Ndosi mbona huondoki taasisi ya chakula na lishe, umesahau nini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndosi mbona huondoki taasisi ya chakula na lishe, umesahau nini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by maluluma, Mar 29, 2012.

 1. m

  maluluma Member

  #1
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]


  [h=2][​IMG]Tangu apate barua ya kuwa aondoke katika taasisi ya chakula na lishe yapata wiki mbili sasa Bwana Ndossi anaendelea kuzura zurura katika maeneo ya taasisi hiyo kwa kisingizio kuwa anafunga mizigo na kuandika ripoti. Wakati inafahamika kuwa mtu yoyote anapokaribia muda wa kustaafu miezi sita kabla anaandika barua ya kujulisha kuwa anastaafu na mara baada ya hapo anatakiwa aanze kujiandaa ili ukifika tarehe ya kustaafu anatakiwa kukabidhi ofisi kwa mtu mwingine aliyeteuliwa kuendelea na ofisi.[/h]
  Tatizo linalomsibu huyu bwana ni kuwa hakuwa tayari kustaafu baada ya kufikisha umri wake ambao pia hata umri alionao ameuchakachukua. Amehangaika sana kutafuta mkataba ili aongezewe kuendelea na ukurugenzi akidai kuwa hakuna mtu anafaa kumwachia nafasi. Aliomba kwa blandina nyoni swahiba wake bahati nzuri nyoni akapigwa panga. Bwana Ndossi alichanganyikiwa sana na akaanza hata kujiandaa maana alileta maboksi ya kufungia mizigo TAYARI KWA KUSTAAFU. Ghafla baada ya muda mufupi kama wiki mbili hivi baadaye akaacha kufunga mizigo yake kumbe alifaulu kumshawishi waziri wa afya ili amwongezee mkataba kwa mara nyingine. Tangia hapo akatangaza kutostaafu kwa kisingizio kuwa hakuna bodi ya kuachia madaraka. Lakini kauli hiyo ilikuwa ni janja yake ya kuendelea na vinono vya bure na vya dhuruma alivyozoea katika taasisi akijiamini kuwa Waziri angempa mkataba wa kuendelea kuongoza Taasisi hata kama amefikisha muda wa kustaafu na kusahau kuwa alisha chakachukua umri mara nyingi wakati alitakiwa kustaafu tangu 2001.

  Kwa asilimia mia moja alijua angepata mkataba. Ghafla akiwa na mategemeo makubwa sana tarehe 16/3/12 akapewa barua ya kufungasha kilicho chake na kuondoka ili kuachia ngazi na kwamba akabidhi taasisi kwa mwingine aliyeteuliwa na wizara kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasissi ya Chakula na Lishe Tanzania. Ukweli ni kwamba hakuamini na hajaamini kilichotokea. Ndio maana tangu itokee sinema hiyo ni takribani wiki mbili sasa anaendelea kufunga mizigo ambayo ihali alipashwa kuifunga muda wote wa nyuma alipokuwa madarakani . Kila siku anakuja ana zurura zurura katika eneo la taasisi akiweka kakitabu kamoja kwenye kaboksi. Kwa muda wote huu ana tumia ofisi ambayo anapaswa atumie mkurugenzi mtendaji mwenzake ili afanye kazi kuamsha taasisi iliyoko ICU. Kuna mashaka makubwa sana kuhusu huyu bwana maana wakati wa utawala wake alituhumiwa kuleta waganga wa kienyeji - Makalumanjila ofisini na sasa ameng'ang'ania ofisi. Je, hawaki tunguli ofisini ?

  Lakini pamoja na yeye kuendelea kuzura hapa ofisi katika kipindi ambacho mwenzake amepokea madaraka yapata wiki mbili hivi tayari kuna mabadiliko yameanzan kutokea. Mazingira ya taasisi yananzan kuwa safi kwa maana wakati wake alizuia fedha za kununuklia hata vitendea kazi vya kufanyia usafi; magari yanapeleka wafanyakazi majumbani yeye alipunguza mafuta na kusababisha baadhi ya magari kutopeleka wafanyakazi makwao na kuwaleta ofisi asubuhi; overtime zimerejeshwa zilikuwa zimezuiliwa na yeye. Ki ukweli kama mambo mengi yanafufuka sasa baada ya yeye kung'olewa. Ni vizuri sakiwa anaendelea kuzunguzunguka hapa ofisini ashuhudie namna mambo yanavyo amka ili ajue kuwa yeye alikuwa kikwazo cha maendeleo ya Taasisi na aone LIVE wenzake wanavyofanya vitu maana hata sasa hivi hata wafanyakazi wanajitolea sana mfano mzuri usafi wa mazingira ya Taasisi ihali yeye usafi ulikuwa ni kukata mti mmoja na kujilipa cheki nono.

  Hili pia lita kuwa ni fundisho kubwa sana kwa watendaji waroho, wababaishaji, wanyanyasaji, wasiopenda wafanyakazi, wabinafsi, wadhalimu, wanaobagua watu na kugawa katika makundi makundi badala ya kujenga umoja, kutoa haki kwa kuangalia sura, undugu, ukabila; kutoweka mbele maslahi ya umma. Huyu bwana aliwanyanyasa wafanyakazi waliodai haki zao halali, aliendekeza masuala ya double standards, kila safari ya nje hata isyohusu alienda kupata pesa tu na safari hizo hazikunufaisha taasisi, alitukana watu anavyotaka, alikuwa na majivuno, alitishia watu anavyotaka. Taasisi alioipokea 2003 ameididimiza kabisa, ameichakaza. Hakuihurumia hata kidogo kuwa watanzania wanaihitaji sana kwa afya zao; kuwa hata watoto siku moja wangeliajiriwa pale. FUNDISHO HILI NI KUBWA SANA KWAKE NA HATA KWA WAPAMBE, MASWAHIBA NA MASHOGA WAKE MAANA BADO WAPO WALIOKUWA WKIMSHAURI, KUMPA KIBURI, KULA NA KUNYWA NAYE.


  SOTE TUUNGANE SASA KAMA KITU KIMOJA, FAMILIA MOJA, TUIJENGE TFNC MPYA. KILA MOJA AITAMANI.
   
 2. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  kana majivuno sana hako kamzee ndossi
   
 3. M

  Mukalunyoisa Senior Member

  #3
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 139
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  jamani na sie mkurugenzi wetu ameshafikisha umri wa kustaafu tangu 2008 lakini hadi leo bado yupo ofisini ananyanyasa wafanyazaki tu ilihali yeye akilipa safari za nje zisizokuwa na tija.
   
 4. brazilian

  brazilian JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 607
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ninavyo mfahamu Ndosi alikuwa mwalimu wangu wa Biology mwaka 1976 hadi 1977 na nilimwacha Mkwawa High School wakati huo
   
 5. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Inabidi swala lipelekwe kwa kamanda Kova ili atume wale jamaa wa Ukonga (FFU), ndiyo wamtoe kwa nguvu.
   
 6. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Napita tu! Nitarudi baadae!
   
 7. Ba Martha

  Ba Martha JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2012
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  TFNC imechoka kulko taasisi zote za serikali...ni moja ya taasisi muhimu sana kwa maendeleo ya taifa lakini ni butu. Bahati mbaya Watanzania wengi hawajui umuhimu wa lishe hasa katika kuzuia vifo vya akina mama na watoto. Tafiti zinaonyesha asilimia 44 ya vifo vya watoto vinavyotokea Tanzania vinatokana na lishe duni...Ndossi ondoka watu wenye idea mpya waifufue TANZANIA FOOD AND NUTRITION.
   
 8. H

  Huihui2 JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Au Ndossi anashindwa kutoka kutokana na LISHE aliyoipata hapo ambapo hawezi kuopata popote tena
   
 9. bigcell

  bigcell JF-Expert Member

  #9
  Mar 31, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Au ni Edward Ngoyai Ndosi mi napita tu wanajamvi naenda kilabuni kupata kijeti fasts mara moja
   
Loading...