Ndoo zile zimejaa nini?

Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
5,149
4,674
Kwa wasafiri wa barabara ya Dar kwenda mbeya watakuwa wameona ndoo nyingi zimejazwa vitu vyeupe kando ya barabara kabla hujavuka mpaka wa Morogoro na Iringa. Mwaka mmoja uliopita kulikuwa na ndoo mbili tatu hivi lakini leo kuna msururu wa ndoo zimejaa vitu hivyo. Tafadhali anayejua atuambie,usikute ni bonge la biashara.
 
Ni kokoto kwa ajili ya terazo
 
Ni kokoto kwa ajili ya terazo

Nashukuru ndugu yangu kwa kunijulisha,yale maeneo siku za karibuni yameanza kuvutia wawekezaji wengi. Moja kuna campsite mbili eneo lile na ya tatu inajengwa barabarani kabisa,pili Wachina wanalima vitunguu pale kinoma. Nilivyoona vitu vinameremeta kwenye ndoo nikajua wachina wameshaanza kulamba bingo.
 
hauwezi kujua hao wachina wamevutika na vitunguu tu au kuna vitu vingine wanaokota kule milimani

Kimsingi,kuna dili zaidi pale,yale mawe yanaweza kuwa dalili njema ya kitu kingine nyuma yake.Tunaweza tukaamini kuwa terazo kumbe kitu kingine
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom