Steve Dii
JF-Expert Member
- Jun 25, 2007
- 6,402
- 1,262
Ifuatayo ni tahiriri ya mhariri wa HabariLeo kuhusu timu ya ngumi Tanzania kushindwa kwenda kushiriki kwenye mashindano Amerika.
Ndugu Mhariri, walau ungetaja ni kiasi gani takribani tungeweza kuwa na upeo mkubwa zaidi katika unayoyasema na kulinganisha na mambo mengine mengi ambayo serikali inapanga na kuyafanya ndani ya miezi minne au mitano!
Kweli kabisa serikali yetu siyo ya kutegemea katika yote. Wakina Matumula na wenzake wanapopata nafasi na kushinda na kuiletea sifa Tanzania, serikali isijitie kimbelembele basi... (Mbona wanasoka wetu walikaribishwa hadi bungeni na kuchangiwa pesa kibao au ndondi ni mchezo wa vagi tu?!!).
Vyama gani hivyo?.. vague statement, again where is your credibility as an editor for the nation's newspaper?! Taja angalau chama kimoja na kuonyesha upeo wako, ili msomaji apate uelewo wa mambo unayoongelea. Na nakuomba ujitahidi kuandika vitu kutoka rohoni mwako na si kwa mashinikizo ya viongozi wa serikali. Lusekelo does it well and works under the same roof
Natamani kweli mtu ajitokeze kuwadhamini wanadondi wetu, natamani pia kuona wanashinda mashindano makubwa duniani na kuitangaza Tanzania yetu ila sifa zote zimwendee mdhamini wao na siyo serikali tena.
Sir/Madam, seems to me that you are confused na hujui la kuwaambia wasomaji wa gazeti. Kuwa na msimamo ndugu, kwa namna fulani unataka kuonyesha umakini na unachokiongelea, lakini kutokana na kubanwa na watu fulani unateleleka ghafla na kupoteza mwelekeo. Miye naamini kabisa kuwa kile ulichotaka kuandika hapo ilikuwa kuikemea serikali...ila ndiyo hivyo tena... umewapisha wababe, labda nisikulaumu sana!!
SteveD.
Source: HabariLEO.Serikali isibebeshwe mzigo kwa Ngumi kushindwa kwenda Marekani
Mhariri
HabariLeo; Saturday,October 27, 2007 @00:01
TIMU ya Ngumi imeshindwa kwenda Chicago, Marekani, kwenye mashindano ya Ngumi ya Dunia yanayoendelea.
Kushindwa kwa timu hiyo kwenda kwenye mashindano hayo ni jambo la aibu na la kusikitisha, kwa vile kitendo hicho kinahatarisha ushiriki wa Tanzania kwenye mashindano ya Olimpiki mjini Beijing, China, mwakani.
Wadau mbalimbali wa ngumi wamelizungumzia hilo na wengine kuitupia lawama serikali kwa timu hiyo kushindwa kwenda Marekani.
Sisi ni miongoni mwa waliosikitishwa kwa timu hiyo kushindwa kwenda Chicago kwa ajili ya mashindano hayo, yanayotarajiwa kumalizika mwanzoni mwa mwezi ujao.
Pamoja na hayo, hatuwaungi mkono wadau wanaoilaani serikali kwa kutoisaidia timu hiyo kwenda Marekani.
Jiulizeni, je, vyama mbalimbali vya michezo vina kawaida ya kuandaa kalenda yake ya mwaka? Huo ni utamaduni ambao haupo kwa vyama vyetu.
Pengine Ngumi ilikuwa na kalenda. Lakini, je, iliomba msaada muda gani? Maana haiwezekani kwa safari inayogharimu mamilioni ukaomba msaada miezi minne au mitano kabla. Mipango inatakiwa ianze kufanywa mapema.
Ni lazima wananchi na wanamichezo mbalimbali watambue kuwa serikali ina mambo mengi ya kufanya hivyo ni lazima iachiwe nafasi, kwa maana ya kuombwa msaada katika muda mwafaka.
Lakini pia serikali itafanya mambo mangapi? Tunadhani wakati umefika sasa kwa viongozi wa vyama mbalimbali, si ngumi pekee, kusimama kwa uwezo wao wenyewe badala ya kutegemea serikali na kuitupia lawama hata pasipostahili.
Tunachosema hapa ni kwamba viongozi wa vyama mbalimbali wanatakiwa kutafuta wafadhili na kubuni njia ya mapato ili kujiendesha badala ya kuitegemea serikali na kuitupia lawama kila kukicha.
Huu ndiyo wakati wake, kama inavyojulikana kuwa Agosti mwakani kutakuwa na michuano ya Olimpiki nchini China.
Muda huu ndiyo wa kuomba misaada, kutafuta wafadhili na vyanzo mbalimbali vya mapato ili hadi kufikia wakati wa mashindano, kusiwe tena na malalamiko ya kukosa nauli na baadhi ya timu kushindwa kwenda kwenye mashindano.