui anapanda mateso juu yako)

1. Kuota kuna Vipingamizi vya kuzia usiendelee mbele( Ni Ishara adui anaweza Uzio kwenye Mafanikio yako)

2. Kuota unakula vyakula usiku (Ni Ishara kuwa umeunganishwa na mtandao wa kiuchawi)

3. Kuota unaoanda mlima kwa taabu sana( Ni Ishara kuwa adui anakufanya uhangaike sana kabla ya kupata riziki)

4. Kuota uko kwenye Mataa ya Barabarani( Ni Ishara kuwa pana Vikwazo vya kuendelea

5. Kuota umetumbukia shimoni (Ni Ishara kuwa adui ameshakuweka kwenye shimo fulani)

6. Kuota Upepo Mkali (Ni ishara Mungu qnakwambia Mbele kuna Vita)

7. Kuota unanyonyesha Mtoto wakati hauna mtoto(Ni Ishara kuwa kuna maadui wananufaika na wewe bila wewe kujijua)

8. Kuibiwa nguo kwenye ndoto(Ni Ishara kuwa adui anapanga kukuondolea Heshima na utukufi wako)

9. Kuota umebeba mzigo mzito (Ni Ishara adui amekubebesha mizigo mizito)

10. Kuota kofia yako imechukuliwa na upepo ( Ni Ishara ya kuaibishwa)

11. Kuota upo katikati ya giza nene( Ni Ishara ya Upofu wa Kiroho unakuvamia)

12. Kuota moto mkali unateketeza (Ni ishara ya mashambulizi ya Majanga kutokea)

13. Kuota unafanya mitihani ila hujamaliza karatasi zikakusanywa (Ni Ishara kuwa Roho ya Kufeli inakuandama)

14. Kuota Unasafiri ila hufiki unakokwenda(Ni Ishara adui anarefusha Mafanikio yako yasikufikie haraka)

15. Kuota umepigwa risasi ( Ni Ishara kuwa adui anakurushia mashambulizi)

16. Kuota umevaa nguo zilizochanika ( Ni Ishara ya roho ya Umaskini)

17. Kuota uko kwenye mazingira Yamezungukwa na Vinyesi ( Ni Ishara ya Kuwa Ibilisi anafanya kila awezalo kukuzia Usiende Mbinguni)

18. Kuota uko Uchi Ndotoni ( Ni Ishara ya kuaibishwa na kufedheheshwa)

19.Kuota umepoteza pete ya ndoa au gauni ya harusi ( Ni Ishara kuna Mpango wa Mashambulizi dhidi ya ndoa yenu)

20. Kuota mmevamiwa na kuibiwa ( Ni Ishara kuwa adui anapanga kuwaletea roho ya Umaskini au Ufakara na kupungukiwa)

21. Kuota umeumwa na Mbwa ( Ni Ishara kuwa roho za Uzinzi na Uasherati zinakutesa)

22. Kuota umeshambuliwa na Paka ( Ni Ishara ya Mashambulizi ya roho za Kichawi)

23. Kuota unashambuliwa na Nyoka (Ujue adui anakutegea Sumu)

24. Kuota umepoteza Fedha (Ni Ishara ya shambulio juu ya uchumi(

25. Kuota kuna mtu anakulaani. (NI ishara kuwa bado kuna misingi ya laana haijavunjwa juu yako)

26. Kuota unatokwa Damu puani na sehemu zingine za Mwili (Ni Ishara kuwa Kuna Mashambulizi juu ya Afya yako)

27. Kuota uko sokoni unazunguka na hauna kiti cha kufanya ( Ni Ishara kuwa roho za Ukichaa zinakunyemelea)

28. Kuota unafanya mapenzi Kwenye ndoto ( Ni Ishara kuwa unasumbuliwa na Roho ya jini Mahaba au Uzinzi)
Na pia ukiwa na haya hata maisha yako yanakua hayana ujasiri na unakua mtu wa hasira tu

29. Kuota umevaa nguo za Msingi wakati wewe ni mtu mzima sasa ( Ni shara ya Kudumaa kimafanikio)

30. Kuota Unakufa ( Ujue roho ya mauti ya Kiuchumi,kimwili kiafya inakuandama(

31.Kuota majeneza au Makaburi ( Ni Ishara ya roho ya mauti inafanyakazi)

32. Kuota unafukuzwa na Wanyama ( Ni ishara kuwa kuna Mashambulizi yalishaachiliwa juu yako katika ulimwengu wa roho)

33. Kuota Ndege Bundi au Popo ( Ni ishara kuwa unasumbuliwa na roho ya unafiki na masengenyo)

34. Kuota kuna Utando umekuzonga ( Ni ishara ya roho ya kukataliwa)

35.Kuota umepoteza Vyeti vya Shule ( Ni ishara adui anakuzuia usipate kazi)

36. Kuota umevaa Wigi Kwenye ndoto ( Ni Ishara ya utukufu Bandia juu yako)

37. Kuota makufuri ( Ni ishara kuna maeneo fulani juu ya maisha yako yamefungwa)

38. Kuota unalia ( Ishara ya roho ya huzuni)

39. Kuota Umeangusha Biblia au Umeshindwa kusoma Neno ( Ni Ishara kuwa adui anataka kuliondoa Neno juu yako)

40.Kuota unaogelea Kwenye Maji ( Ni Ishara ya majaribu yako mbele zako)

41.Kuota unatembea peku( Ni ishara ya roho ya umaskini na kwa wanandoa ni ishara ya Kuachana na mwenzi wako)

42. Kuota umevaa manguo Meusi au Kofia nyeusi ( Ni Ishara bado kuna utawqla wa Giza na Mapepo ndani yako)

43. Ukiota nyoka mweusi ni ishara ya ADUI mkubwa anakufuatilia.

Ukiota ndoto za namna hiyo hapo Juu yakupasa kuchukua Hatua za Kuomba Maombi ya Vita.


Na ukituma ndoto ili kupata tafsir jitambulishe kisha andika ndoto inayokusumbua

MBARIKIWE NA BWANA Mungu
Mkuu una maandiko yoyote kutoka kwenye biblia kusupport hayo uliyoandika hapo juu au ndiyo hekima za dunia?
Tunakosea tunapoweka limit ndoto hii maana yake ni hiki,hapo inaonyesha hatuhitaji msaada wa Mungu kutusaidia kujua maana ya ndoto tunazo ota.Mkuu unahitaji kujifunza kama wewe ni mtumishi wa Mungu.
 
Tayukwa

Tayukwa

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2014
Messages
1,078
Points
2,000
Tayukwa

Tayukwa

JF-Expert Member
Joined Dec 11, 2014
1,078 2,000
Kuamini sana tafsiri za ndoto hakuna tofauti na kuamini ramli za waganga wa kienyeji.

Halafu hii naona ipo kibiashara zaidi maana ameanza na kuweka namba zake za simu.

Kutokana na hali za maisha kwa sasa mindoto mibovu mibovu kama hii ni kawaida tu.

Chakufanya ikiwa umeota ndoto mbaya
1. Kwanza mlaani shetani, pia muombe Mungu akuepushe na ubaya kutokana na ndoto hiyo huku ukifanya kama ishara ya kutema mate mara tatu.
2. Babilisha upande uliolalia mwanzo. Kama umelala kushoto, hamia kulia na kinyume chake.

Cha kufanya Kama umeota ndoto njema yaani yenye kukufurahisha
Muombe Mungu akubariki kutokana na kheri za ndoto hiyo, pia muombe akukinge kutokana na shari ya ndoto hiyo.
 
Mchelle

Mchelle

Member
Joined
Mar 20, 2010
Messages
96
Points
95
Mchelle

Mchelle

Member
Joined Mar 20, 2010
96 95
Karibuni niliota napanda mlima mkali sana kwenda juu, ubaya zaidi hata ile miti ya kushikilia nikakosa kabisa. Nikawa nashika nyasi chache zilizoota kwenye mlima huo. Nilipoota hakukuwa na eneo lingine la kupita zaidi ya hapo. Nilibahatika kufika kileleni ila sikuwa na viatu, nikatembea peku hadi nikaja kukuta kijiji fulani huko mbele.
Hiyo nayo nini inaelezea??
 

Forum statistics

Threads 1,315,253
Members 505,171
Posts 31,851,499
Top