NDONDO CUP:- Mashindano ya uchawi kwa kisingizio cha mpira

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
75,193
157,336
Ndondo Cup ni mashindano yanayoandaliwa na Clouds FM kupitia kipindi chao cha michezo cha Sports Extra kinachoruka hewani kuanzia Saa Tatu usiku hadi Saa nne na kudhaminiwa na Dr. Mwaka

Mashindano haya yamegeuka kuwa mashindano ya uchawi hadharani na sio ya soka tena.
Watu wanafanya uchawi mchana kweupeeee.
Kuna machifu, wengine huingia hadi na ungo uwanjani.
Matukio ya kuvunja Nazi, mayai, Kupandisha mashetani nk vimekuwa ni vitu Vya kawaida mno.

Kwakweli mashindano haya yabadilishwe jina na kuwa Ndondo uchawi cup
 
Bujibuji hujaeleweka, siyo wote tuna muda wa kufuatilia cloud, hebu funguka kidogo, je wanaenda uwanjani au ni kipindi cha redio??
 
Kabla ya yote kwanza maudhui ya jina. Ndondo cup, binafsi nafarijika kama ubora najua upo mbeleni. Ni Jambo la kupongeza
 
Kuelewa watanzania tulivyo basi fuatilia ndo ndo cup

hakuna quality ya viwanja
kiwango cha mpira duni
lakini shindani linazidi kuwa marufu
Kweli mkuu yaani soka lao liko chini sana...nadhani wangeenda maeneo ya kilosa au ifakara au TPC wangeweza kupata vipaji vya soka hasa lakini hizi timu za ndondo ni chovu sana kulinganisha na umaarufu wanaopewa
 
Viwanja vinavyotumika ni vibovu mno. Angalau sehemu ya kuchezea mpira iwe na nyasi.
Wasiendekeze mambo ya uchawi. Hao ndiyo wachezaji wetu wa baadaye wa Simba, Azam na Yanga. Mambo ya ovyo yanaanzia huko.
Ajabu sasa kuna udhamini. Sasa utumike vizuri
 
Back
Top Bottom